ZAIDI ya wanafunzi 50,000 watashindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu kutokana na kushindwa kupata mikopo kutoka katika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
 Hayo yamebainika ikiwa ni siku tatu tangu HESLB kutoa majina ya  wanafunzi waliofanikiwa kupata mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016,  huku idadi kubwa ikiwa haimo katika majina hayo.
 Katika mwaka huu wa  masomo bodi ya mikopo imeweza kuwapatia mikopo wanafunzi 12,000 pekee  sawa na 17.1% ya waombaji zaidi ya 70,000, hivyo kufanya idadi ya  wanafunzi waliokosa mikopo kufikia asilimia 82.9 ya waombaji wote.
  Wanafunzi waliokosa mikopo ya kuwawezesha kujiunga na elimu ya juu na  hivyo wazazi wao kutakiwa kugharamia elimu hiyo wameelezea kusikitishwa  na hali hiyo huku wakiitaka serikali kuwaangalia kwa jicho la kipekee  kwani hawana uwezo wa kuanza masomo pasipo kufadhiriwa na serikali.
  Wanafunzi hao walionekana kukata tamaa ya kutimiza ndoto yao ya kujiunga  na elimu ya chuo kikuu, wamefika makao makuu ya bodi hiyo huku  wakiongozana na baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi kutoka Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kutaka kujua hatima yao.
 “Nimetokea  Tabora, wazazi wangu walinipa Sh. 100,000 ya kutumia wakiamini tunapewa  mikopo na serikali, lakini tumenyimwa na hatujui hatima yetu, nimebakiwa  na Sh. 6,000, naomba serikali ituhurumie, isikie kilio chetu  hatustahili kuteseka hivi,” ameeleza Abdul Omary mwanafunzi mteule UDSM.
 Fatuma Bakari, mwanafunzi mwingine kutoka UDSM, amesema: “Siwezi  kujiunga na Chuo bila mkopo, tumefika hapa ili kuomba bodi ya mikopo  itusaidie hatuna tumaini lolote zaidi ya kuomba Mungu atusaidie tuweze  kupata mikopo na kuanza masomo.”
 Waziri wa Mikopo serikali ya  wanafunzi (Daruso), Shitindi Venance ameeleza kutokukubaliana na majibu  waliyopewa na uongozi wa juu wa bodi ya mikopo kwani yanakatisha tamaa  na kuzima ndoto za wanafunzi wa masikini kusoma chuo kikuu.
 “Hapa  UDSM ni wanafunzi 600 tu waliopata mikopo kati ya wanafunzi 7,000  waliopangiwa kuanza masomo, hili ni janga kubwa kwa watoto wa masikini  kwani hawawezi kujisajili chuoni wala kupata makazi katika mabweni mpaka  walipe ada na wengi wametoka mikoani.
 “Tunachukua hatua moja mbele  na kuamua kulifuatilia suala hili kwa katibu mkuu wa wizara ya elimu na  katibu mkuu wa wizara ya fedha kwa sababu bodi bado wanasisitiza tuwe na  subira ilihali muda umeenda na wanafunzi wanateseka” ameeleza Shitindi.
 Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole  amewaambia wanahabari waliofika ofisini kwake kuwa bodi haistahili  kulaumiwa kwani serikali kupitia wizara ya fedha na wizara ya elimu ndio  yenye uwezo wa kutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji ya wakati  husika.
 “Lengo la bodi ya mikopo ni kuwawezesha wanafunzi wa vyuo  vikuu kusoma kwa ufadhili wa serikali na wala sio kuwakwamisha,  tunaendelea kujadiliana na serikali kuona kama itatuongeza fedha ili  tuweze kutoa awamu ya pili ya majina ya wanafunzi waliopata mikopo,  tunawaomba wanafunzi wavute subira,” anaeleza Ngole
 Hata hivyo Ngole  amesema hawezi kusema lini watatangaza majina ya awamu ya pili kwani  hilo linategemea ni lini serikali itatoa fedha kwa ajili ya wanafunzi wa  awam ya pili.
 Katika mwaka uliopita wa masomo 2014/2015 serikali  ilitoa mikopo kwa wanafunzi 30,000 sawa na 51.7% ya waombaji wote 58,000  na hivyo kufanya waliokosa mikopo kuwa wanafunzi 28,000 sawa na 49%  pekee tofauti na mwaka huu ambapo waliokosa wamefikia asilimia 82.9
Showing posts with label BODI YA MOKOPO YA ELIMU YA JUU. Show all posts
Showing posts with label BODI YA MOKOPO YA ELIMU YA JUU. Show all posts
Subscribe to:
Comments (Atom)
- 
MAJIMBO YA ILALA, SEGEREA NA UKONGA – CCM ITAKUWA NA WAKATI MGUMU Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ipo kati ya Latitudo 6 na 7 kusini mwa I...
- 
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
- 
Shujaa wetu: Franz Wesinger-Mhandisi aliyejenga kanisa Katoliki Mbulu Kanisa la Mbulu ndilo kanisa kubwa kuliko yote Tanzania na la ...
 
