Wednesday, November 7, 2012
Bwana, Anatufundisha ,Nasisi Tusali.......
Zipo Silaha mbalimbali za Kiroho alizovaa Yohane Mbatizaji nazo ni Sala,.. kufunga na sadaka. Kwa leo tutafakari silaha ya kwanza: Ambayo ni
................SALA.....
Tumeitwa na Kirsto. Tumeitika wito wake. Hivyo, tunafanya kazi yake. Yeye alikuwa mtu wa sala. Aliwafundisha watu namna ya kusali kwa mafundisho yake na tendo halisi la kusali. Sisi kama wafuasi wake na tulioitika mwito wake wa kuwa viongozi wa taifa lake, tuige mfano wake. Katika tafakari hiyo, tusaidiwe na Yesu wa Mwinjili Luka.... Mwinjil Luka, anatilia mkazo mkubwa katika umuhimu wa sala. Kwa yakini, umuhimu huo unaonekana bayana. Kwanza jinsi Yesu aliivyosali mara nyingi. Pili, alivyowahimiza watu wasali. Tatu, jinsi alivyota mifano bora ya kusali.
Injili ya Luka inaonesha dhahiri kuwa kabla ya kuchukua hatua kubwa na muhimu, yesu anaanza kwa sala. Tuzitazame fasuli zifuatazo:
l1. Ubatizo wa Yesu (Lk 3:21-22)
Katika nafasi ya kubatizwa kwa Yesu, Luka anasema kuwa watu wote walipokuwa wamebatizwa, naye Yesu alibatizwa. Na alipokuwa anasali, mbingu zilifunguka, na Roho Mtakatifu alimshukia akiwa katika umbo la njiwa. Sauti ikasikika kutoka mbinguni: "Wewe ndiwe Mwanangu, nimependezwa nawe".
Hatua hiyo ya kubatizwa ilikuwa ya maana sana. yesu alithibitishwa kuwa Mwana tena mpenzi wa Mungu. Alijiunga na foleni ya wadhambi ili apokee ubatizo wa toba, toba iletaya ondoleo la dhambi. Lakini yeye hakuwa na dhambi. Alihakikishiwa kuwa njia aliyochukua yaani utume wake ilikuwa sahihi, na kwa kweli yalikuwa mapenzi ya Mungu.
l2. Yesu anawateua mitume kumi na wawili (Lk 6:12-16).
Tendo lilitanguliwa na sala. Yesu alikwenda mlimani kusali, akakesha huko usiku kucha akisali. Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, miongoni mwao akawachagua kumi na wawili ambao aliwaita mitume. Alijitenga na watu ili awe karibu na Mungu baba yake. Kwa hiyo, uteuzi wa mitume uliongozwa na Baba. Hatua hiyo ilibeba umuhimu mkubwa sana - kuwateua viongozi wanaofaa. tunasoma pia uteuzi wa mitume ukitanguliwa na sala katika Mdo 13:1-3. Katika kanisa la Antiokia kulikuwepo na watu wengine waliokuwa manabii na walimu. Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema: :Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi niliyowaitia." Basi, baada ya kusali na kufunga zaidi, wakawekea mikono, wakawaacha waende zao.
l3. Petro anamkiri Yesu Kristo (Lk 9:!8-20) Yesu alikuwa akisali peke yake na wanafunzi wake walikuwa karibu kabla hajaanza kuwauliza: :Eti, watu wanasema mimi ni nani?" Baada ya kutoa majibu mbali mbali, Yesu anawauliza wanafunzi wenyewe: "Ninyi je, mwasema mimi ni nani?" Petro kwa niaba ya wanafunzi wenzake alitoa jibu sahihi: "Wewe ndiwe kristo wa Mungu." Hiyo ilikuwa hatua kubwa, yaani azma ya Yesu kujua kama watu na wanafunzi wake wanamfahamu: Yeye ni nani na utume wake ni upi. Kumfahamu ni sharti muhimu ili utume wake uzae matunda.
Friday, November 2, 2012
LEO NI SIKU YA MAREHEMU WOTE DUNIANI....TUWAOMBEE!
MAKABURI YA CHINI YA ARDHI.
ANGALIA MAKABURI YA WENZETU YA NDANI, KATIKA VIMBA VIMBA!
Leo ni siku ya marehemu wote duniani, kila ifikapo tarehe 02/11 tunawakumbuka wapendwa wetu wote waliotutangulia mbele ya haki. Kwa namna ya pekee nimepata nafasi ya kutembelea makaburi ya hapa Cesena leo mchana huu, ambapo nimeenda kusali na kuwatembelea marafiki ambao tayari walishatutangulia mbele ya haki. Ili kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu apende kuwaweka miongoni mwa wateule wake mbinguni, na kama bado wanayo mapungufu ya dhambi zao basi waweze kutakaswa, ili hatimaye waonje pendo na huruma ya Mungu.
Ibada za kuwaombea marehemu zinafanyika katika kila Parokia.....na katika maeneo ya makaburi......
Thursday, November 1, 2012
JIPANGE NA Rio de Janeiro, Brazil
Home > Youth > 7/25/2012 8:56:32 AM
Maonesho ya shughuli za miito mitakatifu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, kwa mwaka 2013, huko Rio de Janeiro, Brazil
Maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa huko Rio de Janeiro, Brazil kwa Mwaka 2013 yanaendelea kwa mwendo kasi wa kuhamasisha mashirika ya kitawa na kazi za kitume, yanayotaka kushiriki katika maonesho ya shughuli na utume wao miongoni mwa vijana, kujiandikisha kuanzia sasa, ili kuwawezesha kushiriki katika Maonesho ya Miito wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa kwa Mwaka 2013.
Lengo ni kuendelea kuhamasisha miito mbali mbali ndani ya Kanisa kwa kutambua kwamba, mavuno ni mengi lakini watenda kazi katika shamba la Bwana ni wachache.
Maonesho haya yanatarajiwa kuwekwa katika eneo la kitalii mjini Rio de Janeiro, kwa lengo la kutaka kuwahamasisha vijana kuchangamkia wito na maisha ya kipadre na kitawa; kwa kujitoa kimasomaso kwa ajili ya Mungu na jirani zao. Maonesho haya yatakuwa na matangazo ya maneno kutoka kwa watakatifu mbali mbali ambao wamekuwa na mvuto wa pekee katika maisha na utume miongoni mwa Vijana.
Kamati ya Maandalizi inabainisha kwamba, kutakuwepo na shuhuda, mahubiri, michezo na matamasha ya muziki rasmi kwa ajili ya vijana. Lakini, nafasi kubwa zaidi itatolewa kwa vijana kupata nafasi ya kusali, kutafakari na kushiriki katika maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu kwa kutambua kwamba, Ekaristi ni chimbuko la miito mbali mbali ndani ya Kanisa. Vijana watapata nafasi ya ukimya na kuabudu Ekaristi Takatifu kwani Mwenyezi Mungu anapenda kuzungumza na mtu kutoka katika undani wake.
Baada ya vurugu na makelele ya maisha, kijana anahitaji muda wa ukimya na tafakari ya kina, kuhusu hatima ya maisha yake bila kusahau uhusiano wake na Mwenyezi Mungu pamoja na jirani wanaomzunguka. Ili kweli maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa yaweze kuzaa matunda yanayokusudiwa, yaani toba na wongofu wa ndani kama sehemu ya mchakato wa kukumbatia hija ya utakatifu wa maisha, vijana watapata fursa ya kujipatanisha na Mungu pamoja na jirani zao, katika mahema maalum yaliyotengwa kwa ajili ya Ibada hii.
Wakati wote huu, Familia ya Mungu, Jimbo kuu la Rio de Janeiro, itaendelea kushiriki bega kwa bega na mahujaji hawa kutoka sehemu mbali mbali za dunia, kama njia ya kuonesha upendo, ukarimu na mshikamano wao na vijana; wanaopaswa kupendwa, kuheshimiwa na kuthaminiwa katika maisha, matumaini, shida na mahangaiko yao ya kila siku. Mashirika ya Kitawa na Kitume, Jimboni humo, yanayo fursa na mwanya wa pekee wa kushirikisha karama na utume wake miongoni mwa vijana.
Ushiriki wa Mashirika haya kwanza kabisa, utategemea uwepo wake nchini Brazil, umuhimu wa Mashirika haya sehemu mbali mbali za dunia na Sheria za Kanisa zitakuwa ni mwongozo muhimu wa kuchagua Mashirika yote yatakayopania kujiunga na Maonesho ya shughuli za miito wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, huko Rio de Janeiro, Brazil.

Wednesday, October 31, 2012
MAZISHI YA PD:MASSAWE HUKO TOSAMAGANGA IRINGA
Mkuu wa Shirika la Consolata Tanzania amezikwa jana huko Tosamaganga Iringa
Picha
inayoonekana ni marehemu Padre Salutaris Lello Masawe aliyekuwa Mkuu wa
Shirila la Wamisionari wa Consolata Tanzania ambaye amezikwa leo katika
makaburi ya Jimbo la Iringa yaliyopo Tosamaganga. |
Add caption |
Wakristo Wakatoliki wameshauriwa
kujiuliza kuwa wanahusiana na wengine vipi kama
ishara ya kujiandaa kuufikia uzima wa milele mbinguni.
Hayo yamezungumzwa leo na Askofu
wa Jimbo Katoliki la Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa alipokuwa
akihubiri wakati wa Misa ya Mazishi ya Padre Salutaris Lello Massawe
ilifofanyika katika Kanisa la Moyo Mt. wa Yesu Parokia ya Tosamaganga jimboni
humu.
Amesema binadamu hataulizwa
endapo alitenda matendo ya upendo bali ataulizwa kama
alikuwa na roho ya ubinadamu na haki katika kuwajali wengine.
“Swali la kujiuliza kila wakati
katika maisha ni kwamba, umehusiana na watu wangapi wakakubariki? Na tena
hatutaulizwa endapo tulitenda upendo bali tutaulizwa kama
tulikuwa na roho ya ubinadamu na haki katika kuwajali wengine” amesema
Amesema Mungu ana mzaha katika
kuvichukua viumbe wake kwani huchukua muda anaoutaka ambao binadamu haujui
lakini jambo la msingi ni kujiandaa kiroho ili kuwa tayari wakati wowote.
“Munu ana mzaha pia. Mzaha
wenyewe ni kiama huu ambao kila mtu anajiuliza kwa nini Massawe ameondoka
wakati ambao hakutarajiwa? Kila mtu anajiuliza, kwa nini mapema? Kwa nini
ghafla? Huo ndiyo mzaha wenyewe ila yeye anajua kila mtu atamchukuaje na kwa
wakati gani” amesema.
Akimzungumzia Massawe Mhashamu
askofu Ngalalekumtwa amesema alikuwa ni mtu mwenye bidii, uaminifu katika
kuwajibika na alikuwa na maneno ya kutia moyo.
“Kazi za kitume alizitenda kwa
bidii na kwa uaminifu. Pia alikuwa na maneno ya kutia moyo. Aliadhimisha
matendo ya wokovu kwa nidhamu. Tunaimani kabisa kuwa huko alikokwenda ni
kuzuri” amesema.
Amewataka Wakristo kuwa ni watu
wa kutenda haki na kujituma katika kuwasaidia wanaohitaji msaada kwa kutenda
matendo ya upendo wakijua kuwa maisha ya mwanadamu ni safari ya kumtafuta
Mungu.
“Tendeni matendo ya haki, matendo
ya upendo kwa kuwasaidia wahitaji kwa kujua kuwa safari ya mwanadamu ni
kumtafuta Mungu; binadamu kajaliwa moyo mkubwa wa kuweza kumwelekea Mungu”
amesema.
Mazishi hayo yalihudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa serikali na madhehebu ya kidini kutoka ndani na nje ya
nchi ambapo jumla maaskofu wanne walihudhuria mazishi hayo.
Maaskofu hao ni pamoja na
Mhashamu Desderius Rwoma wa Jimbo Katoliki la Singida, Mhashamu Alfred Maluma
wa Njombe, Mhashamu Evaristo Chengula wa Mbeya pamoja na Mhashamu Tarcisius
Ngalalekumtwa wa Iringa ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania..
Tuesday, October 30, 2012
NAFASI NYINGINE TENA KWETU...
Vijana wasanii waalikwa kujiandikisha kwa ajili ya matamasha ya WYD 2013
Vijana kutoka pande zote za dunia , watakusanyika huo Rio de Janeiro kwa ajili ya kushiriki kaitka adhmisho la Siku ya Vijana a dunia , itakayo fanyika Julai mwakani. Vijana hayo si kwamba watakuwa mahujaji tu lakini pia iatkuw ni nafasi kwa vijana kuifahamisha dunia juu ya uwezo wao katika sanaa, tamasha za kuigiza , michezo, ngoma na muziki. Kwa ajili hiyo, hapo tarehe 15 Desemba 2012,wale wanaopenda kushirki wanaweza kuanza kujiandikisha. Uadikishaji huo umetengwa katika makundi matatu , Muziki, wachoraji wa sanaa na tamasha. Masharti ya kujiunga katiak vikundi hivyo yametolewa kwamba, wale wanao penda kushiriki katika tamasha la sanaa , utendaji wa onyesho lao ni lazima uonyeshe sura ya mafundisho ya kanisa na ubora wa sanaa. Na kwa wanamuziki , muziki huo ni lazima, uendane na mapokeo na mafundisho ya kanisa Katoliki, ingawa kila kikundi kitatenda na kuimba kwa mahadhi ya utamaduni wao. Na kwamba , baada ya makundi yote yanayotaka kushiriki kujiandisha, waandaaji wa WYD, watachagua vikundi vitakavyoshiriki katika matukio hayo na vitatangazwa March 13 2013. Nwa kwamba, Sherehe hizi za sanaa , hazitaingiliana na Katekesi zitakazo kuwa zikitolewa na matukio mengine yaliyoandaliwa rasmi kwa ajili ya WYD. Lengo la maonyesho ya kisanii, ni kuanzisha mazungumzano kati ya imani na tamaduni, na asili yake ni tangu mwaka 1997. Fomu za kujiandikisha zinapatikana katika tovuti ya CLICK HAPA http://www.rio2013.com/en

BURIANI PADRE LELO MASSAWE
Mwili wa Mkuu wa Shirika la
Wamissionari wa Consolata, nchini Tanzania, Padre Salutaris Lucas Massawe unazikwa leo katika Parokia ya Mshindo mkoani Iringa.
Padre Massawe, alikufa kwa kuzama baharini Oktoba 25 katika ufukwe wa Bagamoyo mkoani Pwani.
Padre massawe na mapadre wenzake washirika la consolata kutoka mataifa mbali mbali barani afrika walikwenda Bagamoyo kupumzika baada ya mkutano wa wakuu wa
Shirika la Waconsolata Barani Afrika, uliokuwa unafanyika consolata mission centre bunju, Jiji la Dar es Salaam.
Septemba 7, 2011 alichaguliwa kuwa Mkuu wa Shirika la Waconsolata
nchini Tanzania hadi alipokufa Oktoba 25, 2012.
Kabla ya kuwa mkuu wa shirika hilo, Padre Massawe alifanya kazi za umissionari katika nchi za Ethiopia na Italy.
HISTORIA YA MAREHEMU
Marehemu Padre Salutaris Massawe alizaliwa tarehe 8 Julai 1962, katika kijiji cha kibosho wilaya ya moshi vijijini.
Alisoma shule ya Msingi
Singachini kuanzia mwaka 1971 hadi mwaka 1978
mwaka 1979-1985 alikuwa akisoma katika Sekondari Maua Seminari iliyoko mkoani kilimanjaro.
Aliendelea na masomo ya Falsafa na Taalimungu kwenye Chuo cha
Waconsolata kilichoko mjini Nairobi kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1988.
Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, kunako tarehe 27 Juni 1993 alipewa daraja takatifu la Upadre katika kanisa la Kristo Mfalme na Askofu Amedeus Msarikie wa Jimbo la Moshi wakati huo.
Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, kunako tarehe 27 Juni 1993 alipewa daraja takatifu la Upadre katika kanisa la Kristo Mfalme na Askofu Amedeus Msarikie wa Jimbo la Moshi wakati huo.
Mungu alimpa maisha ya duniani na sasa amemwita, ili ampe maisha ya mbiguni yasiyo na mwisho....
Raha ya milele umpe, ee bwana...
na mwanga wa milele umwangazie
apumzike kwa amani
amina,
Wednesday, October 10, 2012
.Bikira Maria anapewa heshima zaidi
Bikira Maria kati ya Waorthodoksi
Kwa kiasi kikubwa imani ya Waorthodoksi kuhusu Maria inalingana na
ile ya Wakatoliki, ingawa hawakubali jinsi baadhi ya dogma hizo
zilivyotangazwa na jinsi zinavyofafanuliwa.
Bikira Maria katika Uprotestanti
Martin Luther alipoanza Matengenezo ya Kiprotestanti aliandika kwa heshima juu ya Bikira Maria, lakini kadiri mabishano yalivyozidi kati ya madhehebu ya Kikristo, Waprotestanti walizidi kupinga mafundisho ya Kanisa Katoliki juu ya Mama wa Yesu. Siku hizi baadhi yake, hasa Waanglikana na Wamethodisti wanamrudishia Maria nafasi yake kama kielelezo cha imani na cha kupokea neema ya Mungu.
Bikira Mariamu katika Uislamu
Kurani inamtaja mwanamke mmoja tu, tena mara 34: ni Mariamu, mama wa nabii Isa. Akichanganywa na dada wa Haruni na Musa, aliyekuwa na jina hilohilo, anatajwa kama binti Imrani. Pia habari nyingine kadhaa zinapishana na zile za Injili.
Hata hivyo anapewa heshima ya pekee, kama inavyoonekana katika sura
ya 3:43: “Na kumbukeni malaika waliposema, ‘Ewe Mariamu, kwa hakika
Mwenyezi Mungu amekuchagua na kukutakasa na kukutukuza kuliko wanawake
wa walimwengu”. Tena katika aya 3:46: “Na kumbukeni waliposema malaika:
‘Ewe Mariamu, bila shaka Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za Neno
litokalo kwake, jina lake Masihi Isa mwana wa Mariamu, mwenye heshima
katika dunia na ahera, na yu miongoni mwa waliokaribishwa’”.
Aliambiwa amefanywa “ishara” pamoja na mwanae, ingawa haisemwi ni
ishara ya nini. Sura ya 19, yenye jina lake, inaeleza kwamba Malaika
Jibrili (Gabrieli) akimpasha habari ya mimba alisema, ‘Hakika mimi ni
mjumbe wa Mola wako ili nikupe mwana mtakatifu’.
Akasema, ‘Ninawezaje
kupata mtoto hali hajanigusa mwanamume yeyote, wala mimi si mwasherati?’
Akasema, ‘Ni kama hivyo; Mola wako amesema: Haya ni rahisi kwangu, na
ili tukufanya ishara kwa mwanadamu na rehema itokayo kwetu, na ni jambo
lililokwisha hukumiwa’ ” (19:19-21). “Na mwanamke yule aliyejilinda tupu
yake na tukampulizia roho yetu na tukamfanya yeye na mwanawe ishara kwa
walimwengu” (21:91).
Pamoja na kusifiwa kwa usafi wake, anaongezewa sifa za imani na
unyenyekevu: “Na Mariamu binti Imrani aliyejilinda uchi wake, na
tukampulizia humo Roho yetu na kayasadikisha maneno ya Mola wake, na
vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu” (66:12).
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...