Wednesday, March 13, 2013
Tamasha 2011
HICHI KILIKUWA KIKOSI CHA TIMU YA KIGANGO CHA BOKO - 2001
NA HII NDIYO ILIKUWA TIMU YA KIGANGO CHA BUNJU KWA MWAKA 2011
Tuesday, March 12, 2013
Makardinali wanaoingia kwenye Conclave mjini Vatican
Jiografia ya Makardinali wanaoingia kwenye Conclave mjini Vatican
Wakati huu wa uchaguzi wa Papa Mpya jambo la msingi kukumbuka ni kwamba, Kanisa ni moja, Takatifu, Katoliki, na la Mitume. Makardinali katika mwelekeo wa mawazo yao ya jumla wamebainisha kwamba, wanataka kumchagua Kiongozi mkuu wa Kanisa atakayeliongoza Kanisa la Kristo kama Baba mwenye huruma na mapendo, kielelezo cha umoja na mshikamano wa Kanisa; kiongozi mwenye dhamana ya kulinda na kusimamia kweli za Kiinjili, Maadili na utu wema. Haijalishi mahali anapotoka mtu, jambo la msingi ni kiongozi.
Kwa jumla, kuna Makardinali 115 wenye haki ya kupiga na kupigiwa kura wanaoanza mchakato huu kwenye Kikanisa cha Sistina kwa kula kiapo, tafakari ya Neno la Mungu na uchaguzi wa kwanza. Makardinali 60 wanatoka katika nchi za Ulaya, kuna Makardinali 33 kutoka Amerika, Makardinali 11 kutoka Barani Afrika, Asia kuna Makardinali 10 na Oceania kuna Kardinali mmoja. Itakumbukwa kwamba, kwenye Conclave ya Mwaka 2005, Kenya haikuwa na Kardinali, lakini mwaka huu, Kardinali John Njue yupo.
Kuna Makardinali 40 ambao wametekeleza utume wao au bado wanaendelea kufanya shughuli mbali mbali mjini Vatican. Kati ya Makardinali wenye haki ya kupiga na kupigiwa kura 67 ni wale walioteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita.
Wastani wa umri wa Makardinali wanaopiga kura ni kati ya miaka 71. Kardinali Walter Kasper mwenye umri wa miaka 80 ni kati ya wale waliobahatika kuingia katika Conclave wakiwa na umri mkubwa zaidi. Kati ya Makardinali vijana wana umri wa miaka 54 na 56. Kardinali Luis Antonio Tagle ana umri wa miaka 56.
Mwishoni, itakumbukwa kwamba, kundi la Makardinali Maaskofu lina Makardinali 6; Kundi la Makardinali Mapatriaki lina jumla ya Makardinali 4; Kundi la Makardinali Mapadre lina jumla ya Makardinali 153 na Makardinali Mashemasi wako 44. Kuna jumla ya Makardinali 207.
Hatua za mwisho mwisho(PAPA)
Hatua za mwisho mwisho kabla ya Papa Mpya kutokeza hadharani!
Padre Federico Lombardi msemaji mkuu wa Vatican anabainisha kwamba, uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro unakamilika kwa Kardinali kupata theluji mbili ya kura zote halali zilizopigwa. Baada ya hapo, Dekano wa Makardinali ambaye wakati wa uchaguzi ni kardinali Giovanni Battista Re, atamuuliza Kardinali aliyechaguliwa kama anakubali kisheria kwamba, amechaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.
Baada ya hapo, ataulizwa jina ambalo atalitumia katika utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Wakati wote huu, Mshehereheshaji mkuu wa Papa ndiye atakayekuwa anachukua rasmi taarifa zinazotolewa na Papa Mteule akisaidiwa na Washereheshaji wengine wawili wanaokuwepo mahali hapo kama Mashahidi. Seehemu hii ya mchakato ikikamilika, hapo karatasi zilizotumika kwa ajili ya kupigia kura zinachomwa na hapo moshi mweupe unatoka kuashiria kwamba Kanisa limempata Papa Mpya.
Papa Mpya ataelekea kwenye "Chumba cha machozi" neno ambalo pengine linaonesha ile hali ya ndani anayokuwa nayo Kardinali baada ya kuambiwa kwamba, amechaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Anaporudi kwenye Kikanisa cha Sistina, Injili inayozungumzia Ukulu wa Mtakatifu Petro inasomwa, Makardinali wanasali kwa kitambo kidogo na hapo Makardinali moja baada ya mwingine wanaanza kwenda kula kiapo cha utii kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro, wakati wote huu, Makardinali na Papa wanaendelea kumshukuru Mungu kwa kuimba utenzi wa shukrani, Te Deum.
Padre Lombardi anasema, Papa Mpya kabla ya kwenda kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kutoa baraka zake kwa mji wa Roma na Ulimwengu kwa ujumla, "Urbi et Orbe" atapitia kwanza kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Paulo kusali kwa kitambi kifupi na baadaye atawasalimia na kuwapatia baraka zake za kitume waamini, mahujaji na wote watakaokuwa wamekusanyika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro. Papa mpya ataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kusimikwa kwake, siku yoyote inayoonekana inafaa zaidi!
Monday, March 11, 2013
- JUMATANO TAREHE 13/03/2013
2.JUMAMOSI TAREHE 16/03/2013
Vijana wote wa Parokia tutashiriki katika Hija ya Vijana wa Jimbo la Dar es salaam itakayofanyikia Bagamoyo.......Usafiri utafika Vigangoni saa moja asubuhi tayari kwa safari...
JUMAPILI TAREHE 17/03/2013
RATIBA ZA IBADA ZA MISA TAKATIFU
KIGANGO CHA BOKO.
MISA YA KWANZA 12:30-2:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA TATU SAA 4:00-5:30 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI
MISA YA KWANZA SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 4:00-5:30 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL-MBWENI MALINDI
SAA 2:00-4:00 ASUBUHI.
KIKAO CHA HALMASHAURI YA WALEI PAROKIA
KIKAO CHA HALMASHAURI YA WALEI PAROKIA
Halmashauri ya WALEI Parokia watakuwa na Kikao mara baada ya Misa ya Pili Saa 4:00 asubuhi kikao kitafanyikia Parokiani Boko wajumbe wote mnatakiwa kufika Bila kukosa. ni siku ya Uchaguzi wa Viongozi wa WALEI ngazi ya Parokia.
....Wasilisha Mchango wako wa Hija ya Bagamoyo kwa Mhazini wa Jumuiya yako au Kigango chako Kabla ya Tarehe 09/03/2013..........
anza maandalizi ya ibada ya matawi don bosco tarehe 24/03/2013 mchango ni tshs 3500
Saturday, March 9, 2013
HISTORIA YA JIMBO LA MOROGORO
Jimbo Katoliki la Morogoro Historia |
-
Jimbo la Morogoro lilizaliwa Machi 25, 1953 na
Mhasham Bernard Hilhorst alikuwa askofu wake wa kwanza.
-
Hata hivyo, historia ya Jimbo la Morogoro inaanza
karne ya 19 katika miaka ya 1860. Mapema mwaka 1858 Askofu Amandus
R. Maupoint wa Jimbo Katoliki la Mtakatifu Denis, Reunion alifanya
makao yake Kisiwani Unguja. Miaka miwili baadaye Wamisionari wengine
walikuja Unguja kufanya uinjilishaji.
Baada ya miaka
michache ilionekana ilifaa kazi ya uinjilishaji Unguja ikabidhiwe
kwa Shirika la Kidini lenye uzoefu. Shirika la Mapadri wa Roho
Mtakatifu walikabidhiwa jukumu hilo.
-
Novemba 12, 1862 Unguja ilipandishwa hadhi toka “Mission Territory”
na kuwa “Apostolic Prefecture
of Zanguebar.” Unguja
ikapata Msimamizi wa Kitume chini ya
Mamlaka ya Askofu Maupoint.
-
Juni 16, 1863 Mapadri
Anthony Horner na Edward Baur na Mabradha
Celestine na Felician wa Shirika la Roho Mtakatifu waliingia
Unguja na Baadaye mwaka 1868 Wamissionari hao waliongozwa na Padre Horner walifika Bagamoyo mara ya kwanza Machi 4, 1868.
-
“Apostolic Prefecture of Zangueber, kama eneo la Kitume
lilivyojulikana siku hizo, lilikuwa ni pamoja na Kisiwa cha Unguja
na ukanda wa mashariki kuanzia Guardafui hadi Cap Delgado, yaani
eneo lote la Afrika ya Mashariki.
-
“Prefecture” hiyo
iligawanywa katika sehemu mbili kuu Wamisionari wa Afrika yaani
“White Fathers”walipoingia Unguja April 29, 1878. Hivyo, sehemu
iliyojulikana kama ya Maziwa Makuu ambayo ilikuwa ni pamoja na
Nyanza ambayo kwa sasa ni Jimbo Kuu la Mwanza, Musoma, Shinyanga na
Geita; Tanganyika, ambayo ni Majimbo ya Kigoma, Sumbawanga na Mbeya
na Congo ilikabidhiwa kwa Mapadri hao wapya, Wamisionari wa Afrika.
Na sehemu iliyobaki ilikuwa bado chini ya Shirika la Roho Mtakatifu.
-
Mwaka 1887 sehemu ya “Prefecture” ambayo sasa ilipata hadhi ya
kuitwa “Vacariate” of “Zanguebar”
nayo ikagawanywa katika sehemu kuu tatu:
(a)
Zanguebar Kaskazini na Nairobi. Hii ilijumlisha Mombasa.
(b)
Zanguebar Kusimi, yaani Kilwa na Mzizima au Dar es Salaam.
(c)
Zanguebar Kati, ambayo mwaka 1906 iliitwa Vicariat ya Bagamoyo.
-
Zanguebar Kusini ilikabidhiwa kwa Wamisionari
Wabenediktini. Ilikuwa na hadhi ya “Prefecture.”
-
Mwaka 1910 Vikariat ya Bagamoyo iligawanywa tena
katika sehemu mbili, yaani Vikariat ya Kilimajaro na Vikariat ya
Bagamoyo. Zote zilikuwa chini ya Shirika la Roho Mtakatifu.
-
Mwaka 1934 Vikariat ya Dodoma
ilizaliwa, sehemu ilimegwa toka Vikariat ya Dar es Salaam na
Vikariat ya Iringa, na sehemu nyingine ilimegwa toka Vikariat ya
Bagamoyo.
-
Mwaka 1950 Vikariat ya Bagamoyo ikamegwa na
kuunda Vikariat ya Tanga na miaka mitatu baadaye, yaani Machi 25,
1953 wakati Majimbo yalipoundwa Tanganyika, Vikariati ya Bagamoyo
iliyobakia ikapata hadhi ya Jimbo na kuwa Jimbo la Morogoro wakati
Dar es salaam ikainuliwa na kupata hadhi ya kuwa Jimbo Kuu la Dar es
salaam.
Maaskofu wa Morogoro
-
Tangu kuanzishwa kwake kama Vikariat ya
Bagamoyo
mwaka 1906, wafuatao ndio Maaskofu Wake:
Askofu Raoul De Courmont (1883 - 1896) | |
Askofu Emille Allgeyer (1897 - 1906) | |
Askofu F.X.Vought (1906 – 1923) | |
Askofu B.Wilson (1924 – 1933) | |
Askofu Bernard Hilhorst (1934 – 1954) | |
Askofu Herman V.Elswijk (1954 – 1967) | |
Askofu Adrian Mkoba (1967 – 1992) | |
Askofu Telesphor Mkude (1992 sasa) |
-
Mhasham Adrian Mkoba ndiye Askofu wa kwanza
Mzalendo wa Morogoro.
Hali ya Kijiografia
-
Jimbo Katoliki la Morogoro limeundwa na eneo lipatalo
kilomita za mraba 43,380 kusini mashariki mwa Jamhuri ya Tanzania.
Jimbo la Morogoro limeundwa kutokana na Wilaya za Serikali tano,
yaani Morogoro Mjini, Morogoro Vijijini, Kilosa, Mvomero, na
Bagamoyo. Wilaya ya Bagamoyo ni sehemu ya Mkoa wa Pwani Kiserikali,
wakati Wilaya nne zilizobaki zipo katika Mkoa wa Morogoro.
-
Makao Makuu ya Mkoa wa Morogoro yapo katika
Manispaaa ya Morogoro. Vile vile katika Manispaa hii yanapatikana
Makao Makuu ya Jimbo la Morogoro, Kanisa Kuu la Jimbo, na Makao ya
Askofu wa Jimbo.
Wakazi wa Jimbo
- Jimbo la Morogoro lina wakazi wapatao 1,559,271.
Kati ya hao wakatoliki ni 638,591.
-
Ni asilimia ishirini (20%) tu ya wakazi wa Jimbo la Morogoro
wanaishi mijini, wakati asilimia kubwa, yaani 80%, wanaishi vijijini.
-
Makabila asilia yanayopatikana Jimboni Morogoro ni Waluguru,
Wanguu, Wakutu, Wazigua, Wakami, Wakaguru, Wavidunda, Wasagara, Wakwavi, Wakwere,
Wazaramo na Wadoe,
-
Mbali ya makabila haya asilia, Jimbo la Morogoro lina
wahamiaji vile vile. Makundi haya ya wahamiaji wengi wao ni Wachaga,
Wamasai, Wangoni na Wagogo.
-
Kila kabila lina lugha yake ya asili. Hata hivyo,
Kiswahili kinatumika katika sehemu zote katika Jimbo la Morogoro
MASHIRIKA YALIYOPO JIMBO LA MOROGORO
Vito
mbalimbali katika taji la dhahabu ambalo Kristo amempamba Bibiarusi wake. Au
fungu zuri la maua ya kila rangi. Ni mifano miwili iliyotumika kuelezea wingi wa
mashirika ya kitawa ndani ya Kanisa Katoliki. Jimbo la Morogoro ni mojawapo kati
ya yale yanayofurahia zaidi neema kubwa namna hiyo.
Tukirudi
nyuma hadi karne ya XIX , tunakuta kwamba watawa wa Roho Mtakatifu (Holy Ghost
Fathers) ndio waanzilishi wenyewe wa Kanisa nchini, wakitokea Zanzibar na
Bagamoyo, na kufuatwa muda si mrefu baadaye na masista kutoka kisiwa cha Réunion
(Filles de Marie) Hivyo tangu awali watawa wamekuwa mstari wa mbele sio tu
katika maisha ya Kiroho, bali pia katika umisionari.
Mwanzo
mgumu: kwa miaka mingi mashirika hayo yaliinjilisha wakistahimili tabu na hari
za mchana, mpaka watawa wengine hasa wananchi, tunda la kazi yao, wakaja
kuwaunga mkono kwa saa tofautitofauti.
Masista
wengi wa nchi nzima wanafahamu sana jimbo hili kwa sababu waliwahi kusoma Bigwa,
katika sekondari iliyoanzishwa kwa ajili yao na Umoja wa Mama Wakuu Tanzania (ambao
kwa sasa unakamilisha ujenzi wa kituo kingine cha malezi ya pamoja si mbali na
shule hiyo).
Hatua
mpya ya uwepo wa mashirika jimboni ilipigwa pale ambapo Wasalvatoriani kisha
kupatana na mashirika mengine walichagua Morogoro kama mahali pa kujenga
seminari kuu ya kitawa ambayo kwa sasa ni Taasisi ya Falsafa na Tauhidi (wengine
wanafikiria kuigeuza tena iwe Chuo Kikuu chenye vitivo mbalimbali). Hayati
Askofu Adriani Mkoba alifungua milango ya jimbo kulipokea kila shirika
litakalohitaji watawa wake wasomee huko. Tangu hapo ujenzi na malezi havijakoma
katika eneo la mlima Kola, kwenye barabara ya Dar es Salaam. Yeyote anayepita
anajionea maendeleo hayo na kuzungumzia aina hiyo ya Vatikano chini ya milima ya
Uluguru.
Mvuto
wa taasisi hiyo ndio sababu kuu ya mashirika kumiminika Morogoro miaka ya mwisho;
lakini ukianza kuelekea Dodoma, kwenye eneo la Kihonda unakuta vilevile
mashirika mengi, ingawa majengo yao yamefichikafichika kati ya nyumba za
wananchi.
Kwa
jumla sasa hivi jimbo lina mashirika zaidi ya 30 ya kila aina: ya wanaume na ya
wanawake, ya kikleri na ya kilei, ya maisha ya wakfu na ya maisha ya kitume, ya
kipapa na ya kijimbo. Inakosekana bado monasteri ya maisha ya sala tu, ingawa
Askofu Telesphor Mkude ana hamu nayo.
Mhashamu
akiona kwa furaha kubwa ongezeko hilo ambalo linaendelea haraka, mwanzoni mwa
Jubilei kuu ya mwaka 2000, pamoja na kumteua kwa mara ya kwanza makamu wake
maalumu kwa maisha ya wakfu aliamua kuunganisha mashirika hayo yote katika
ASSICAL (Association of Institutes of Consecrated and Apostolic Life –
Morogoro Diocese) ili yaweze kufahamiana na kubadilishana mawazo, mang’amuzi,
matarajio na mipango hasa upande wa malezi na wa utume.
Tangu
hapo utume huo unazidi kuimarika kwa njia ya mikutano na adhimisho la pamoja la
sikukuu ya watawa iliyoanzishwa na Papa Yohane Paulo II kwenye tarehe 2 Februari
ya kila mwaka. Kwa kweli ni tukio la kufurahisha kuona mamia ya watawa wa mabara
karibu yote kushangilia miito yao mbalimbali kwa ajili ya ufalme wa mbinguni.
Lakini siku moja haiundi mwaka. Kuna siku nyingine 364 ambazo ni nafasi ya kila
mtu kumshukuru Mungu kimatendo kwa karama aliyomjalia. Uaminifu wa kila sasa
ndio unaothibitisha kwamba neema inapokewa kwa mikono miwili badala ya kuchezewa.
La sivyo adhimisho halina maana. Changamoto hiyo ipo daima mbele ya kila mmoja
na ya kila jumuia, kwa sababu maisha ya kitawa ni ya kulenga utakatifu pamoja na
wengine, sio kibinafsi.
Mbali
ya utakatifu, mashirika yanalenga kutoa mchango katika Kanisa na katika jamii,
kila moja kadiri ya karama yake. Ingawa nguvu nyingi za mashirika mbalimbali
yaliyohamia jimboni kwa ajili ya malezi zinaishia katika kazi hiyo ya msingi,
tunaweza kusema nia ya kufanya kitu hata nje ya nyumba ipo. Kadiri ushirikiano
unavyostawi, njia zinaonekana, kwa sababu penye nia pana njia.
Mahitaji
ya jimbo hasa ni mengi, kama kawaida. Hivyo mapadri na walei wanatazamia sana
kufaidika na uwepo wa umati huo wa waamini wenzao waliojitoa kabisa kwa maisha
ya wakfu na ya kitume. Baadhi ya mashirika yana nyumba zisizo za malezi, nazo
ndizo zinazoitikia zaidi mahitaji hayo. Kwa namna ya pekee Masista wa Moyo Safi
wa Maria wa Morogoro, ambao ndio wengi, wanahudumia parokia, shule na zahanati
nyingi jimboni kote.
Mungu
atujalie sisi sote kushika kwa unyenyenyeku nafasi aliyotupangia katika
kufikisha watu kwenye uzima wa milele.
1. MASHIRIKA YA MAISHA YA WAKFU
1.1. Mashirika ya Kitawa
1.1.1. Ya Kiume
1.
Ndugu
Wafransisko Wakonventuali – SLP 932 – Morogoro
Simu: +023/0784594072 – Barua pepe: krzcie@yahoo.com
– Tovuti: www.ofmconv.org
2.
Ndugu
Wafransisko Wakapuchini – SLP 900 – Morogoro
Simu:
+023/2603204 – Barua pepe: kolafriars@yahoo.com
– Tovuti: www.ofmcap.org
3.
Ndugu Waagustino – SLP 1947 – Morogoro
Simu:
+023/2604773 – Barua pepe: osamorogoro@yahoo.com
– Tovuti:
4.
Wakarmeli OCD – SLP 363 – Morogoro
Simu:
+023/2603800 – Barua pepe: ocdtzmission@yahoo.com
– Tovuti:
5.
Shirika la Roho Mtakatifu – SLP 16 – Bagamoyo
Simu:
+023/2440063 – Barua pepe: eap@habari.co.tz
– Tovuti
6.
Wamisionari wa
Mt. Francis wa Sales – SLP 12 – Morogoro
Simu:
+023/2600036 – Barua pepe: msfsmoro@africaonline.co.tz
– Tovuti: www.fransalians.com
7.
Shirika la Madonda Matakatifu (Wastigmatini) – SLP 2213 – Morogoro
Simu:
+023/2603523 – Barua pepe: stigmatines@morogoro.net
– Tovuti: www.stigmatines.com
8.
Wamisionari Wana wa Moyo Safi wa Maria (Waklareti) – SLP 427 –
Morogoro
Simu:
+023/2600429 – Barua pepe: cmfmorobarbastro@yahoo.com
– Tovuti: www.claret.org
9.
Wasalesiani wa Don Bosco – S.L.P. 4045 – Morogoro – Simu:
+0764–854602 – Barua pepe: –
Tovuti:
10. Wasalvatoriani – SLP 1878 – Morogoro
Simu:
+023/2600897 – Barua pepe: sdsschol@go2.pl
– Tovuti: http://www.sds–ch.ch/africa
11. Wamisionari wa Consolata – SLP 769 – Morogoro
Simu:
+023/2603563 – Barua pepe: allasemi@morogoro.net
– Tovuti: http://www.consolata.org
12. Shirika la Misheni (Wavinsenti) – SLP 6051 – Morogoro
Simu:
+023/2600029 – Barua pepe: depaulmoro04@yahoo.com
– Tovuti:
13. Mabradha wa Elimu ya Kikristo wa Mt. Gabrieli (Wamontfort) – SLP 1124
– Morogoro
Simu: +023/2602204 –
Barua pepe: montmoro@africaonline.co.tz
– Tovuti:
1.1.2.
Ya Kike
1.
Mabinti wa
Maria (wa St. Denis)– SLP 230 – Bagamoyo
Simu:
023/2440417 – Barua pepe: dmdestdenistan@yahoo.fr
– Tovuti:
2.
Masista Wamisionari wa Damu Takatifu – SLP 865 – Morogoro
Simu:
+023/2604655 – Barua pepe: – Tovuti:
3.
Shirika la Moyo Safi wa Maria (wa Morogoro) – SLP 1049 – Morogoro
Simu:
+023/2603591/2604314 – Barua pepe: mgololesisters@intafrica.com
– Tovuti:
4.
Masista wa Msalaba Mtakatifu (wa Chavonod)– SLP 1677 – Morogoro
Simu:
+023/2603328 – Barua pepe: holycross@africaonline.co.tz
– Tovuti:
5.
Masista Watersiari Wakapuchini wa Familia Takatifu – SLP 1989 –
Morogoro
Simu:
+023/2604845 – Barua pepe: htctanz@hotmail.com
– Tovuti
:
6.
Masista wa Mt. Anna (wa Luzern) – SLP 1807 – Morogoro
Simu:
+023/2601550 – Barua pepe: stannsmoro@africaonline.co.tz
– Tovuti:
7.
Masista Wakolejina wa Familia Takatifu – SLP 945 – Morogoro
Simu:
+023/2600424 – Barua pepe: collemoro@hotmail.com
– Tovuti:
8.
Masista wa Maria Imakulata (wa Krishnagar) – SLP 2028 – Morogoro
Simu:
+023/2604066 – Barua pepe: smimoro@africaonline.co.tz
– Tovuti:
9.
Masista wa Mama wa Karmeli – SLP 1302 – Morogoro
Simu: +023/2600359 –
Barua pepe: – Tovuti:
10. Masista wa Mt. Gemma
– SLP 304 –
Morogoro–
Simu: +0784/457358
– Barua pepe: – Tovuti:
11.
Masista Waursula wa Yesu Mteswa – SLP 1048 – Morogoro
Simu: +0756/937297 –
Barua pepe: – Tovuti:
12. Masista wa
Sakramenti Kuu – SLP 2135 – Morogoro
Simu: +023/2602902 –
Barua pepe: – Tovuti:
13.
Mabinti wa Mt. Fransisko wa Sales – SLP 640 – Morogoro
Simu: +023/2600900 –
Barua pepe: dsfstanzania@rediffmail.com
– Tovuti:
14. Masista wa Maria
Imakulata (wa Wroclaw) – SLP 1878 – Morogoro
Simu: +0787/759496 –
Barua pepe: – Tovuti:
15. Masista wa Mt.
Yosefu (wa Annecy) – SLP 58 – Dumila
Simu: +0745/214343 –
Barua pepe: agnesadampukulam@yahoo.com
– Tovuti:
16. Masista wa Mt.
Yosefu (wa Chambery) – SLP 135 – Mikumi
Simu: +0787/710338 –
Barua pepe: – Tovuti: www.csjchambery.org
17. Masista wa Bikira
Maria Malkia wa Mitume – SLP 1925 – Morogoro
Simu: +023/2604165 –
Barua pepe: – Tovuti:
18. Masista wa Mt. Anna
(wa Bangalore) – SLP 363 – Morogoro
Simu: +023/603800 –
Barua pepe: – Tovuti:
19. Masista Waabuduo
Damu ya Kristo – SLP 6508 – Morogoro
Simu: – Barua pepe:
– Tovuti:
20. Dada Wadogo wa Mt.
Fransisko – SLP 1878 – Morogoro
Simu: +0787/759496 –
Barua pepe: – Tovuti:
21. Masista Wabenedikto
Waafrika wa Mt. Agnes – SLP 6015 – Morogoro
Simu: +0784/464024 –
Barua pepe: mlowevicky@yahoo.com –
Tovuti:
22. Masista wa Mt.
Karolo Borromeo – SLP 1232 – Morogoro
Simu: +0732/931181 –
Barua pepe: – Tovuti:
23. Masista Warosmini wa
Maongozi – SLP 133 – Morogoro
Simu: +0787/024621 –
Barua pepe: – Tovuti:
24. Masista wa Maryknoll
– SLP – Morogoro
Simu: – Barua pepe:
– Tovuti:
25.
Masista Wafransisko wa Upendo – S.L.P. 6083 –
Morogoro
Simu: – Barua pepe:
– Tovuti:
1.2. Mashirika ya Kilimwengu
1.2.1.
La Kiume
1.
Mapadri wa
Shirika la Kilimwengu katika Kazi ya Roho Mtakatifu – SLP 640 – Morogoro
Simu: +023/2603340 –
Barua pepe: – Tovuti:
1.2.2.
Ya Kike
1.
Unitas kwa Afrika – SLP 1003 – Morogoro
Simu:
+023/2600138 – Barua pepe: – Tovuti:
2.
Masista wa Grail – SLP 6090 – Morogoro
Simu: +023/2613690 –
Barua pepe: – Tovuti:
2. MASHIRIKA YA MAISHA YA KITUME
2.1. Ya Kiume
1.
Wamisionari wa Damu Azizi – SLP 1925 – Morogoro
Simu:
+023/2604165 – Barua pepe: stgascoll @yahoo.com
– Tovuti: www.cpps–preciousblood.org
2.
Jumuia ya Mapadri katika Kazi ya Roho Mtakatifu – SLP 1935 – Morogoro
Simu: +023/2601353 –
Barua pepe: – Tovuti:
2.2. La Kike
1.
Jumuia ya Masista katika Kazi ya Roho Mtakatifu – SLP 6038 – Morogoro
Simu: +023/2601764 –
Barua pepe: – Tovuti:
3.
TAASISI ZA MALEZI YA PAMOJA KATI YA MASHIRIKA YA KIKE
1.
Sekondari ya Masista ya Bigwa – SLP 369 – Morogoro
Simu:
+023/2603066 – Barua pepe: bigwasrs@yahoo.com
– Tovuti:
2.
Kituo cha Malezi ya Masista cha Kola – SLP 913 – Morogoro
Simu: +023/2600658 –
Barua pepe: tcastanzania@hotmail.com –
Tovuti:
4.
CHAMA (CHA WANAUME NA WANAWAKE)
1.
Ndugu Wadogo wa Afrika – SLP 6083 – Morogoro
Simu: – Barua pepe: unwa@unwa.tk
Tovuti: www.unwa.tk
UCHAGUZI WA PAPA 2013
Makardinali wa kanisa Katoliki kutoka sehemu tofauti za dunia,wameanza
utaratibu wa kumchagua mrithi wa Papa Benefickt wa XVI aliyejiuzulu
mwezi uliopita.
Zoezi hilo limeanza leo Vatican saa 3.00 asubuhi kwa saa za Vatican sawa
na saa 6 mchana kwa saa za Afrika Mashariki kwenye ukumbi wa New Synod
Hall.Mkutano huo ndio utafungua mchakato wa uchaguzi wa Papa mpya na unatarajiwa kuandaa ratiba ya uteuzi wa papa mpya.Makardinali hao ndio watapanga siku ya kufanyika mkusanyiko wao unaoitwa `Papal Conclave' kwa ajili kufanya uchaguzi huo.
Kutokana na utaratibu wa kanisa Katoloki, uchaguzi wa Papa hutakiwa kufanyika siku 15 hadi 20 kufuatia siku kiti cha papa kilipoanza kuwa kitupu na Uchaguzi kwa kawaida hufanyika katika Kanisa la Sistine Chapel.
Takribani makardinali 115 kutoka nchi mbalimbali duniani,wanahusika na uchaguzi huo wa Papa ambapo Kati ya hao, makardinali 67 waliteuliwa na Papa Benedict,Joseph Aloisius Ratzinger.
Kwa upande wake aliyekuwa papa ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani amekuwa akitumia muda kufanya ibada, kusoma vitabu na meseji za kumtakia kila la kheri papa aliejuzulu kutoka sehemu mbalimbali duniani na kutafakari.
Hadi sasa hakuna tarehe yoyote iliotajwa kuhusu uchaguzi huo wa papa ingawa vyanzo vya habari vya Italan vimedokeza kuwa huenda Machi 11 2013 ikawa siku hiyo ya uchaguzi wa papa.
Kiongoazi wa chuo cha makardinali Angelo Sodano ameongea kuwa siku maalumu ya kuanza kwa uchaguzi huo,haitatajwa hadi hapo makardinali wateule wote watakapo wasili mjini Rome
Papa mpya atatokea bara gani?
Kadinali Ricardo Jamin Vidal wa Philippines(kulia) na Luis Antonio
Tagle wamewasili kuhudhuria mkutano wa makadinali kabla ya kongamano
litakalomchagua Papa mpya
Nafasi ya Papa ajae imeendelea kuwa wazi kwa kila mtu kutoka katika maeneo mbalimbali ya dunia, na kutoka katika makanisa mbalimbali.
"Wakati alipofariki John Paul II mwaka 2005, kila mtu alikuwa anafikiria atakaeshinda nafasi hiyo kwa mwezi huo naku ra ilikuwa muda mfupi tuu'' amesema kadinali alijiuzulu akiongea na shirika la habari la AFP.
Kwa upande wa Afrika Makardinali waliotajwa ni pamoja na Peter Turkson kutoka Ghana, Robert Sarah Guinea na Wilfrid Napier kutoka Afrika Kusini
Friday, March 8, 2013
MANENO YA MAANDIKO
2 Yohana 1 : 1-13
1.1 Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli;
1.2 kwa ajili ya hiyo kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hata milele.
1.3 Neema,
na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana
wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.
1.4 Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.
1.5 Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.
1.6 Na
huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri,
kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.
1.7 Kwa
maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu
Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.
1.8 Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu.
1.9 Kila
apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana
Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.
1.10 Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.
1.11 Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.
1.12 Kwa
kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini
nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe
imetimizwa.
1.13 Watoto wa ndugu yako aliye mteule, wakusalimu.
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...