Saturday, April 13, 2013
Tuesday, April 2, 2013
RATIBA YA JUMA TAREHE 02-07/04/2013
Safisha mwenendo wako kuwa mfano kwa jamii yako, toa mafundisho ya dini zaidia wasiojiwezi....Maisha ya Kitakatifu.
lipa ada yako ya mwezi kwa kiongozi wako wa jumuiya, Kanda au Kigango.
2.JUMAPILI TAREHE 24/03/2013
Vijana ndiyo chachu ya Kanisa Nguvu kubwa ya Ujenzi na Mabadiliko yaanze kwetu Hudhuria Misa Jumapili kama Amri ya Kanisa inavyotuelekeza.
KANDA MAALUMU YA ANTONY WA PADUA -MBWENI TETA
MISA NI SAA 3:00 ASUBUHI
Kutakuwa na Kikao cha Halamashauri Ya VIWAWA Parokia ya Boko -Kikao kitaanza saa 4:30 asubuhi...Kigangoni Rafael wajumbe ni Viongozi wote wa Vigango fika bila kukosa Tuukuze UTUME wetu
lipa ada yako ya mwezi kwa kiongozi wako wa jumuiya, Kanda au Kigango.
- JUMAMOSI TAREHE 06/04/2013
Viongozi wote wa VIWAWA ngazi ya Jumuiya Kigango cha Mt Rafael mnatakiwa kukutana Kanisani saa 10:00 jioni kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa viongozi wa Vijana Kigango.
2.JUMAPILI TAREHE 24/03/2013
Vijana ndiyo chachu ya Kanisa Nguvu kubwa ya Ujenzi na Mabadiliko yaanze kwetu Hudhuria Misa Jumapili kama Amri ya Kanisa inavyotuelekeza.
JUMAPILI TAREHE 07/04/2013
RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
MISA YA KWANZA 12:30-2:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
MISA YA TATU SAA 4:00-5:30 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI
MISA YA KWANZA SAA 1:00-3:00 ASUBUHI
MISA YA PILI SAA 3:00-4:30 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL-MBWENI MALINDI
MISA YA KWANZA SAA 1:00-3:00 ASUBUHI.
MISA YA PILI SAA 3:00-5:00 ASUBUHI
KANDA MAALUMU YA ANTONY WA PADUA -MBWENI TETA
MISA NI SAA 3:00 ASUBUHI
Kutakuwa na Kikao cha Halamashauri Ya VIWAWA Parokia ya Boko -Kikao kitaanza saa 4:30 asubuhi...Kigangoni Rafael wajumbe ni Viongozi wote wa Vigango fika bila kukosa Tuukuze UTUME wetu
Saturday, March 30, 2013
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Pasaka kwa Mwaka 2013
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Pasaka kwa Mwaka 2013 nchini Tanzania ni: Amani na Maendeleo!
Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salama akitoa ujumbe wake wa Siku kuu ya Pasaka kwa Mwaka 2013 inayokwenda sanjari na Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, anawaalika Wakristo kwa namna ya pekee kabisa kuombea amani, umoja na mshikamano wa kitaifa, hasa kutokana na kushamiri kwa vitendo vya choko choko za kidini nchini Tanzania zilizopelekea: madhulumu na mauaji ya viongozi wa kidini pamoja na uchomaji moto wa nyumba za Ibada.
Kinzani za kidini zinazoendelea nchini Tanzania ni changamoto kwa Wakristo na Waislam kukutana na kujadiliana mustakabali wa Tazania. Kwa vile Serikali inayowajibu wa kulinda na kudumisha misingi ya haki, amani na utulivu inapaswa kuwapo ili kufuatilia majadiliano haya.
Kwa miaka mingi Wakristo na Waislam nchini Tanzania wameishi na kupendana kama ndugu na wala tofauti zao za kidini halikuwa ni jambo la kuwagawa! Lakini mambo yamebadilika katika miaka ya hivi karibuni kiasi cha kuwafanya watu kuanza kujiuliza, hivi kweli ni nani anayehusika na uchochezi wa vurugu za kidini na kwa manufaa ya nani?
Majadiliano ya kidini ni njia muafaka inayoweza kumaliza choko choko za kidini, kila upande ukilijadili suala hili katika ukweli, upendo na haki. Kardinali Pengo anaendelea kuwasihi Wakristo na watanzania wenye nia njema kuepukana na kishawishi cha kutaka kulipiza kisasi kutokana na madhulumu wanayokabiliana nayo. Anasema, ulinzi na usalama wakati wa Maadhimisho ya Juma kuu ni kazi na jukumu la Serikali, kumbe anatumaini kwamba, Wakristo wataweza kuadhimisha Mafumbo ya Imani yao kwa amani na utulivu.
Kardinali Pengo anasema, atakwenda Kanisa kuadhimisha Mafumbo ya Ukombozi, kama ni kufa ni afadhali afie Kanisani na wala hataacha kwenda kusali kwa sababu ya vitisho vya ulipuaji wa Makanisa vilivyozagaa nchini Tanzania wakati huu.
Kardinali Pengo amevishauri vyombo vya dola kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya ukweli, uwazi na maadili ya kazi. Anasema, Serikali haiwezi kuacha Tanzania kutawaliwa na "wahuni wachache" wanaoleta vurugu kwa kisingizio cha dini na kukazia kwamba, hatua madhubuti hazina budi kuchukuliwa ili haki, amani na utulivu viweze kudumishwa.
Itakumbukwa kwamba, Waziri mkuu Mizengo Pinda wa Tanzania na ujumbe wake walipotembelea Radio Vatican hivi karibuni alibainisha kwamba, Serikali ya Tanzania inatarajia tarehe 4 Aprili 2013 kukutana na viongozi wa kidini na wadau mbali mbali ili kwa pamoja kuweza kujadili mustakabali wa Tanzania kwa kuangalia amani na utulivu kama nyenzo muhimu katika ustawi na maendeleo ya Tanzania.
Friday, March 29, 2013
IBADA YA ALHAMISI KUU-POPE FRANCIS
Nimewapeni mfano, nanyi hudumianeni kwa ukarimu na upendo!
Baba Mtakatifu Francisko, Jioni ya Alhamisi kuu, tarehe 28 Machi 2013 ameadhimisha Ibada ya Karamu ya Mwisho, katika Gereza la Watoto la "Casal del Marmo," lililoko mjini Roma kwa kuwaosha miguu watoto kumi na wawili, kielelezo cha upendo wa Kristo unaomwilishwa katika huduma kwa jirani, lakini zaidi kwa wale wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii.
Katika mahubiri yake kwa vijana hawa, amewashirikisha upendo ulioneshwa na Yesu Kristo, Siku ya Alhamisi kuu, alipoweka mavazi yake kando, akaanza kuwaosha mitume wake miguu, kitendo ambacho kilimshangaza Mtume Petro, kiasi cha kutaka kukataa katu katu kuoshwa miguu na Yesu, lakini akafafanuliwa maana yake, kiasi kwamba, akaweza hata kuridhika na uamuzi uliotolewa.
Yesu ambaye ni Mwalimu na Bwana, Nafsi ya Pili ya Fumbo la Utatu Mtakatifu, ndiye aliyetekeleza kitendo hiki cha unyenyekevu, ambacho kilikuwa kinafanywa na watumwa! Akawaachia mfano wa kuigwa na kuendelezwa, kwa kutambua kwamba, uongozi ni huduma hasa kwa wanyonge na wale wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii.
Ni mwaliko wa kumegeana upendo unaobubujika kutoka kwa Kristo, aliyewapenda watu wake upeo kiasi cha kuyamimina maisha yake pale juu Msalabani. Huduma ya upendo, iwachangamotishe waamini na watu wenye mapenzi mema kujikita katika msamaha na upatanisho unaopaswa kububujika kutoka katika undani wa mtu mwenyewe.
Baba Mtakatifu Francisko anasema, kama Padre na Askofu wa Roma, anajisikia kuwajibika kuwaonjesha huruma na upendo wa Kristo kwa njia ya huduma inayopata chimbuko lake kutoka katika moyo wake na wala si jambo la kutaka kujionesha mbele ya watu.
Kwa maneno machache, hii ni imani katika matendo, inayowachangamotisha waamini na watu wenye mapenzi mema, kusaidiana kwa hali na mali; wakiungana kwa pamoja kutafuta mafao ya wengi. Huduma ya upendo ni changamoto endelevu inayotolewa na Yesu aliyekuja kutumikia na kuyamimina maisha yake kwa ajili ya ukombozi wa wengi.
Thursday, March 21, 2013
KIPINDI CHA KWARESIMA
Bibilia na Kipindi cha Kwaresima
Katika Agano la Kale Musa ndiye aliyeongoza Waisraeli. Sisi tunakumbuka na kufuata safari yao ya ukombozi, walipokaa jangwani miaka 40 ili kuelimishwa kinaganaga juu ya yale yatokanayo na maneno 10 ambayo Musa alipewa na Mungu alipofunga siku 40 juu ya mlima Sinai.Hayo yalikamilishwa na Yesu katika Agano Jipya kama kiongozi na mkombozi wa wote. Kabla hajaanza utume wake, yeye pia alifunga siku 40 jangwani akijilisha matakwa ya Baba ili ayatekeleze na kuwatangazia watu wote.
Juhudi za Kwaresima
Kufuatana na hayo yote Kanisa linafunga siku 40 katika jangwa la kiroho. Wakati wa Kwaresima linawaongoza waamini katika safari ya kujirekebisha kulingana na Neno la Mungu la Agano la Kale na la Agano Jipya. Wote wanahimizwa kufunga safari hiyo kadiri ya hali yao: kwanza wale wanaojiandaa kubatizwa usiku wa Pasaka (hasa kwa kufanyiwa mazinguo matatu yanayofuatana katika Dominika III, IV na V), lakini pia waliokwishabatizwa, ambao kabla ya hapo wanatakiwa kutubu na kuungama dhambi ili warudie kwa unyofu ahadi za ubatizo.Makundi yote mawili watakula pamoja Mwanakondoo ili kuishi upya kwa upendo, jambo litakalofanya hata wasio Wakristo wafurahie Pasaka.
Kazi za urekebisho zinahitaji juhudi za pekee. Vivyo hivyo kwa ukombozi wa kiroho Kwaresima inadai bidii nyingi pande mbalimbali: katika kufunga, kutoa sadaka, kusali na kusikiliza Neno la Mungu hasa wakati wa ibada. Hayo yote yanahusiana na kusaidiana.
Mkristo akijinyima chakula cha mwili anajifunza kufurahia zaidi mkate wa Neno la Mungu na wa ekaristi, tena anatambua zaidi anavyopaswa kuwahurumia wenye njaa na shida mbalimbali. Toba inahimizwa isiwe ya ndani na ya binafsi tu, bali pia ya nje na ya kijamii: itokane na upendo na kulenga upendo kwa kurekebisha kasoro upande wa Mungu (sala), wa jirani (sadaka) na wa nafsi yetu (mfungo).
Mfungo, yaani kujinyima tunavyovipenda na hata tunavyovihitaji, uwe ishara ya njaa yetu ya Neno la Mungu, ya nia yetu ya kushiriki mateso ya Yesu yanayoendelea katika maskini, ya kulipa kwa dhambi zetu na kuachana nazo. Sadaka inayotokana na sisi kujinyima inampendeza Mungu kuliko ile isiyotuumiza; msaada unaweza kutolewa pia kwa kutetea haki za binadamu dhidi ya wanyanyasaji. Sala inastawi kwa kusikiliza sana Neno la Mungu hasa kwa pamoja (katika familia, jumuia, liturujia n.k.). Ndiyo maana wakati wa Kwaresima Kanisa linazidisha nafasi za kulitangaza na hivyo kuelimisha wote kuhusu mambo makuu ya imani na maadili yetu.
Kwaresima katika liturujia.
Kuna mpangilio kabambe wa masomo ya Misa, hasa ya Dominika, ili wote wafuate hatua kuu za historia ya wokovu (somo la kwanza) na kuchimba ukweli wa ubatizo (mwaka A), agano na fumbo la Kristo (mwaka B) na upatanisho (mwaka C). Kwa njia hiyo tunatangaziwa jinsi Mungu anavyotuokoa; pia upande wetu kuanzia Dominika ya kwanza tunajielewa kuwa watu vishawishini ambao tunapaswa kushinda kwa kumfuata Yesu, si Adamu: kwenda jangwani ili kumtafuta Bwana na matakwa yake.Kilele cha safari ya Kwaresima ni Dominika ya Matawi, tunapoingia Yerusalemu pamoja na Yesu anayekwenda kufa na kufufuka kwa ajili yetu. Liturujia ya siku hiyo ina mambo mawili: kwanza shangwe (katika maandamano), halafu huzuni (kuanzia masomo, ambayo kilele chake ni Injili ya Mateso).
Baada ya Kwaresima kwisha, tutapitia tena historia ya wokovu katika kesha la Pasaka ambapo hatua zote zinaangazwa na ushindi wa Kristo mfufuka.
JUMA KUU LA PASAKA
Juma kuu
Katika madhehebu mengi, juma hilo linaanza na Jumapili ya matawi ambapo linaadhimishwa kwa shangwe tukio la Yesu Kristo kuingia huo mji mtakatifu kama mfalme wa Wayahudi huku akipanda punda na kushangiliwa na umati wa wafuasi wake, waliofurahia hasa alivyomfufua Lazaro wa Betania.
Lakini Yesu alieleza kuwa ufalme wake si wa dunia hii, na kuwa yeye hakuja kutumikiwa bali kutumikia na kutoa uhai wake uwe fidia ya umati.
Hivyo siku zilizofuata alikabili kwa hiari mateso na kifo kutoka kwa wapinzani wake na kwa mamlaka ya Ponsio Pilato, na hatimaye akafufuka mtukufu usiku wa kuamkia Jumapili.
Kabla ya hapo Yesu alijumlisha hayo matukio yajayo katika karamu ya mwisho aliyokula pamoja na mitume wake 12, akiwaachia agizo la kufanya daima karamu ya namna hiyo kama ukumbusho wake.
Basi, kuanzia Alhamisi kuu jioni hadi Jumapili ya Pasaka jioni Wakristo wanaadhimisha siku tatu kuu za Pasaka, zinazofanya ukumbusho wa Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka.
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...