Saturday, April 27, 2013

Matangazo ya Dominika ya kesho Tarehe 28/04/2013

Mpendane. kama vile nilivyowapenda ninyi nanyi mpendane vivyo hivyo huu ni mwaliko tuupatao kutoka kwa kristo mwenyewe. neno upendo ni neno dogo au fupi kiherufi lakini linabeba maana nzito na kubwa sana hasa kwetu sisi tulio wafuasi wa kristo. na ambao tunafanya utume wa Vijana Wakatoli (askari kamili wa Yesu) Salamu yetu ni Mapendo.......Daima. swali ni je tunayaishi haya Mapendo tunayoyatamka.....tunakuwa wavumilivu kwa wengine, tunawapenda wengine kama sisi tunavypjipenda na tupo tayari kuteseka kwa ajili ya mwengine.

Tunaona ilikuwa siku ya alhamisi katika karamu ya mwisho Yesu kama mkubwa wa familia na yeye na mitume wake akichukua nafasi ya ukubwa wa familia; anatimiza wajibu wake wa kuwapa maneno machache mitume wake yawe kama mwongozo wa maisha yao. Yesu akijua wazi kuwa hiyo ndiyo karamu yake ya mwishona mitume wake,......ni kweli sisi kama wakubwa au viongozi wa ngazi fulani tuyatekeleza yale tulipewa kufanya......au sisi ndiyo chanzo cha kuyazima yale yenye nuru ya Mungu na kupandikiza ya kishetani.....

MATANGAZO YA JUMAPILI YA KESHO
KIGANGO CHA BOKO
IBADA YA KWANZA
 SAA 12:15-2:00 ASUBUHI
IBADA YA PILI
SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
IBADA YA TATU
SAA 4:00-5:30 ASUBUHI
Viongozi wote wa VIWAWA ngazi ya Kanda Mkutane na Uongozi wa VIWAWA wa Kigango mara baada ya misa ya Pili.

KIGANGO CHA MT. RAPHAEL- MBWENI MALINDI
IBADA YA KWANZA
 SAA 1:00-3:00 ASUBUHI
IBADA YA PILI
SAA 3:00-5:00 ASUBUHI

KIGANGO CHAMBWENI
IBADA YA KWANZA
 SAA 1:15-3:00 ASUBUHI
IBADA YA PILI
SAA 3:00-5:00 ASUBUHI

KANDA YA MT. ANTONY WA PADUA
IBADA YA KWANZA
 SAA 3:15-5:00 ASUBUHI
UONGOZI WA VIWAWA PAROKIA UTAKUWEPO KWA AJILI YAKUTOA SEMINA JUU YA UTUME WA VIWAWA NA KUONA MAENDELEO YA VIJANA WA KANDA HIYO...FIKA NA UMWAMASISHE MWENZAKO.........

NAFASI ZA USHIRIKI WA ZIARA YA MBULU ZIMEBAKI CHACHE JITAHIDI UCHUKUE FORM MAPEMA......USIJE JUTIA NAFASI HII MWISHO WA KUREJESHA FORM NI TAREHE 29/05/2013.....TUNAWATAKIA MAANDALIZI MEMA

        ................................DOMINIKA NJEMA................................

Saturday, April 20, 2013

MJUE MH.ISIDORI BAKANJA

Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaji unaofanywa na utawala wa Mfalme Leopold II wa Kongo katika Jimbo Free. Yeye alizaliwa katika Bokendela juu ya Congo mto, kaskazini ya mji wa Mbandaka (zamani Coquihatville). Baba na mama yake waliitwa Iyonzwa na Inyuka. Bakanja ya jina mwenyewe ilikuwa variously hutamkwa kama Bakanda, Bakana, Bokando, Makanda na Makando. Katika miaka ya ishirini ya mapema Bakanja akaenda chini ya mto wa ajira Mbandaka kutafuta. Huko akawa mwashi na aliajiriwa na serikali katika sekta ya ujenzi. Wakati katika Mbandaka alimkuta wamisionari Wakatoliki wa Mpango Trappist (Wasitoo), alifundishwa na wao na alibatizwa katika Parokia ya St Eugene, Bolokwa-Nsimba, juu ya Mei 6, 1906. Alipokea Kwanza Ushirika na Kipaimara baadaye katika mwaka huo huo. Bakanja aliishi imani yake mpya sana tu, cherishing wawili ishara ya nje ya rozari na scapular ambayo yeye kamwe alishindwa kuvaa. Kwa neno na mfano, alivutia marafiki na marafiki na imani ya Kikristo.
Bakanja kisha mimba wazo la kurudi kwa kijiji eneo lake ili kufanya kazi kwenye mashamba ya Ulaya inayomilikiwa. Licha ya maonyo kutoka kwa marafiki zake, yeye alipata kazi kama mtumishi katika nyumba ya msimamizi wa shamba iitwayo Reynders saa Busira. Wakati Reynders kuhamishiwa kwa Ikili, Bakanja walifuatana naye. Huko, meneja mashamba mara fulani Van Cauter, ambaye alikuwa anajulikana kwa kuwa fanatically kinyume na Ukristo na wamisionari wa Kikristo. Bakanja alifanya kazi zake uangalifu na uhusiano wake na Reynders walikuwa mzuri, ingawa mwisho alionya yake ya bure kwa kuficha imani yake ya Kikristo. Van Cauter, hata hivyo, alikuwa na hasira wakati Bakanja alikataa kuondoa scapular yake, na akaamuru ukali viboko. Bakanja kukubaliwa adhabu kudhulumu katika roho ya Yesu katika mateso yake. Baadaye, Van Cauter aliona Bakanja wakiomba wakati wa kipindi cha mapumziko na akaruka ndani ya hasira. Alikuwa Mkuu wake mtandikeni Bakanja tena papo hapo. Bakanja alipewa viboko zaidi ya 250 kwa mjeledi kiboko kujificha kwamba alikuwa na misumari ndani yake. Yeye alikuwa kisha wamefungwa na minyororo. Kwa kirefu, yeye ilitolewa na kuamuru kuongozana Reynders kwa Isoko. Shida na uwezo wa kutembea, Bakanja kujificha katika misitu. Siku tatu baada ya iligunduliwa na mwingine rasmi kuitwa Dorpinghaus ambaye alikuja kukagua shamba. Bakanja ulifanyika kwa mashua mto na kupokea matibabu kwa ajili ya vidonda vyake, ambayo kwa wakati huu walikuwa mwanzo putrify. Mifupa yake wazi pia ilimfanya mateso ya papo hapo.
Saa Ngomb'Isongo, ambapo mashua mto kuweka katika, imeonekana vigumu kuacha maambukizi. Kufa ya septicaemia, Bakanja alipelekwa Busira kutunzwa na Katekisti mitaa na kupokea ziara ya wamishenari wawili Trappist Julai 24 na 25 1909, ambaye alipokea sakramenti ya mwisho. Alifariki mnamo Agosti 15, kusamehe na kuomba kwa ajili ya kumtesa wake. Cauter Van hatimaye kupelekwa mahakamani na waajiri wake na alipewa hukumu ya jela.
Juu ya Aprili 25, 1994 Bakanja Isidore ilikuwa beatified na Papa Yohane Paulo II mbele ya mamia ya Maaskofu wa Afrika, makuhani na kidini, kuhudhuria Mkutano Maalum kwa Afrika ya Sinodi ya Maaskofu katika Roma.

VISIT evangelization 26-30/06/2013,,,


Dear VIWAWA, we invite to participate in the evangelizing tour, to be held in the state of David Parish insane person.

The main objective of this visit is to the evangelization of detail where in conjunction with our caregivers and our host we analyzed the following factors:

      Religious teaching which is the provision of education in the truth.
     In the tradition of Faith for Teens
     State of obedience and humility (values ​​Youth)
     Our mission youth (social issues, politics and economy)
     And more


VISITA evangelizzazione 26-30/06/2013

Caro VIWAWA, vi invitiamo a partecipare al tour di evangelizzazione, che si terrà nello stato di David Parish pazzo.

L'obiettivo principale di questa visita è quello l'evangelizzazione della Cina, dove in collaborazione con i nostri assistenti e il nostro ospite abbiamo analizzato i seguenti fattori:

      L'insegnamento religioso, che è l'offerta di istruzione nella verità.
     Nella tradizione di fede per adolescenti
     Stato di obbedienza e di umiltà (valori Gioventù)
     La nostra missione giovanile (questioni sociali, della politica e dell'economia)
     E più

hate taboo ... love always ....,,odio tabù ... amare sempre ....

Hii ndiyo salaam inayotuongoza ....Mapendo......daima ....chuki...mwiko.....hebu leo mimi na weww tufanye tafakari ya kina juu ya salama hii,.... tukiongozwa na amri kuu ya kanisa ambayo ni "mapendo" tunakumbushwa kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda(ci viene ricordato di amare il nostro prossimo come noi stessi)

Tuesday, April 16, 2013

ZIARA YA UINJILISHAJI 26-30/06/2013

Wapendwa VIWAWA, tunawakaribisha kushiriki katika ziara ya uinjilishaji, itakayofanyika katika jimbo la mbulu Parokia ya daudi.
Lengo kubwa la ziara hii ni kwenda kuinjilishaji wa Kina ambapo kwa kushirikiana na walezi wetu pamoja na mwenyeji wetu tutachambua mambo yafuatayo:
  1.  Ufundishaji wa dini ulio utoaji wa Elimu katika kweli. 
  2. Mapokeo ya Mwaka wa Imani kwa Vijana
  3. Hali ya Utii na Unyenyekevu(maadili ya Vijana)
  4. Utume wetu wa vijana(maswala ya jamii, siasa na uchumi)
  5. Na mengine mengi  
waweza tafakari mafundisho haya ya dini
Kanisa linapofundisha juu ya Mungu au linapozungumza juu ya Mungu linatoa elimu katika ukweli, elimu inayolenga kumjenga Mwanadamu katika ubinadamu wake. Tangu mwanzo Kanisa limejikita katika Elimu si kwa sababu nyingine yoyote bali kumwinua binadamu katika ubinadamu akapate kujifahamu yeye ni nani, ametoka wapi na kwa nini yuko pale alipo. Mtaguso Mkuu wa Vatikan umesisitiza pia juu ya mfungamano kati ya uinjilishaji na utoaji wa Elimu.

Baba Mtakatifu Benedikto XVI anakazia uzito ukweli huu anapozungumzia utume msingi wa Kanisa wa uinjilishaji unaotoa kipaumbele katika elimu na kuwianisha na malengo ya Taifa lolote kuendeleza na kuiinua jamii katika hadhi inayotegemewa. Ikumbukwe kwamba Kanisa katika utume wake linaoanisha daima dhana za imani na akili kwamba imani huiangaza akili kutambua ukweli na hivyo kumfanya binadamu kuutambua ukweli ulio msingi wa maisha adilifu yampasayo kuishi.

Baba Mtakatifu Benedikto XVI anakazia kuwepo kwa muungano kati ya uinjilishaji na utoaji wa elimu hasa nyakati hizi ambapo elimu dunia inaelekea kumpoteza mwanadamu katika ulimwengu. Hivyo amelialika Kanisa kulichukulia makini suala la uenezaji wa Imani kufungamana na utoaji wa elimu ili kweli elimu itoe ujuzi na maarifa ya kumwendeleza mtu mzima kiroho na kimwili.

Baba Mtakatifu Benedikto XVI ametahadharisha kuwa mfumo wa elimu hivi sasa umeshindwa kutoa malezi bora kwa kizazi kipya kiasi kwamba imedhihirika wazi uwepo wa mmomonyoko wa maadili katika jamii. Elimu inayotolewa ni elimu maarifa tu bila thamani za maisha.

Nyakati hizi watu wengi wanaogopa kusema ukweli na badala yake kukimbilia propaganda za kidunia na utumbuaji wa maisha tu. Matokeo yake watu wanapumbazwa na propaganda za biashara na kuishia kufikiria kwamba maisha ni ponda mali kufa kwaja bila kuangalia thamani halisi ya maisha ya Mwanadamu.

Ulimwengu wa leo unatoa elimu amabayo haimwajibishi mwanadamu katika matendo yake na baadaye anapokutana na changamoto za maisha anakosa mwelekeo na kuishia kuchukua hatua zisizo za kibinadamu kwani ndani yake kakosa utu kageuka kitu ambacho kikikosa thamani yake hutupwa jalalani au kuchomwa moto. Baba Mtakatifu na Kanisa zima lazima liguswe na hili kwani utume wake si kuokoa roho tu bali na mwili pia ambao ndilo hekalu la roho hapa duniani.

Wajibu wa Kanisa kujikita katika utoaji Elimu ni kuboresha mazingira ya maisha ya mwanadamu. Baba Mtakatifu anasema Kanisa litawajibishwa na Bwana iwapo halitapigania kujenga utu wa mwanadamu jinsi ile alivyokusudiwa na Muumba. Hivi sasa kumekosekana heshima kwa ubinadamu hivi kwamba, watu hawathamini tena zawadi ya maisha, wanaona kama mzigo, au kitu cha kufanyia utafiti kwenye maabara kwa malengo ya kiburi tu; mimba kutupwa ovyo, biashara zilizokithiri za viungo na miili ya binadamu, na watoto kuuzwa kama bidhaa. Iko hatari hapa ya ubinadamu kukengeuka kama enzi za Sodoma na Gomora. Hivyo Kanisa lililo Mwili wa Kristo halina budi kusimama kidete kurudisha tena hadhi na thamani ya binadamu iliyo hatarini kupotea.

Baba Mtakatifu Benedikto XVI amemnukuu Baba Mtakatifu Paulo VI, kuwa Mwanadamu wa leo husikiliza zaidi ushuhuda kuliko mafundisho ya mwalimu, vinginevyo Mwalimu atasikilizwa kwa sababu anatoa ushuhuda. Hivyo amelitaka Kanisa kutumia ushuhuda wa maisha katika utoaji wa elimu kwa jamii. Maisha ya ushuhuda yanayoshuhudia ukweli wa Imani na maisha, ndicho kifundishio pekee kwa jamii ya leo.

Changamoto kwa Kanisa na Wanakanisa ni kujitoa mhanga kutoa mifano hai ya maisha yaliyojengwa katika dhamiri iliyo safi, hai na adilifu. Maisha ya utakatifu, usafi, unyenyekevu, upole, amani, haki na mshikamano ndizo silaha pekee za kumfikisha Yesu Mkombozi wa dunia kwa watu.

       Wahi sasa achukue form na ada ya ushiriki ni tshs 150,000 tu ziara itaanza tarehe 26-30/06/13 na mwisho wa kukusanja michango ni tarehe 29/05/12



 Mpendwa Kijana , Nakutakia kheri na Baraka katika kumshuhudia Yesu katika ulimwengu wa leo ambao unaonekana kupoteza maarifa. Shime Mkristu mwenzangu twende tukalirudishe lile tumaini la Kristu kwa watu hawa kwani sisi tumeona mwanga basi tuupeleke mwanga huu na kwa wengine.



Saturday, April 13, 2013

Shutuma za udini dhidi ya Mwl. J. K. Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania

Shutuma za udini dhidi ya Mwl. J. K. Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania



Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania ni kati ya viongozi wa siasa wanaoheshimika sana Barani Afrika. Lakini kwa bahati mbaya, "Nabii hakosi heshima isipokuwa kwa watu wa nyumbani kwake".

Kwa miaka kadhaa, baadhi ya Waamini wa dini ya Kiislam nchini Tanzania amedai kwamba, wakati wa utawala wa Mwalimu Julius K. Nyerere, waamini hao walinyanyaswa kiasi kwamba, wamebaki nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na waamini wa dini nyingine nchini Tanzania.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican, katika mahojiano maalum na Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki Musoma, anakanusa uvumi huu kwa kusema kwamba, ni malalamiko ambayo yamezagaa nchini Tanzania kiasi kwamba, kuna baadhi ya watu wamediriki hata kutengeneza Kanda ili kueneza uvumi huu. Haya ni mawazo yaliyonunuliwa kutoka nje, ili kuvuruga misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano wa kitaifa ambao watanzania kwa takribani miaka 50 iliyopita wamekuwa wakiufaidi.

Askofu Msonganzila anasema, hizi ni dalili za ukoloni mambokesho! Kinzani za kidini kwa madai kwamba, Serikali ya Tanzania inaongozwa na mfumo Kristo ni uzushi usiokuwa na msingi. Watanzania watakumbuka kwamba, wakati wa Azimio la Arusha, Serikali ilitaifisha shule zilizokuwa zinamilikiwa na kuendeshwa na Kanisa, ili kutoa fursa kwa watanzania wengi zaidi kupata fursa ya elimu.

Kanisa lilitambua na kuheshimu nia njema iliyooneshwa na Baba wa Taifa bila kunung'unika. Ikumbukwe kwamba, mikakati ya kichungaji katika sekta ya elimu ni sehemu ya Uinjilishaji wa kina unaofanywa na Kanisa Katoliki katika mchakato wa kukomboa mtu mzima: kiroho na kimwili, kumbe kumiliki na kuendesha shule katika viwango mbali mbali si jambo la nasibu bali ni sehemu ya vinasaba vya Kanisa Katoliki.

Hata baada ya kutaifishwa shule, watanzania wengi waliokuwa na kiu ya elimu walipata bila ya ubaguzi wowote, kinyume kabisa cha madai yanayotolewa na baadhi ya waamini kwa sasa! Kuna watanzania wengi ambao baadhi yao ni viongozi waandamizi Serikali wamesoma katika shule zilizotaifishwa au zilizokuwa zinamilikiwa na Kanisa, bila shaka hawa ni mashahidi makini wa hali halisi ilivyokuwa katika shule hizi.

Askofu Michael Msonganzila anasema, hizi ni zama za ukweli na uwazi, watanzania wanapaswa kufungua macho, masikio, mioyo na akili zao ili kuuona ukweli. Huu si muda wa malumbano, bali watu wawekeze katika elimu inayomwangalia mtu mzima: kiroho na kimwili, ili kuweza kuwajengea watoto wa kitanzania, kesho iliyo bora zaidi.

Elimu ya dini na elimu dunia zina nafasi yake. Watanzania wasikubali kutumiwa na watu wasiowatakia mema kwa kufanya ghasia na malumbano yasiyokuwa na tija kwa maendeleo yao. Wakumbuke daima kwamba, vita na ghasia hazina macho, kwa kujiingiza katika migogoro ya kidini, watapoteza hata kile kidogo walicho nacho kwa sasa! Ni wakati wa kujenga na kuimarisha mshikamano na umoja wa kitaifa dhidi ya maadui walioko ndani na nje ya Tanzania wanaotaka kulitumbukiza Taifa katika maafa ya udini.

Msitafute njia ya mkato katika maisha!




Katika maadhimisho ya kumbu kumbu ya mwezi mmoja tangu Baba Mtakatifu Francisko alipochaguliwa kuliongoza Kanisa, Jumamosi, tarehe 13 Aprili 2013 ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu iliyohudhuriwa na Wanajeshi wa Kikosi cha Zimamoto cha Vatican na Watawa wa Upendo kwenye Kikanisa cha Domus Sanctae martha, kilichoko mjini Vatican.

Papa amewakumbusha kwamba, hata katika mahangaiko, mateso na shida mbali mbali anazoweza kukabiliana nazo mwamini, kamwe asithubutu kutafuta njia ya mkato bali wajiaminishe kwa Mwenyezi Mungu. Waamini wa Kanisa la Mwanzo, kadiri ya Matendo ya Mitume, walijikuta wanaanza kulalamikiana na kubaguana katika huduma mambo ambayo yalikuwa yanadhohofisha umoja na mshikamano wa upendo miongoni mwa wafuasi wa Kristo. Mitume wakachukua uamuzi wa kuwakutanisha na kujadiliana kwa pamoja na hatimaye, wakapata suluhisho la matatizo yao.

Mitume walibainisha kwamba, dhamana yao ya kwanza ni kusali na kutangaza Habari Njema ya Wokovu; kumbe Mashemasi saba walioteuliwa walipewa dhamana ya kutoa huduma ya upendo ambayo ni mwendelezo wa huduma na mshikamano wa upendo unaofanywa na Mama Kanisa sehemu mbali mbali za dunia. Kristo yuko daima pamoja na wafuasi wake na kamwe hawezi kuwaacha wakaangamia.

Baba Mtakatifu anasema, hivi ndivyo ilivyotokea pale mitume wake walipokuwa wameelemewa na hofu pamoja na woga, akawatokea na kuwaambia wasiogope. Hata kama waamini wanakosea, wasikate tamaa, bali watambue kwamba, Yesu yuko pamoja nao. Wachunguze pale walipokosea, wajiwekee mikakati ya kusahihisha na kurekebisha pamoja na kujipa moyo wa kusonga mbele kwa imani na matumaini zaidi. Waamini kamwe wasitafute njia ya mkato katika maisha!

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR