click hapa kusikiliza tafakari ya masomo ya kesho.
NOVEMBER
JUMAPILI DOMINIKA YA 32 MWAKA C
RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
IBADA YA MISA YA KWANZA 12:15 – 1:45 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 2:00 – 3:50 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA TATU SAA 4:00-5:20 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:15 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:00 – 2:50 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA – MBWENI TETA.
IBADA YA MISA NI 3:00 – 5:00ASUBUHI
MASOMO YA DOMINIKA 32
SOMO LA 1: 2Mak. 7:1-2, 9-14
Ilitokea ya kuwa ndugu saba, pamoja na mama yao, walikamatwa kwa amri ya mfalme na kuteswa sana kwa mijeledi na mapigo ili kuwashurutisha kuonja nyama marufuku ya nguruwe. Mmoja akajifanya mnenaji wao, akasema, wataka kuniuliza nini juu yetu? Sisi tu tayari kufa kuliko kuzivunja amri za wazee wetu. Wa pili alipokuwa kufani alisema,wewe, mdhalimu, unatufarikisha na maisha ya sasa, lakini Mungu wa ulimwengu atatufufua sisi tuliokufa kwa ajili ya amri zake, hata tupate uzima wa milele. Na baada yake alidhihakiwa Yule wa tatu, naye mara alipoagizwa, alitoa ulimi wake, akanyosha mikono yake bila hofu akasema kwa ushujaa, kutoka mbinguni nalipewa hivi, na kwa ajili ya amri za Mungu navihesabu kuwa si kitu, na kwake natumaini kuvipokea tena. Hata mfalme na watu wake walishangazwa kwa roho ya kijana huyu, kwa jinsi alivyoyadharau maumivu yake. Akiisha kufa huyu, walimtesa wa nne na kumtenda mabaya yale yale. Naye alipokaribia kufa alisema hivi; ni vema kufa kwa kwa mikono ya mwanadamu na kuzitazamia ahadi zitokazo kwa Mungu, kuwa tutafufuliwa naye. Lakini kwako wewe hakuna ufufuo.
Somo 2: 2The.2:16 – 3:1-5
Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupatia faraja ya milelena tumaini jema, katika neema, awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neon na tendo jema. Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neon la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu; tukaokolewena watu wasio haki; wabaya; maana si wote walio na imani. Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na Yule mwovu. Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba unayafanya tuliyowaagiza, tena kwamba mtayafanya. Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.
INJILI:Lk. 20:27-38
Baadhi ya wasadukayo, wale wasemayo ya kwamba hakuna ufufuo, walimwendea Yesu, wakamwuliza, wakisema Mwalimu, Musa alituandikia ya kuwa, mtu akifiwa na ndugu yake mwenye mke, lakini hana mtoto, na amtwae huyo mke, ampatie ndugu yake mzao. Basi,kulikuwa na ndugu saba . na wa kwanza alioa mke, akafa hana mtoto; wa pili akamtwaa Yule mke, akafa hana mtoto; hata wa tatu akamwoa, na kadhalika wote saba, wakafa, wasiache watoto. Mwisho akafa Yule mke naye. Basi, katika ufufuo atakuwa mke wa yupi? Maana aliolewa na wote saba. Yesu akawaambia, wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kafufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo. Lakini, ya kuwa wafu hufufuliwa, hata na Musa alionyesha katika sura ya kijiti, hapo alipomtaja Bwana kuwa ni Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake.
Matangazo mbali mbali
Jumapili hii tarehe 10/11/13 kutakuwa na kikao cha Halmashauri ya Viwawa Parokia ya Boko, kikao kitafanyikia parokiani Saa 4:00 asubuhi mara baada ya ibada ya pili. Wajumbe ni viongozi wote wa Viwawa ngazi ya Vigango.
Agenda za kikao.
ü Maandalizi ya semina ya Tarehe 23/11/13 – Mbweni
ü Mapendekezo ya mipango ya mwaka 2014 – 2015
ü mengineyoendelea zaidi......
jdhibitisha ushiriki wako kwenye semina ya tarehe 23/11/13 kwa kulipa ada sasa ni tshng 5000 lipa kwa mhazini wako jumuiya, kigango au parokia.....tunawatakia maandalizi mema.