15
|
JUNI
SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU
MWAKA "A" 2014
MWAKA "A" 2014
RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
IBADA YA MISA YA KWANZA 12:15 – 1:45 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 2:00 – 3:50 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA TATU SAA 4:00-5:20 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:15 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:00 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA – MBWENI MPIJI.
IBADA YA MISA NI 3:00 – 5:00ASUBUHI
Zaburi:Tazama sala ya siku.
Dan.3:52-56
K. Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.
SOMO 1:Kut.34:4b-6, 8-9
Musa aliinuka
asubuhi na mapema, naye akakwea katika mlima wa Sinai, kama Bwana alivyomwamuru,
akazichukua hizo mbao mbili za mawe mkononi mwake. Bwana akashuka ndani ya lile
wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana. Bwana akapita
mbele yake, akalitangaza, Bwana , Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye
fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; Musa akafanya haraka,
akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu. Akasema ikiwa sasa nimepata
neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu maana ni watu wenye
shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.
SOMO 2:2Kor.13:11-14
Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni
mamoja, make katika Amani; na Mungu wa upendo na Amani atakuwa pamoja nanyi.
Salimianeni kwa busu takatifu. Watakatifu wote wawasalimu. Neema ya Bwana Yesu
Kristo, na pendo la Mungu. Na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.
INJILI:Yn.3:16-18
Yesu alimwambia Nikodemu: kwa maana jinsi hii Mungu
aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanae wa pekee, ili kila mtu amwaminiye
asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni
ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye
hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la
mwana pekee wa Mungu.