


![]() |
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Tundu Lissu akiwasili leo |
Mwenyekiti wa Bunge, Mh. Mussa Azan Zungu akiongozwa na Mpambe wa Bunge kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati alipositisha kikao cha Bunge cha asubuhi leo Novemba 26, 2014. |
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizugumza na Mbunge wa Viti Maalum Rachel Mashishanga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo Novemba 26, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Mbunge wa Urambo, Mh. Samuel Sitta (katikati) akiwatuliza na baadhi ya wabunge wa Upinzani, Bungeni mjini Dodoma leo Novemba 26, 2014 |
Nifuraha kwetu Kuona yale tunayofanya yana sifa na Utukufu kwa Mungu, tokea 2011 hadi leo 2014 utume wetu upo na unazidi kuimara, tunawashukuru sana Walezi wetu na Wadau wetu wote kwa michango yao mbali mbali, hapo juu vijana wa wa parokia ya Boko wakiwa na Paroko wa Parokia ya Kigenge Chini Jimbo kuu la Arusha |
Askofu Nzigirwa akiongoza Ibada ya Matawi Don Bosco, ikiwa ni siku pia ya Azimisho la Vijana Ulimwenguni ilikuwa mwaka 2012. |
![]() |
Mwenyekiti wa Kigango cha Mt. Rafael, Baada ya Semina ya Siku Moja iliyofanyika katika Kijiji cha Furaha Mbweni mwaka 2011 |
Baadhi ya Vijana wa Kigango cha Bunju, kwa sasa Parokia ya Bunju wakiburudisha kwenye Sherehe ya Pentekoste ilikuwa mwaka 2012. |
Hatimaye leo baba Mtakatifu Papa Francisco amempandisha kutoka askofu hadi kuwa askofu Mkuu askofu Beatus Kinyaiya, O.F.M. Cap (pichani) wa jimbo kuu Katoliki la Dodoma.
Askofu Beatus Kinyaiya alizaliwa Mei 9, 1957. Akapata daraja takatifu la Upadre katika shirika la Kimisionari la Wafranciscan Minor tarehe 25 juni, 1989.
Aliteuliwa kuwa askofu wa jimbo Katoliki la Mbulu tarehe 22 Aprili, 2006, nakusimikwa/ wekwa wakfu rasmi na Kardinali Polycarp Pengo kuwa askofu wa jimbo la Mbulu tarehe 2 Julai 2006.
Leo tarehe 06 Novemba, 2014 ameteuliwa kuwa askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Dodoma ambalo nalo limepandishwa hadhi na kuwa jimbo kuu.
Atasimikwa rasmi kuanza utume wake huo mpya katika jimbo hilo mwezi wa Januari, 2015.