Saturday, January 24, 2015

Walei na Kanisa letu

Tumsifu Yesu Kristo. Kwa mara nyingine tena tunakukaribisha katika mada hii ya utume wa walei, ili tuisikie sauti ya Mama Kanisa anayetuelekeza nini cha kufanya ili Kanisa lizidi kuwa hai na Injili ya Kristo isonge mbele kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu.

Thursday, January 22, 2015

18

 Januari
 Jumapili: Dominika ya 2 ya Mwaka "B".
SOMO  1. 1 Sam. 3:3b-10, 19

 Samueli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu; basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, mimi hapa. Akamwendea Eli kwa haraka, akasema mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena. Bwana akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, sikukuita, mwanangu; kalale tena. Basi Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake. Bwana akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akamtambua ya kuwa Bwana ndiye alimwita yule mtoto. Kwa hiyo Eli akamwambia Samweli, enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena Bwana; Samweli akaenda akalala mahali pake. Bwana akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! ndipo Samweli akasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Samweli akakua, naye Bwana alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha neno lake lo lote lianguke chini.

Tuesday, January 13, 2015

Mkutano Mkuu wa VIWAWA 31/01/2015

Mapendo sana!!!!!!
Ule Mkutano Mkuu wa VIWAWA, Parokia unafanyika tena mwaka huu, tukiwa na kumbukumbu nzuri ya Mafanikio yaliyotokana na Mkutano wa Tarehe 01/06/2013.


Monday, January 12, 2015

Mwongozo wa Sinodi ya Maaskofu kuhusu Familia arehe 4 hadi tarehe 25 Oktoba 2015

Mama Kanisa ameanza hija kuelekea maadhimisho ya Sinodi ya kumi na nne ya kawaida ya Maaskofu itakayofanyika mjini Vatican kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 25 Oktoba 2015 kwa kuongoza na kauli mbiu “Wito na Utume wa Familia katika Kanisa na Ulimwengu mamboleo”.

Sherehe za Mapinduzi leo Zanzibar

tunachukua nafasi hii kuwatakia siku njema na yenye amani katika sherehe ya mapinduzi ya Zanzibar.

Sunday, January 11, 2015

Masomo ya Tarehe 11/01/2015 mwaka B, wa Kanisa Dominika ya sikuku ya Ubatizo wa Bwana2015

11

 Januari
 Jumapili: ya Ubatizo wa Bwana.
SOMO  1. Isa. 42:1-4, 6-7

 Bwana asema: Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu. Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. Mwanzi uliopondeka hautavunjika, wala utambi utokao moshi hautazima; atatokeza hukumu kwa kweli. Hatazimia , wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake. Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufugwa.

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR