Tuesday, December 9, 2014
Desturi za Krismasi
Sherehe ya Krismasi imekuwa sikukuu muhimu sana katika tamaduni za mataifa yaliyoathiriwa na Ukristo. Kuna desturi nyingi zilizojitokeza katika karne zote za kusheherekea Krismasi. Sehemu ya desturi hizi zimeenea pia nje ya nchi za asili na hata kutumiwa na watu wasiofuata imani ya Kikristo.
- Pango la Noeli lililoanzishwa na Fransisko wa Asizi mwaka 1223 kijijini Greccio (Italia) na kuenea kila mahali kama sanaa inayoonyesha kwa njia mbalimbali jinsi Yesu alivyozaliwa.
- Mapambo ya krismasi: ni hasa nuru na taa za pekee. Alama za nyota kwa kukumbuka nyota iliyopeleka mamajusi hadi Bethlehemu inawekwa ndani na nje ya nyumba na maduka.
- Mti wa Krismasi - ni ishara ya pekee ya Krismasi yenye asili katika Ujerumani kusini-magharibi ya karne ya 16 hivi. Asili yake iko katika maigizo yaliyosimulia hadithi za Biblia na mti wa Paradiso unaohusiana na masimulizi ya dhambi la kwanza na ujumbe wa Kristo kama mwokozi anayekuja kuondoa dhambi hilo. Kutoka maigizo ya kanisani ishara ya mti uliopambwa matunda uliingia katika nyumba za Wakristo ambako ulipambwa zaidi kwa matunda, keki tamu na pipi kwa watoto. Umekuwa mapambo ya nyumbani kwa majira ya Krismasi. Tangu Krismasi kuwa nafasi muhimu kwa uchumi kuna pia maduka mengi yanayoweka miti hii na katika mazingira ya kibiashara uhusiano wake na mti wa Paradiso umesahauliwa mara nyingi.
- Zawadi za Krismasi - Martin Luther alitaka kuongeza umuhimu wa Krismasi kwa Wakristo ambao wakati wake walikuwa na desturi ya kuwazawadia watoto kwenye siku ya Mtakatifu Nikolasi tarehe 6 Desemba, wiki 2 kabla ya sikukuu. Hapo Luther alipendekeza kuhamisha zawadi kwa watoto kwenda siku ya kuzaliwa kwake Yesu ili wamkumbuke zaidi Yesu kuliko mtakatifu huyo. Hapo alirejea zawadi zilizopelekwa kwa Yesu na mamajusi kutoka mashariki kufuatana na taarifa ya Injili ya Mathayo mlango 2. Desturi ya kuwazawadia watoto kwenye sikukuu hii ilienea hadi kuwa desturi ya kupeana zawadi kati ya watu wa kila umri. Katika karne ya 20 desturi ilienea kiasi cha kuwa nafasi muhimu ya biashara. Katika nchi nyingi mwezi wa Desemba umekuwa mwezi wa mapato makubwa kushinda miezi mingine. Hata katika miji mikubwa ya nchi kama Dubai au Japani ambako Wakristo ni wachache desturi ya kupeana zawadi imeenea na mapambo ya Krismasi katika maduka yanataka kuwahamasisha wateja kununua zawadi za majira.
- Baba Krismasi / Baba Noeli
Sikuku ya Noel (Krismasi)
Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu ambako Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.
Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.
Jina
Kuna majina mawili yaliyo kawaida kwa Kiswahili kwa ajili ya sikukuu hii.- Krismasi inatokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo.
- Noeli inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokewa kutoka lugha ya Kifaransa "noël". Hilo ni ufupisho wa Kilatini "Natalis (dies)", "(siku ya) kuzaliwa".
Monday, December 1, 2014
Sunday, November 30, 2014
Maana ya Majilio katika maisha ya binadamu
Kwanza Majilio ni nini?
Majilio (pia: Adventi) ni kipindi cha liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo (kama vile Kanisa Katoliki, ya Waorthodoksi, Waanglikana na Walutheri) kinatangulia sherehe ya Noeli na kuanza mwaka wa liturujia. Kinaweza kudumu kati ya siku 22 na 40.
Jina lake kwa Kilatini ni adventus maana yake ujio (wa Yesu Kristo), lakini jina la Kiswahili ni sahihi zaidi kwa sababu linadokeza kuwa ujio wa Yesu ni kwa ajili yetu na kuwa alikuja zamani, anakuja kila siku na atakuja kwa utukufu mwisho wa dunia.
Maana ya Majilio katika Maisha ya Binadamu
Sisi binadamu hatuwezi kuishi daima katika hali ileile bila ya matazamio. Hasa kijana anatarajia mambo mapya tena mema. Hivyo tunajitahidi kuyapata. Asiyetazamia chochote amevunjika moyo, hana hamu ya kuishi. Lakini matazamio ya kibinadamu yakimfikia mtu hayamridhishi moja kwa moja. Kristo tu anatimiza hamu zote kwa kumkomboa kutoka unyonge. Majilio yanatukumbusha kila mwaka matarajio ya kweli na hivyo yanaamsha hamu ya kuishi kwa bidii ya kiroho.
Urefu wa Majilio unategemea siku inayoangukia Noeli, kwa kuwa ni lazima yawe na Jumapili nne. Hivyo basi yanaanza kwa Masifu ya Jioni ya kwanza ya Jumapili inayoangukia tarehe 30 Novemba au tarehe ya jirani zaidi; yanakwisha kabla ya Masifu ya Jioni ya kwanza ya Noeli.
Kwa jumla ni kipindi cha toba: rangi yenyewe ni zambarau; haziruhusiwi sherehe za fahari; ala za muziki na maua vinaweza kutumika kwa kiasi tu. Masharti hayo yanalegezwa katika Jumapili ya tatu kwa sababu ya furaha ya kuona tunakaribia sherehe yenyewe.
Katika kipindi hicho tunaadhimisha tumaini la Israeli lililotimizwa Yesu alipokuja katika unyenyekevu wa umbile letu; pia tunangojea arudi kwa utukufu. Kama alivyotekeleza ahadi mara ya kwanza, atazitekeleza pia mara ya pili, ingawa kwake miaka elfu ni kama siku moja tu. Kati ya majilio hayo mawili, Bwana anatujilia mfululizo kifumbo katika sakramenti (hasa ekaristi) na katika maisha ya kila siku kwa njia ya matukio na watu (hasa maskini). Basi tunapaswa kuwa tayari daima kumpokea ili siku ya mwisho tukamlaki, naye atukaribishe kwenye uzima wa milele. Pia tunapaswa kumuomba aje kutukomboa, yeye aliye tumaini letu.
Katika safari ya Majilio watu watatu wanatuongoza tukutane na Yesu: 1. Isaya nabii wa tumaini, mwenye kipaji cha kutokeza matazamio ya binadamu na kumhakikishia atatimiziwa na Mwokozi. 2. Yohane Mbatizaji, mwenye kuhimiza toba kwa kuwa tunapaswa kupindua maisha yetu ili tukutane vema na Kristo. 3. Maria, bikira aliyekuwa tayari kumpokea Masiya kwa upendo na kushirikiana naye katika kutimiza mpango wa wokovu.
Tukiwafuata hao watatu tunaweza kujipatia maadili yale yanayotuandaa kumpokea Mwokozi anapotujilia: ndiyo matunda maalumu tunayotarajiwa kuyachuma wakati wa Majilio: 1. Kukesha katika imani, sala na kutambua ishara za Bwana kutujilia katika nafasi yoyote ya maisha na mwishoni mwa nyakati. 2. Kuongoka kwa kufuata njia nyofu. 3. Kushuhudia furaha inayoletwa na Yesu kwa kuwa na upole na uvumilivu kwa wenzetu, kwa tumaini la kuwa bidii zetu zinawahisha ufalme wa Mungu wenye heri isiyo na mwisho. 4. Kutunza unyenyekevu kwa kufuata mifano ya maskini wa Injili ambao ndio waliompokea Mkombozi.
Majilio (pia: Adventi) ni kipindi cha liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo (kama vile Kanisa Katoliki, ya Waorthodoksi, Waanglikana na Walutheri) kinatangulia sherehe ya Noeli na kuanza mwaka wa liturujia. Kinaweza kudumu kati ya siku 22 na 40.
Jina lake kwa Kilatini ni adventus maana yake ujio (wa Yesu Kristo), lakini jina la Kiswahili ni sahihi zaidi kwa sababu linadokeza kuwa ujio wa Yesu ni kwa ajili yetu na kuwa alikuja zamani, anakuja kila siku na atakuja kwa utukufu mwisho wa dunia.
Maana ya Majilio katika Maisha ya Binadamu
Sisi binadamu hatuwezi kuishi daima katika hali ileile bila ya matazamio. Hasa kijana anatarajia mambo mapya tena mema. Hivyo tunajitahidi kuyapata. Asiyetazamia chochote amevunjika moyo, hana hamu ya kuishi. Lakini matazamio ya kibinadamu yakimfikia mtu hayamridhishi moja kwa moja. Kristo tu anatimiza hamu zote kwa kumkomboa kutoka unyonge. Majilio yanatukumbusha kila mwaka matarajio ya kweli na hivyo yanaamsha hamu ya kuishi kwa bidii ya kiroho.
Majilio katika liturujia ya Katoliki
Katika mwaka wa liturujia ya Kanisa la Katoliki, sherehe ya Noeli inaandaliwa na kipindi cha Majilio ambacho kina mambo mawili: kinakumbusha Mwana wa Mungu alivyotujilia mara ya kwanza, na papo hapo kinatuandaa kumpokea atakapotujilia tena siku ya mwisho. Kufuatana na hayo kina sehemu mbili: hadi tarehe 16 Desemba kinahusu zaidi kurudi kwa Bwana; siku nane za mwisho kinatuelekeza moja kwa moja kuadhimisha kuzaliwa kwake.Urefu wa Majilio unategemea siku inayoangukia Noeli, kwa kuwa ni lazima yawe na Jumapili nne. Hivyo basi yanaanza kwa Masifu ya Jioni ya kwanza ya Jumapili inayoangukia tarehe 30 Novemba au tarehe ya jirani zaidi; yanakwisha kabla ya Masifu ya Jioni ya kwanza ya Noeli.
Kwa jumla ni kipindi cha toba: rangi yenyewe ni zambarau; haziruhusiwi sherehe za fahari; ala za muziki na maua vinaweza kutumika kwa kiasi tu. Masharti hayo yanalegezwa katika Jumapili ya tatu kwa sababu ya furaha ya kuona tunakaribia sherehe yenyewe.
Katika kipindi hicho tunaadhimisha tumaini la Israeli lililotimizwa Yesu alipokuja katika unyenyekevu wa umbile letu; pia tunangojea arudi kwa utukufu. Kama alivyotekeleza ahadi mara ya kwanza, atazitekeleza pia mara ya pili, ingawa kwake miaka elfu ni kama siku moja tu. Kati ya majilio hayo mawili, Bwana anatujilia mfululizo kifumbo katika sakramenti (hasa ekaristi) na katika maisha ya kila siku kwa njia ya matukio na watu (hasa maskini). Basi tunapaswa kuwa tayari daima kumpokea ili siku ya mwisho tukamlaki, naye atukaribishe kwenye uzima wa milele. Pia tunapaswa kumuomba aje kutukomboa, yeye aliye tumaini letu.
Katika safari ya Majilio watu watatu wanatuongoza tukutane na Yesu: 1. Isaya nabii wa tumaini, mwenye kipaji cha kutokeza matazamio ya binadamu na kumhakikishia atatimiziwa na Mwokozi. 2. Yohane Mbatizaji, mwenye kuhimiza toba kwa kuwa tunapaswa kupindua maisha yetu ili tukutane vema na Kristo. 3. Maria, bikira aliyekuwa tayari kumpokea Masiya kwa upendo na kushirikiana naye katika kutimiza mpango wa wokovu.
Tukiwafuata hao watatu tunaweza kujipatia maadili yale yanayotuandaa kumpokea Mwokozi anapotujilia: ndiyo matunda maalumu tunayotarajiwa kuyachuma wakati wa Majilio: 1. Kukesha katika imani, sala na kutambua ishara za Bwana kutujilia katika nafasi yoyote ya maisha na mwishoni mwa nyakati. 2. Kuongoka kwa kufuata njia nyofu. 3. Kushuhudia furaha inayoletwa na Yesu kwa kuwa na upole na uvumilivu kwa wenzetu, kwa tumaini la kuwa bidii zetu zinawahisha ufalme wa Mungu wenye heri isiyo na mwisho. 4. Kutunza unyenyekevu kwa kufuata mifano ya maskini wa Injili ambao ndio waliompokea Mkombozi.
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...