Marehemu Padre Anthony Chonya, alikuwa Padre wa Jimbo la Iringa, Mzaliwa wa Parokia ya Malangali na Parokia yake ya mwisho kuitumikia ni Parokia ya Magungu Mgololo.
Monday, January 26, 2015
Saturday, January 24, 2015
MASOMO YA TAREHE 25/01/2015 jumapili ya 3 ya mwaka B wa kanisa
25
Januari
Jumapili: Dominika ya 3 ya Mwaka "B".SOMO 1. Yon. 3:1-5, 10
Neno la bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema, ondoka uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukaihubiri habari nitakayo kuamuru. Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikua mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu, Yona akaanza kuingia mjini mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.
Walei na Kanisa letu
Tumsifu
Yesu Kristo. Kwa mara nyingine tena tunakukaribisha katika mada hii ya utume wa walei, ili tuisikie sauti ya Mama Kanisa
anayetuelekeza nini cha kufanya ili Kanisa lizidi kuwa hai na Injili ya
Kristo isonge mbele kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu.
Thursday, January 22, 2015
18
Januari
SOMO 1. 1 Sam. 3:3b-10, 19
Samueli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu; basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, mimi hapa. Akamwendea Eli kwa haraka, akasema mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena. Bwana akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, sikukuita, mwanangu; kalale tena. Basi Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake. Bwana akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akamtambua ya kuwa Bwana ndiye alimwita yule mtoto. Kwa hiyo Eli akamwambia Samweli, enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena Bwana; Samweli akaenda akalala mahali pake. Bwana akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! ndipo Samweli akasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Samweli akakua, naye Bwana alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha neno lake lo lote lianguke chini.
Monday, January 19, 2015
Tuesday, January 13, 2015
Mkutano Mkuu wa VIWAWA 31/01/2015
Monday, January 12, 2015
Mwongozo wa Sinodi ya Maaskofu kuhusu Familia arehe 4 hadi tarehe 25 Oktoba 2015
Mama
Kanisa ameanza hija kuelekea maadhimisho ya Sinodi ya kumi na nne ya
kawaida ya Maaskofu itakayofanyika mjini Vatican kuanzia tarehe 4 hadi
tarehe 25 Oktoba 2015 kwa kuongoza na kauli mbiu “Wito na Utume wa
Familia katika Kanisa na Ulimwengu mamboleo”.
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...