Friday, January 18, 2013

Historia ya Ukristo


Historia ya Ukristo

Sanamu ya Yesu Kristo mkombozi ilijengwa Rio de Janeiro (Brazil) ni kubwa kuliko zote zilizopata kutengenezwa.
                                                  UKRISTO....
Ukristo ni Dini  inayomwamini Mungu  pekee kama alivyofunuliwa na Yesu Kristo ambaye ndiye mwanzilishi wake.
Dini hiyo, iliyotokana na ile ya Wayahudi, inayolenga kuenea kwa Binadamu  wote, na kwa sasa ni kuu kuliko zote duniani, ikiwa na wafuasi zaidi ya bilioni mbili.
Kitabu chake kitakatifu kinajulikana kama Bibilia. Ndani yake inategemea hasa Injili na vitabu vingine vya Agano jipya.
Asili
Chimbuko la Ukristo ni kuwepo kwa mtu aliyezaliwa takriban miaka 2000 iliyopita huko mashariki ya kati, katika kijiji cha Bethlehemu kilichopo hadi hivi leo kwenye mipaka ya Palestina, naye alikuwa akiitwa Yesu wa Nazareti au mwana wa Yosefu mchonga samani; mama yake akifahamika kwa jina la Bikira Maria.
Masiya Yesu
Ukristo ni matokeo ya utume wa Yesu, uliopokewa na waliomwamini kuwa ndiye Masiya, yaani Mpakwamafuta (Kristo kwa Kigiriki), mkombozi aliyetimiliza ahadi za Mungu kwa uzao wa Abrahamu.Utabiri wa kuja kwake ulianzia katika bustani ya Edeni pale Mungu alipomwambia mwanamke ."uzao wako utamponda kichwa" nyoka, yaani shetani.

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR