Thursday, March 7, 2013

Historia ya Makanisa Zanzibar

1800 – 1900

WAKATOLIKI, MAKUNDI YA WAKIRISTO WASIOPENDA MIKUTANO ASMI, VITA AU GHASIA (QUAKERS) NA UJUMBE WA VYUO VIKUU KWA AFRIKA YA KATI ( UMCA)

Baada ya Wareno kurudi nyuma Wakiristo kidogo tu Wakigoa ndio waliobakia Zanzibar.  Wakiristo hawa hawakuwa na kanisa la kufanyia Ibada lakini waliweza kuifanya hai jumuia yao kwa kwa kuifanya ibada zao kibinafsi.  Baadae katika miaka 1800 makundi ya watu wa wamagharibi yalianza kujumuisha wamisionari na wachungaji wamisionari waliokuwa wakipita pita mara chache na wachungaji katika meli bandarini.  Katika mwaka 1844 wamisionari wa kikiristo zaidi wa kudumu waliwasili Afrika mashariki kwa kupitia mchungaji wa kilutheri Joseph Krapf na wafuasi wawili ambao walifanya kazi kwa ajili wa Jumuia ya kimisheni ya kanisa la kiingereza (English Church Missionary Society).  Wakifanyakazi, Mombasa, walitembelea Zanzibar na miaka michache mbeleni walitoa kamusi bora kabisa la Kiswahili lakini hawakuwahi kuanzisha kanisa ndani ya visiwa hivyi. 
Ukuwaji wa harakati dhidi ya utumwa ndani ya Uingereza ulishajiisha raghba ya wamisionari wakiristo, ikikuzwa na hotuba ya David Livingstone aliyoitoa mwaka 1857 akiomba Uingereza kupeleka wamisionari na wafanyakazi Afrika.  David Livingstone alilingania kwamba mwisho wa utumwa utakuwepo tu kupitia “ biashara na ukiristo”.  Baadae Livingstone alitumia siku nyingi tu Zanzibar ambao alipatiwa nafasi ya kutumia nyumba ya Sultani.
Hotuba zake zilipelekea kuundwa kwa ujumbe wa Vyuo Vikuu  kwa Afrika ya Kati (UMCA).  Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati ulikuwa ni mashirikiano baina ya kitivo na wanafunzi waliopitia vyuo vikuu vya Oxford and Cambridge, ambao baadae tu waliungana na mashabiki kutoka vyuo vikuu vya Durham na Dublin.  Katika mwaka 1860 walimchagua Charles Mackenzie kama ni “Askofu wa Afrika ya kati” na ilipofikia mwezi wa Oktoba wa 1860 alikuwa njiani kuelekea huko Afrika ya Kati.
Lengo la ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya kati (UMCA) lilikuwa ni kufikisha dini ya kikiristo kwa watu wengi sana waliokuwa Afrika ya Kati, kuzunguka ziwa Nyasa, ambalo Livingstone alilizungumzia kwa ufanisi.  Kwa ajili hiyo, baada ya kufika Afrika Kusini Askofu Mackenzie na wafuasi aliokuwa nao walisafiri kwa boti mpaka mto Zambezi na baadae hadi mto shire kuasisi ujumbe wa mwanzo wa ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya Kati katika Afrika katika sehemu iliyojulikana kama Magomero.
Wakati ujumbe huu na eneo lake ulichukuana na jina na ari ya jumuia mama, Ujumbe huu ulishuhudia   kushindwa kwa aina yake kutekeleza malengo yake.  Maradhi na njaa na ukame uliwakumba wamisionari wa mwanzo na kupelekea kufa kwa askofu.  Kundi hili lililazimika kuondoka katika eneo hilo ndani ya kipindi
cha miaka mitatu kwa sababu eneo hilo lilikuwepo mbali sana na upatikanaji wa bidhaa kutoka nje na vituo vya mawasiliano, eneo hilo halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya kwa wale ambao hawana uzoefu na mazoea na hali ya hewa ya hapo na pia eneo halikuwa na utulivu wa kisiasa.  Askofu mpya, George Tozer, kwanza alijaribu kuupeleka ujumbe maili 200 mafikio ya mtiririko wa mto kuelekea eneo la muanuko lakini hata hivyo eneo hilo mara tu  liligundulika kuwa halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya na kwa hiyo lilihamwa kwa miezi hivi tu.
Wakichukua bidii za makusudi, ili kutorejea makosa yaliyopita viongozi wa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) waliangalia uwezekano wa kituo au eneo jengine ambalo litatumika kuweza kufika kati kati ya Afrika.  Maeneo mbali mbali yalifikiriwa kutumika kama Kisiwa cha Johanna,  maeneo katika mwambao wa Afrika Kusini lakini kwa bahati Zanzibar ilikubalika kutumika kutokana na muundo mzuri wa njia za mawasiliano, upatikanaji mzuri wa bidhaa za chakula na wingi wa upatikanaji nguvu kazi bora.  Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) uliobakia uliwasili Zanzibar tarehe 31/08/1864.
Ujumbe huu ulipowasili ulipokewa na wamisionari wakatoliki wa Kifaransa.  Wamisionari wa kikatoliki waliwasili mwanzo Zanzibar kwa kiasi ya miaka minne kabla ya wamisionari wa kiingereza.  Katika mwezi Septemba mwaka 1860 Abbe Favat ambaye alikuwa Mfaransa mdini  maarufu mwenye nguvu alitiliana mkataba na Seyyid Said kumruhusu yeye Abbe Favat kuhamishia Makao Makuu yake katika Kisiwa cha Reunion na kuwa Zanzibar kufikia mwezi Disemba kikundi chake cha “mapadri wawili wasio watawa na watawa sita wa kike” (“Filler de Marie”) walikuwa wakiishi katika makaazi ya watawa ambayo pia yalikuwa na kanisa dogo hapo Shangani.  Jengo hili la watawa linasemekana na lilijengwa katika mwaka 1860, lakini ujenzi huu inawezekana ulikuwa ni matengenezo makubwa ya nyumba iliyokuwepo kabla.  Kanisa dogo katika jengo hili lilikuwa ni kanisa la kwanza lililojengwa Zanzibar kwa miaka 200.
Ruhusa iliyotolewa na Sultan Majid kwa Wafaransa hawa kuanzisha duka ndani ya Zanzibar ilitafsiriwa kama ni juhudi za Sultani za kuweka “ uwiano wa nafasi kubwa waliokuwa nao Waingereza Zanzibar kwa kuwakaribisha wapinzani wao wakuu wa kizungu.”  Ikiwa ushindani wa kisiasa ndio uliompelekea Sultan Majid za kukaribisha pamoja matawi tofauti ya wamisionari wakiristo hata hivyo matokeo hayakuwa hayo kwani kwa upande wa wamisionari hawa hakukuwa na msuguano wowote.  Mahusiano yao mazuri makundi hayo mawili ya wamisionari ulitokana na ukweli kwamba Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati wa kianglikana (UMCA Anglicans) ulikuwa ni ujumbe wa watu watukufu ambao wenye mafunzo ya kikatoliki ya kiengereza (Anglon Catholic Learnings)
Wamisionari wakifaransa walikuwa makini kuepuka matatizo yoyote Zanzibar “kwa kutambua uhalisia wa maisha ulivyo ndani ya nchi ya kiislamu ya Zanzibar, Wafaransa kuanzia 1862 wafuasi wa Holy Ghost Order, waliamua kujikita katika maeneo maalum kama ya elimu, shughuli za uchungaji kwa jumuia ndogo ya mjini ya magoa wakatoliki na huduma za afifu na walifungua hospitali ya mwanzo iliyopendekezwa na Sultani ya kizungu.  Kwa hili waliojenga maoni mazuri kwa warabu.
Juu ya ukarimu wa watu wa Zanzibar, Wazanzibar hawa kidogo hawakuwa na azma yoyote kufuata imani ya wageni hawa wapya.  Wamisionari wa kikatoliki walilielewa hili lakini waliamini kwamba kundi kubwa la wafuasi wapya wa dini hii ya kikiristo litaweza kupatikana masafa machache kuvuka mlango bahari wa Zanzibar huko Tanzania Bara.  Walipeleka ujumbe mdogo Bagamoyo katika mwambao wa Tanzania Bara katika mwaka 1868 na kwa sehemu kubwa walitumia nafasi walizonazo Zanzibar kama ni makao makuu ya kuzidisha harakati zao Tanzania Bara.  Harakati hizi ikiwemo ujenzi wa “ Hospitali ya Kifaransa”  ndani ya Bagamoyo.
“ Hospitali ya Kifaransa”  ndani ya Zanzibar ilijengwa mkabala na jengo la watawa.  Hospitali ilimalizwa kujengwa na kuanza kazi kufikia mwaka 1890.  Kipindi hicho wakatoliki walien delea kutumia uhusiano mzuri na majirani zao wa Zanzibar, wakipata ruhusa ya kujenga kanisa la mtakatifu Joseph katika mwaka 1894. (Cathedral of Saint Joseph in 1894).  Jiwe la msingi la kanisa hili kuu liliekwa tarehe 10 Julai 1896.  Misa ya mwanzo katika kanisa hili kuu jipya iliendeshwa na Askofu Allegeyer katika usiku wa krismas 1898. 
Kadri ya wakati ulivyokuwa ukienda, hospitali hii ya Zanzibar ilipungua umuhimu wake na jengo hilo likafanywa kuwa ni skuli.  Hii ilikuwa ni skuli ya kitawa ya mtakatifu Joseph (St. Joseph Convent School).
Wamisionari wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) hawakuzubaa katika kipindi hichi.  Akianzia kwanza kuishi katika nyumba Mambo Msiige, katika eneo la Shangani, ambapo haikuwa mbali na ujumbe wa Kifaransa, Muingereza mchapa kazi shupavu alianzisha ustawi wa majengo ya ukubwa wa kuvutia na ya aina tofauti.  Kwanza walinunua sehemu ya ardhi ya kilimo Kiungani pembezoni mwa mji wa Zanzibar Kaskazini.  Ujenzi wa “bweni kwa ajili ya vijana watumwa walioachiwa huru” uliendelea katika eneo hilo kufikia mwaka 1866.  Karibu ya hapo mava sehemu ya kuzikia ilianzishwa, na hadi leo mava hii inayo baadhi ya mabaki ya wakiristo wa mwanzo wa Zanzibar.
Baadae ilinunuliwa ardhi nyengine katika mwaka 1873, ardhi hii ilikuwa karibu na kitovu cha mji ambalo ni jengo kubwa zima la mjini ambalo liliwahi kuwa uwanja wa soko kongwe, ambapo watumwa walikuwa wakiuzwa,  Mara wito ulitolewa wa fedha kusaidia ujenzi wa kanisa katika eneo hilo ambao uovu huo wa biashara ya utumwa ulifanyika.  Huu ulikuwa mwanzo kanisa kuu la kristo (Christ Church Cathedral).
Mwaka uliofuata Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) walinunua ardhi ya kilimo Mbweni kusini mwa mji karibu na bahari.
Wamisionari wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya kati (UMCA) walipanga kujaza milki zao kwa majengo ya kidini na yasiyokuwa ya kidini.  Katika mwaka 1882 walianzisha ujenzi wa kanisa la parokia la mtakatifu John (St. John’s Parrish Church) huko Mbweni.  Karibu ya kanisa hilo walijenga kijiji na shamba dogo kwa ajili ya waliokuwa watumwa zamani na pia walijenga “Makaazi ya watoto wadogo wa kiume wa kilimani”,  ambayo baadae iligeuzwa  skuli ya wasichana.  Huko Mbweni walijenga karakana nyingi tu za elimu amali kwa ajili ya kuwafunza wafuasi wapya wa dini stadi muhimu na baadae kuwa Chuo cha kidini cha Mtukufu Mark,  ambacho baadae kilihamishiwa kiungani.
Jiwe la msingi la kanisa kuu la ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA Cathedral) liliekwa mwaka 1873 katika siku ya siku kuu ya krismas katika eneo la mjini.  Uwanja wa soko kongwe ulianza kujazwa majengo ya ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati.
“Jumba la Mkunazini” lilijengwa katika mwaka 1875 na kanisa mara baada ya kujengwa jumba la kunazini lilihamisha makao makuu yake kutoka Mambo Msiige na kuwa Mkunazini.  Zahanati ilijengwa katika mwaka 1877, hatimae iligeuzwa kuwa hospitali yenye kutoa huduma kamili katika mwaka 1893. Skuli ya Mtakatifu Mon`ica, nyumba ya kasisi mkuu na Askofu ilijengwa katika uwanja wa soko kongwe.  Jengo hilo la skuli ya Mtakatifu Monica bado mpaka leo linatumika kama ni hostel/dahalia Mtukufu Monica.
Mwenye kustahiki sifa ya mafanikio haya ilikuwa hakika ni kanisa kuu la kristo. Mradi usio wa kibiashara ambao ulisimamiwa binafsi na Askofu wa tatu wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati Edward Steere, utabakia kuwa moja ya mifano ya kuvutia na bora wa usanifu majengo ndani ya Afrika uliofanywa na wakiristo wa mwanzo.
Wakati eneo lake lilijazwa na haiba nzuri ya shinikizo la kidini, ukaribu wake na kijito kidogo chenye manukato ilisababisha baadhi ya watu kutia wasiwasi juu ya athari zake kwa afya za wamisionari.  Kijito hicho kidogo ambacho kilitambulika kama ni mfano wa mfereji wa venice huko Italy (Venetian Canal) kwa maelezo ya kikanisa kilikuwa kiukweli hasa ni topetope zenye kunuka wakati wa kupwa kwa maji.  Eneo hili liliacha kutoa moshi wenye kunuka na kudhuru katika miaka ya 30 (30’s) baada ya kijito hicho kufunikwa na barabara, moshi ambao uliendelea kujitokeza kwa masiku wakati wa kujaa  na kupwa maji.
Haiba binafsi ya ushiriki katika ujenzi wa Daktari Steer unaweza kuonekana na wengi juu ya mabadiliko aliyoyafanya kwa ramani zilizoletwa kutoka Uingereza na juu ya majaaliwa ya nguzo za mawe ambazo husimamishwa karibu na nyuma ya ukumbi wa kanisa.  Nguzo hizi zilitiwa kipindi ambacho Askofu alikuwa safarini Tanzania Bara kwa kazi za kanisa.  Kwa hivyo, utiaji huo wa nguzo hizo ulikosa usimamizi wake.  Wafanyakazi hao walizitia nguzo hizo kwa kusimamisha wima kama alivyoelekeza Askofu lakini kwa bahati mbaya walizigeuza juu chini juu.  Baada kurejea Askofu alizichunguza na kuamua zibakie kama zilivyo,kama zinavyoonekana leo.  Hii ilitokana na azma yake ya kushindikiza kazi iendelee bila ya kurudi nyuma.
Thamani hasa kubwa ya juhudi zake za usanifu majengo ni Paa la kanisa kuu.  Akikumbuka matokeo  yasiopendeza wakati akijaribu kufanya matengenezo la paa lililooza la kanisa lake kongwe la Kiingereza, Askofu Steer alidhamiria kujenga paa kwa kutumia muda mrefu.

Aliamua kujenga paa la zege badala ya kutumia mbao kwa sababu ya kuhofia mbao hizo kuharibiwa na mchwa na hatari ya moto na hakuweza kujenga paa hilo kwa kutumia vifaa vya chuma kwasababu hakuwa na fedha ya kugharimia.Alitumia vifaa vya kienyeji katika ujenzi, alichanganya saruji na kokoto katika juhudi zake za kujenga paa kubwa lenye upana wa futi 28.5.  Ilikuikamilisha kazi hii alitumia mbea moja ya chombo kilicotengenezwa Uingereza mbacho kililetwa hali ya kuwa hakijaunganishwa pamoja.  Mashine hii iliekwa kwenye eneo la ujenzi ikiwa na viringi vilivyotiwa ili kuweza “kuzungushwa zungushwa kutoka sehemu moja kwenda nyengine pale ambapo kipande kimoja cha paa kinapomalizika kutiwa”.   Pale ambapo muhimili unapotaka kuondoshwa kundi kubwa la watu ilibidi kukusanyika pamoja.  Mkusanyiko huu wa watu unakuwa unatweta wakati vifaa vya kujengea jukwaa vinabomolewa, na huachwa kushangaa na kidogo na kukata tamaa pakiwa hapakutokea lolote.  Paa ambalo watu wote  hawakutegemea kuchukua muda bila ya kuanguka sasa limeweza kubakia zaidi ya karne moja/miaka 100.

Mfalme ambae kwa wakati huo alikuwa Seyyid Barghash alivutiwa sana na aliamua kutoa saa kubwa, ili kuupamba mnara wa kengele ambao uliwekwa pembe ya kusini magharibi ya jengo.  Kwa bahati mbaya haikuwepo saa katika ramani ya mwanzo.  Uamuzi wa busara wa kisiasa kupokea na kuiweka zawadi ya Sultani ulipelekea marekebisho kufanywa juu ya mnara na kuufanya mwembamba na mrefu zaidi.  Uamuzi huo kwa upande mwengine uliathiri pia zawadi zawadi nyengine ya seti nzuri ya kengele 25, seti za mlio wa saa ambazo ziliweza kupiga milio mirefu.  Hata hivyo ukubwa  na uzito wa seti hizo ulikuwa hauwezi kubebwa na mnara huo mwembamba.  Kengele 13 tu zilitiwa kwenye mnara huo na kengele  zilizobakia zilitawanywa kwa makanisa mengine na maskuli.
Wakati shughuli zote hizi zikiendelea katika kisiwa mama, wamisionari kutoka jumuia ya kirafiki ya kidini, the Quakers walianzisha makaazi karibu kabisa na kisiwa cha Pemba.  Quakers walifika Zanzibar mapema kufikia mwaka 1865, wakati huo walikuja kama ni waajiriwa wa kampuni za kibiashara za watu wa Magharibi.  Lakini Juu ya hivyo, mpaka ilipofikia  tarehe 20/Januari/1897 ndipo ujumbe wa kudumu wa Quaker ulianza mahala panapoitwa Banani ambapo ni karibu na kitivu cha ghuba ya Chake Chake mwambao wa Magharibi ya Pemba.
Kama  vile ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati, kichocheo cha fedha kwa ajili ya ujumbe wa Pemba zilitokana na raghba za vita dhidi ya utumwa alizokuwa nazo kila Quaker.   Kuanza hapo tena baadae utumwa ulipigwa marufuku rasmi katika visiwa hivyi ingawa maisha ya wengi waliokuwa watumwa kabla hayakubadilika.Kwa wale watumwa waliohama katika maeneo ya wale waliokuwa wakiwamiliki walikosa makaazi ya kuishi na hofu kubwa ilienea juu ya kuwepo vikundi visivyofuata utawala wa sheria vikizunguka zunguka sehemu za ma shambani.
Ujumbe wa Quaker, kwa maana hio ilibidi uwe ujumbe “Chapakazi” ili watumwa walioachiwa huru waweze kupata kazi na kusoma biashara.  Kiongozi wa ujumbe huu Theodore Bartt bila hata ya kufika Pemba, alisema katika ukumbi wa mkutano ndani ya Uingereza “Ni jambo mwafaka na sahihi kwake yeye mtu alieachiwa huru kumiliki shamba kubwa ndani ya Kisiwa hichi na kuonyesha dunia/ulimwengu kwamba watu walioachiwa huru watafanya kazi kwa bidii na uaminifu na kuwa wastahamilivu na kujitahidi kujenga maisha yao."
Theodore Buft aliamini kwamba biashara na ukiristo ilikuwa ndio njia ya uongofu na kuweza kuweza kuelimika.


Watumwa na Waliobadili Dini

Ujumbe wa Quaker kwa Pemba ulikuwa ni mlolongo wa karibu zaidi wa wakiristo wa uasisi wa “Mji huru”  ndani ya Afrika ya Mashariki kwa ajili ya makaazi ya watumwa walioachiwa huru.  Kwa miaka, jeshi la majini la kifalme walileta makundi kwa makundi watumwa kwa kwa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya waliowakamata kutoka bahari kuu.  Watu hawa walioachiwa huru walikuwa rahisi kwao kugeuzwa na kuwa wakiristo na kwa kweli wengi katika wao waligeuka kuwa wafuasi wa dini ya kikiristo.
Lakini juu ya hivyo, wingi wa wakiristo hawa wapya na mahitaji yao maku bwa yalikuwa ni changamoto kwa raslimali na subira ya wafadhili wao.  Wakiangalia demografia wamisionari waliona njia pekee ya kuwahudumikia wakiristo wapya ni kuanzisha chimbuko la Padri wa kiafrika.
Kwa hivyo wote wakatoliki na waprotestanti walifanya bidii kuwajumuisha makundi ya kienyeji shughuli na mambo ya kanisa na hii yote ilipelekea kujua na kufunza mtumishi bora kwa ajili ya kuendesha shughuli za kidini.
                                            
Kwa Zanzibar harakati zote hizi zilikuwa katika eneo la Kiungani ambapo kwanza ilianzishwa “dahalia kwa watumwa vijana walioachiwa huru”, na baadae “Chuo cha Mafunzo ya ualimu cha Mtakatifu Andrew” na baadae “Chuo cha kidini/theolojia” kila moja kati ya hivyo kilijaribu kuwafunza na kutathmini matokeo ya vijana wa kiafrika.  Kiasi cha wanafunzi 50 kwa kipindi kimoja cha wakati waliishi na kusoma Kiungani.  Mitaala ilisisitiza heshima, elimu, imani na michezo.  Wanafunzi wazuri walifanywa kuwa walimu na wanafunzi bora kuliko wote walifanywa kuwa mapadri.
Jambo moja la kuvutia juu ya michezo iliyoanzishwa kwa ajili ya wanafunzi wa Kiungani ni kwamba ilifanya baadhi ya mashindano ya kwanza ya timu mjumuisho ndani ya Afrika.  Timu hiyo ya skuli mara walicheza dhidi ya makundi ya mabaharia wazungu.  Mchezo wa Kriketi ulianzishwa mwanzo katika mpira wa miguu lakini hata hivyo mchezo wa mpira wa miguu ulipendwa zaidi kwani makundi kwa makundi ya watu walikuwa wakikusanyika kuangalia mpira wa miguu.  Inaaminika kwamba kanisa iliendeleza michezo kusaidia kuwafunza waafrika maadili mapya ya jumuia, ufuataji wa sheria, kuweka wakati, kufanyakazi kwa pamoja na mashirikiano na maofisa husika.  Wanafunzi wa kizanzibari walicheza mechi/michezo hii kwa hamu na raghba na umahiri wao wa mchezo wa mpira ulijenga mshangao na fadhaa kwa wapinzani wao.  Lakini lisilosahaulika zaidi walilojifunza ni kwamba wao wanaweza kufanikiwa katika mchezo wowote na sio mpira wa miguu tu.
 

Serikali ya Zanzibar ilitoa stempu mwaka 1963 kuadhimisha historia ndefu ya uvumilivu wa kidini Zanzibar.
                          

Picha hizi za Stempu, kutoka kushoto kwenda kulia,
Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Kanisa Kuu la Kristo,
Msikiti wa Malindi, Msikiti wa Hujjatul Islam,
Hekalu la Kihindi.

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR