Saturday, November 1, 2014

masomo ya Sikuku ya Watakatifu Wote 01/11/2014

01
 November
 JUMAMOSI: Sikuku ya Watakatifu Wote. 2014.
SOMO  1. Ufu. 7:2-4, 9-14

Somo katika  kitabu cha ufunuo. 
 Mimi Yohane niliona Malaika mwingine, akipanda kutoka mawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale Malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na Bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.......

Somo katika kitabu cha Yohane wa kwanza. 
2. 1Yoh. 3:1-3
Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa; kama yeye alivyo Mtakatifu.


  INJILI.Mt. 21:33-43 
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Mathayo.

Yesu alipowaona Makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia;akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema, Heri walio Maskini wa Roho; Maana ufalme wa Mbinguni ni wao. Heri wenye Huzuni; maana hao watafarijika, Heri wenye upole, Maana hao watarithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa Mbinguni ni wao. Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; Kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

No comments:

Post a Comment

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR