Kibiolojia ni mamalia. Sehemu ya pekee mwilini ni mwiro ambao hali halisi ni pua la tembo lililorefuka na kufanya kazi pia kama mkono wake yaani kwa kutumia mwiro ndovu hushika vitu na kufanya utafiti kwa kugusagusa.
Pembe-jino zake zinatafutwa sana kama mapambo na biashara ya pembe za ndovu imeshakuwa hatari kabisa kwa ndovu wote kwa sababu wanawindwa mno. Hivyo kwa mapatano ya kimataifa biahsara ya pembe hizi imepigwa marufuku.
Kwa jumla kuna spishi tatu za Tembo ambao wanafanana lakini hawazai pamoja. Tembo-nyika ambao ni wakubwa kuliko wengine.
Tembo wa Asia ni wadogo kwa Tembo Nyika lakini anazoea wanadamu kwa hiyo katika nchi kama Uhindi au Uthai hutumiwa kama mnyama wa kazi akibeba mizigo au watu. Zamani spishi hii ilitumiwa hata vitani. Kwa mfano jemadari Hanibal wa Karthago alishambulia Dola la Roma kwa msaada wa Tembo wa kijeshi waliovuka milima ya Alpi.
Tembo-misitu, Tembo huyu asili yake ni Afrika lakini wataalamu wamethibitisha ni spishi tofauti. Hufikia kimo cha mita 2 tu anaishi hasa katika misitu ya Kongo.
Spishi za Afrika
- Loxodonta africana, Ndovu-nyika (African Bush Elephant)
- Loxodonta cyclotis, Ndovu-misitu (African Forest Elephant)
Spishi ya Asia
- Elephas maximus, Ndovu wa Asia (Asian Elephant)
- Tembo hula majani. Kwa chakula hiki ambacho ni kigumu hutegemea meno yao.
itaendelea
No comments:
Post a Comment