Tuesday, January 22, 2013

nembo ya mwaka wa imani





Nembo ya Mwaka wa Imani
Imeundwa kwa alama mbalimbali zinazobeba maana maalum.
A) Mashua: Hii ni ishara ya Kanisa linalosafiri.
B) Mlingoti: Huu ni Msalaba ambao juu yake kuna monogramu (chapa ya herufi zaidi ya moja zinazochanganyika pamoja, moja juu ya nyingine) IHS. Hizi ni herufi tatu za kwanza za Kigriki za jina la Yesu: I = Iota, H = eta, S = Sigma. Alama hizi zinatumika pia kuonyesha kifupisho cha jina la Yesu ambapo kwa kilatini zinatumika kusimama badala ya maneno: Iesus Hominum Salvator; yaani, Yesu Mwokozi wa Wanadamu.
C) Mduara: Nyuma ya monogramu ipo alama ya mduara ambao unaizunguka pia monogramu hiyo. Hii ni alama ya Jua ambayo inawakilisha Ekaristi Takatifu.
(Tafsiri ya maelezo, TEC, 2012)
Nembo ya Ofisi ya Vijana
Vijana wane walioshikana mikono wanasimamia vyama vya Kitume vinavyounda umoja wa Vijana. Katikati kuna alama ya kamba, chini ya neno Fidei. Kamba ni chombo cha kufunga vitu viwili au zaidi. Kamba inayoshikanisha vijana wote ni Imani. Neno Fidei ni neno la Kilatini lenye maana, “ya Imani”. Yaani, umoja huu unahusu imani.
Programu zote za Mwaka wa Imani zitakuwa na nembo hii. Pia, kauli mbiu ya mwaka huu, kwetu vijana, itakuwa pia sala, maneno ya mwinjili Luka,


“Bwana, utuongezee imani

Luka 17:5.
                                   2012—2013

Friday, January 18, 2013

Historia ya Ukristo


Historia ya Ukristo

Sanamu ya Yesu Kristo mkombozi ilijengwa Rio de Janeiro (Brazil) ni kubwa kuliko zote zilizopata kutengenezwa.
                                                  UKRISTO....
Ukristo ni Dini  inayomwamini Mungu  pekee kama alivyofunuliwa na Yesu Kristo ambaye ndiye mwanzilishi wake.
Dini hiyo, iliyotokana na ile ya Wayahudi, inayolenga kuenea kwa Binadamu  wote, na kwa sasa ni kuu kuliko zote duniani, ikiwa na wafuasi zaidi ya bilioni mbili.
Kitabu chake kitakatifu kinajulikana kama Bibilia. Ndani yake inategemea hasa Injili na vitabu vingine vya Agano jipya.
Asili
Chimbuko la Ukristo ni kuwepo kwa mtu aliyezaliwa takriban miaka 2000 iliyopita huko mashariki ya kati, katika kijiji cha Bethlehemu kilichopo hadi hivi leo kwenye mipaka ya Palestina, naye alikuwa akiitwa Yesu wa Nazareti au mwana wa Yosefu mchonga samani; mama yake akifahamika kwa jina la Bikira Maria.
Masiya Yesu
Ukristo ni matokeo ya utume wa Yesu, uliopokewa na waliomwamini kuwa ndiye Masiya, yaani Mpakwamafuta (Kristo kwa Kigiriki), mkombozi aliyetimiliza ahadi za Mungu kwa uzao wa Abrahamu.Utabiri wa kuja kwake ulianzia katika bustani ya Edeni pale Mungu alipomwambia mwanamke ."uzao wako utamponda kichwa" nyoka, yaani shetani.

HISTORIA YA UKRISTO 2


 HISTORIA YA UKRISTO

Musa, mwanamapinduzi aliyewakomboa watu wa Israeli kutoka utumwani Misri takribani miaka 1250 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, ndiye nabii wa kwanza kutabiri wazi ujio wa Masiya au Kristo (Kumbukumbu la Torati 18:15-22, hususan mstari 18: "Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zenu; na nitatia neno langu kinywani mwake na atasema nao yote niliyomwamuru."
Kuja kwake kulitimia katika Agano Jipya, ambalo ni ukamilifu wa yote yaliyotabiriwa katika Agano la Kale. Kwani Musa alitumwa kuanzisha Agano la Kale kama maandalizi ya Agano Jipya, akikabidhi mifumo mingi ya nje na ndani kwa watawala na waamuzi waliomfuatia watakaoshikilia Agano la kusubiri Masiya wakishirikiana na manabii na makuhani.
Yesu alizaliwa miaka kama 1800 baada ya Abrahamu. Vitabu vya Injili vinaeleza matukio na mafundisho ya Yesu ambayo ndiyo mwongozo wa imani hiyo. Maisha na kazi ya Yesu yameibua mambo mengi katika historia. Ndiyo sababu kalenda iliyoenea duniani huhesabu miaka kutoka ujio wake; huu ni mchango mmojawapo wa Ukristo.
Mafundisho ya msingi ya Yesu

Hotuba ya Mlimani na Carl Heinrich Bloch. Hotuba ya Mlimani inachukulika na Wakristo kuwa utimilifu wa Torati iliyotolewa na Musa katika Mlima Sinai.
Yesu alifanya ishara za kustaajabisha, au miujiza. Matokeo ni kwamba, watu wengi wakamwamini. Nikodemu, mshiriki mmojawapo wa baraza la Sanhedrini, ambayo ilikuwa pia mahakama kuu ya Kiyahudi, alivutiwa na kutaka kujua zaidi kuhusu siri ya miujiza hiyo na ujumbe kutoka kwa Mungu; kwani yeye alihamasika kuona ishara zile kutoka kwa Mungu. Yesu akamjibu kwamba hakika mtu hawezi kuingia ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili kwa maji na Roho. Pia akajieleza kuwa mpatanishi wa ulimwengu wa dhambi na Mungu na kwamba
kila anayemgeukia kwa imani hatapotea, bali atarithi uzima wa milele: Kristo ni mfano wa nyoka wa shaba aliyetengenezwa na Musa. (Yohana 2:23-3:21; Hesabu 21:9).
Akiwa akitembea kando ya Ziwa la Galilaya, Yesu alikuta umati wa watu umekusanyika. Basi akapanda mashua na kuenda mbali kidogo na ufuoni, akaanza kuwafundisha kuhusu Ufalme wa Mbingu kupitia mfululizo wa mifano. Mmojawapo ni hili lifuatalo: Ufalme wa Mbingu ni kama punje ya haradali ambayo mtu anaipanda. Ingawa ni mbegu ndogo sana inakua na kuwa mti wa mboga kubwa kuliko yote. Inakua mti ambao ndege wanauendea, wakipata makao katika matawi yake. (Mathayo 13:1-52; Marko 4:1-34; Luka 8:4-18; Zaburi 78:2; Isaya 6:9,10).

HISTORIA YA UKRISTO 3


Maana ya Kristo
Mtume Paulo anazungumza hivi kuhusu Kristo:
Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaotawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri; ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ambayo wenye kutawala dunia hii hawaijui hata moja; maana kama wangalijua, wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu; Lakini, kama ilivyo andikwa:
Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho, maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuaye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua yaliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamnu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu, Maana,
Ni nani aliyefahamu nia ya Bwana, amwelimishe?
Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. (1 Wakorintho 2:6-16).
Kanisa siku za mwanzo
Jumuia ya Wakristo inaitwa Kanisa, lililotajwa na Yesu katika Mathayo 16:18:-
Wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu, nitalijenga kanisa langu. Wala milango ya kuzimu haitalishinda.

Ujio wa
Roho Mtakatifu

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR