Wednesday, August 27, 2014

Ziara ya Uinjilishaji JImbo la Mbulusehemu ya Promo www viwawaboko blogs...

Nembo ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016

Heri wenye rehema maana hao watapata rehema, ndiyo kauli mbiu itakayoongoza maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016 itakayofanyika Jimbo kuu la Cracovia, Poland. Kamati kuu ya maandalizi imechapisha nembo itakayotumika kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani ambayo Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuhudhuria na kushiriki kikamilifu.

Nembo ina rangi kuu tatu: Bluu, Nyekundu na Njano; inaonesha ramani ya Poland na ndani yake kuna Msalaba inayomwonesha Yesu Kristo, kiini cha mkutano huu. Nembo hii inawaalika vijana kujiaminisha mikononi mwa Mungu, utekelezaji wa maneno ya Mtakatifu Faustina Kowalska aliyeeneza Ibada ya Huruma ya Mungu.

Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016 itaanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 26 hadi Julai 2014. Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuwasili nchini Poland hapo tarehe 2
8 Julai 2016.

Kambumbu kuchezwa kwa ajili ya kueneza Ujumbe wa amani duniani

Septemba Mosi katika viwanja vya Olympic vya mjini Roma, kutafanyika mashindano ya mpira wa miguu kati ya timu mbili za kidini kwa heshima ya Papa Francisco, kwa ajili ya kutoa ujumbe wa nguvu wa amani duniani. Ni mpango uliowasilishwa siku ya Jumanne kwa wanahabari katika ukumbi wa Makao Makuu ya Redio Vatican. Kati ya walio shiriki katika mkutano huo ni Msgr. Guillermo Karcher, afisa katika Sekretarieti ya Vatican kwa ajili ya khafla za Kipapa , mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu Javier Zanetti, wakiwepo pia wachezaji kutoka timu ya Lazio, Cristian Ledesma,na Juan Iturbe wa timu ya Roma.

Mchezo huu utakao fanyika katika uwanja wa Olympic Roma, Mosi Septemba 20:45, si mechi za kipinzani bali ni mchezo wa kirafiki kwa ajili ya kutoa ujumbe wa amani, na washiriki wa mechi hii wanatoka mataifa mbalimbali na watu wa imani mbalimbali . Sehemu ya mapato yake yatatengwa kwa ajili ya kufanikisha miradi ya Papa kwa ajili ya elimu na ustawi wa maisha kwa watu maskini mradi unaofanikishwa na kuendelezwa na taasisi ya "Scholas Occurentes" ambayo ni taasisi ya elimu, mkono wa Papa Francisko katika utoaji wa misaada na chama cha "Pupi" kilicho anzishwa na aliyekuwa Argentina mchezaji wa mpira wa miguu Javier Zanetti na mke wake Paula, kwa ajili udumishaji juhudi za kutoa msaada katika mradi unaoitwa "maisha mbadala". Kwa ajili hii, pia unaalikwa kutoa msaada wako katika juhudi hizi kwa kutuma ujumbe wa SMS namba 45593.

Katika mkutano wa waandishi wa habari, Msgr. Guillermo Javier Karcher, aliwasilisha rasmi salaam za Papa Francisko, ambamo alitoa shukurani zake za dhati kwa mpango huo uliandaliwa kwa ajili ya amani, kama alivyowahi kupendekeza siku za nyuma, uwepo wa mechi ya kirafiki kati ya wachezaji kutoka kila timu na wa dini zote na madhehebu yote Kikristo.Taasisi ya “Scholas Ocurrentes”, ililichukua kwa makini pendekezo hilo na kuandaa mechi hii na pia ina lenga kujenga mtandao kwa ajili ya kubadilishana miradi na maadili elimu kwa ajili ya kuendeleza utamaduni wa mijadala na utamaduni wa amani. Katika mtazamo huo, Papa Francisko alipendekeza kwamba kabla ya kila mchezo, kila timu ipande mti wa mzeituni, kama ishara ya amani , kama ilivyo fanyika katika maadhimisho ya mwaka Mtakatifu 2000, yeye akiwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires, alipanda mti katika uwanja wa Plaza de Mayo , akiwa na wanafunzi elfu saba kutoka shule za Kiserikali bila ya utengano wa kidini.
Waandaaji wa tukio hili wanatumaini, mchezo huu wa kwanza wa madhehebu,utaweza kuwa hatua ya mwanzo katika juhudi za kueneza ujumbe wa amani kwa njia ya michezo, kama Papa Francisco alivyo pendekeza. Michezo pamoja na kuwa ni uwanja wa upinzani kati ya timu mbili zinazocheza, lakini ni tukio ambalo daima hufanyika katika hali ya amani na utulivu, kuburudisha na kufurahisha mioyo ya watu. Na hivyo unakuwa ni mfano mzuri wa kuigwa na vyama vya kisiasa , kwamba licha ya kuwa na maoni tofauti katika utendaji lakini katika utofauti huo, unakuwa ni nafasi ya kujenga mazuri kwa ajili ya ustawi wa jamii. Na kuwa mchezaji wa mpira au mwana riadha hakumwondolei mtu imani yake. Imani ni suala linalo ambatana na mtu katika maisha yake yote. Na ndivyo licha ya watu kuwa na imani mbalimbali, wanapaswa kuchanganyika na kucheza pamoja kwa amani na utulivu kama ilivyo timu za mpira katika mechi, hucheza kwa ajili ya manufaa ya wote.


Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya 21 ya Kipindi cha Mwaka A wa Kanisa

Mwamini mwana wa Mungu unayetegea sikio Radio Vatican, Tumsifu Yesu Kristo. Tunakuleteni tafakari ya Neno la Mungu Dominika ya 21 mwaka A tukiongozwa na Nabii Isaya, Mtume Paulo na Mwinjili Matayo, ambao wanatuambia kuwa imani thabiti katika Yesu Kristo Mwana wa Mungu ni msingi wa wokovu wetu. RealAudioMP3

Nabii Isaya katika somo la kwanza anatoa mafundisho yake wakati wa utawala wa Hezekia, yaani wakati wa utawala huu aliyekuwa mtunza mfuko anatumia vibaya mali aliyokabidhiwa yaani hajali shida za watu. Anajitazama yeye binafsi, anajiimarisha katika utajiri binafsi na anakuza jina lake.

Ni kwa shida hii Nabii Isaya anafundisha kinyume na madhulumu yanayofanywa na wenye madaraka. Anawaambia kuwa watanyanganywa funguo na watakabidhiwa wengine wenye kushika sheria ya Bwana. Funguo ni alama ya madaraka, ni alama ya utawala na hivi nabii anawaambia kuwa madaraka yenu yatapokonywa na Mungu. Mpendwa msikilizaji, ndiyo kusema hivi leo kuna wenye mamlaka wengi ambao wamejiimarisha katika mali, katika ubaya, kiasi kwamba wanapopita mitaani petu wanajionesha katika sura hiyo! Wanatoa harufu ya dhuluma.

Nabii anawaonya kuacha mali hizo na kumrudia Bwana. Hata hivyo tukumbuke kuwa Mungu hachukizwi na mali bali na tunaweza kuwa na mali na madaraka halali kama vitu hivi vinatupatia nafasi ya kuwaongoza wengine vema tukiwajalia haki na ustawi wa maisha yao.

Mtume Paulo anatualika kutambua mara na kuacha ubaya tukiongozwa na hekima ya Mungu ambayo inapita ufahamu wa kibinadamu. Kwa jinsi hiyo hatuna budi kuitafuta na kuipokea hekima ya Mungu ili itusaidie katika kutawala taifa la Mungu na mali tulizokabidhiwa na Mungu mwenyewe. Mtakatifu Paulo anazidi kutuambia jinsi hekima ya Mungu ilivyo ya ajabu ya kwamba katika ubaya wa Wayahudi yaani wanapomkataa Masiha, mara moja milango inafunguka kwa ajili ya mataifa ndiyo sisi! Hakika hekima yake haichunguziki, hatuna uwezo wa kuielewa vema kumbe yafaa kusadiki na kujiweka katika maongozi ya Mungu. Ndiyo kusema katika udhaifu wetu Mungu aweza kuibua jambo la ajabu kwa ajili ya wokovu wetu.

Mwinjili Mathayo anatuletea Kristu aliye katika harakati za uchungaji, yuko Kaisaria Filipi, yuko katika kutekeleza utume wake uliomleta duniani. Huko anataka kuhakiki kama watu na mitume wanamfahamu kina au bado. Anaweka swali mbele ya mitume, Je watu wasema mimi ni nani? Na ninyi mwasema mimi ni nani? Jibu toka jumuiya ya watu ni kwamba Yesu ni mmojawapo wa manabii, ni Ni nabii Eliya, ni Yohane Mbatizaji na mwishoni jibu la Mitume linatolewa na Mtakatifu Petro akisema “wewe ndiye Kristo, mwana wa Mungu aliye hai” Jibu hili la Mtakatifu Petro ndilo linabeba kiini cha injili, ni ufunuo wa Masiya mpakwa mafuta wa Bwana.

Kwa njia ya jibu hili mwinjili Mathayo anataka watu wote wamjue Kristo kama masiya na hakuna tena mfalme mwingine zaidi yake. Watu walitoa jibu kuwa ni nabii lakini sasa mwinjili anatuambia wakati wa manabii umekwisha na hivi ni Kristo pekee mwana wa Mungu aliye hai. Mpendwa hivi leo ukiulizwa Yesu ni nani utasema nini? Kwangu mimi Kristu ni mkombozi wa maisha yangu anayenipenda katika udhaifu wangu, anayeniita kila siku kutubu na kumrudia yeye kwa njia ya kitubio. Ni yule anayewapenda wote bila ubaguzi maskini kwa matajiri.

Tupige hatua kidogo mbele katika tafakari yetu tuone je jibu la Mt Petro linaishia pale tu au lina matunda? Jibu la Mtakatifu Petro lina matokeo makubwa mno, Mtakatifu Petro atakuwa mwamba ambapo Kanisa la Kristu litajengwa. Na si mwamba tu bali ni mwamba wa kujengea, ni mwamba wa imani. Makatifut Petro amekiri imani ambayo lazima ikue na izae matunda. Mwamba huu ni imara na hivi hata nguvu za kuzimu haziwezi kuubomoa. Anakabidhiwa funguo ambazo tulisikia Nabii Isaya akizungumzia kwamba mtunza hazina atanyanganywa na Bwana. Tunarudia tena kusema kuwa funguo ni alama ya madaraka, uwezo juu ya taifa la Mungu.

Oneni mpendwa, ni mamlaka gani Mtakatifu Petro amepewa ili ailinde imani! Asimamie Kanisa, afundishe, aonye na zaidi aimarishe imani ya waamini wote wa taifa la Mungu. Leo hii wajibu huu anao Baba Mtakatifu, Khalifa wa Mtakatifu Petro, Askofu wa Roma na mchungaji mkuu wa Kanisa lote la ulimwengu. Tunao wajibu wa kumwombea ili imani yake ibaki imara na abaki katika kuhudumu na kusimamia taifa takatifu la Mungu akijiimarisha katika imani na umisionari. Tumsifu Yesu Kristo. Tafakari hii imeletwa kwako na Padre Richard Tiganya C.PP.

Wednesday, August 20, 2014

PAPA FRANCIS AMRUHUSU PADRI WA JIMBO LA MOSHI KUOA


KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekubali kumuondolea sakramenti ya upadri, Padri Raymond Mosha wa Jimbo Katoliki la Moshi ikiwa ni miaka 20 tangu padri huyo aombe kujiondoa kwenye daraja hilo.

Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa Jumapili ya juzi katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi wakati wa ibada za Jumapili zilifanyika katika makanisa ya jimbo hilo.

Miongoni mwa parokia ambazo barua hiyo ilisomwa ni Parokia ya Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika ibada zote. Uamuzi huo ambao ni nadra sana kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa sasa hivi padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na familia kama Wakristo wengine.

Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha, ana mke na watoto watatu ambao kwa sasa wako vyuo vikuu.

Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka 1994 kabla ya uamuzi kutolewa juzi.

Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la Padri Mosha linaonekana likiwa ni namba 23.

Akizungumzia hatua hiyo, Padri Mosha alisema: “Ninafurahi kufunguliwa kifugo hiki na hii itanifanya niishi kama Mkristo. Kwa vile hawajaniondolea sifa ya kutoa huduma kama vile ibada za mazishi, sakramenti ya mwisho na ubatizo, nitaendelea kutoa kwa wahitaji kwa sababu ninaupenda ukristo.

“Nashukuru sasa nimekuwa muumini wa kawaida nitaweza kufunga ndoa kanisani kwa kuwa nilikuwa nimefunga ndoa ya kisheria tu kwa DC.”

Kuhusu kwa nini aliamua kuacha upadri, Profesa Mosha alisema ni baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 20 na akaona ipo haja ya kuwa na familia lakini kanisa lilikuwa haliruhusu.

“Sasa kwa kuwa kanisa haliruhusu mapadri kuoa ndiyo maana nikaamua kuandika barua ambayo hata hivyo, imechukua muda mrefu kujibiwa na tayari nina watoto watatu wako chuo kikuu."

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR