Baba
Mtakatifu Francisko, amepeleka salaam zake za rambirambi kwa familia za
Masista watatu wanashirika la Mtakatifu Xavery, waliouawa katika
nyumba yao ya Kamenge, Kaskazini mwa mji wa Bujumbura siku ya Jumapili.
Majina ya Marehemu Masista ni Sista Olga Raschietti, Sista Luchia
Pulici na Sr Bernadetta Boggian. Wote wanatajwa kuwa raia wa Italia.
Rambirambi
za Papa zimetumwa kwa Mjumbe wake wa Kitume nchini Burundi, Askofu
Mkuu Evariste Ngoyagoye na nyingine kwa Mama Mkuu wa Shirika la
Masista wa Mtakatifu Xavery, akionyesha kusikitishwa sana na
kilichotokea kwa Masista hao. Papa anatumaini damu hii ya watu wa Mungu
iliyomwangika bure, itaweza kuwa mbegu ya matumaini katika ujenzi wa
udugu wa kweli kati ya jamii ya watu wa Burundi. Na ameahidi
kuwakumbuka katika sala zake mashahidi hawa wa Injili , na ukaribu wake
kwa shirika, na jumuiya ya waamini nchini Burundi.
Mkuu wa
Shirika la Watawa Xaverian nchini Burundi, Padre Mario Pulcini,
akithibitisha uwepo wa tukio, ameonyesha hisia kwamba ni tukio la wizi.
Na kwamba, Sista Lucia na Sista Olga, waliuawa Jumapili mchana wakati
Sista Bernadetta, alikwenda kupokea Masista wengine waliowasili katika
uwanja wa ndege tokea Italia.
Wakati aliporejea nyumbani
alikutana na hali ya ukimya uliompa wasiwasi na baadaye akiwa na Padre
Mario waliona wenzao tayari walikuwa wameuawa ndani ya nyumba yao. Na
Sista Bernadetta ameuawa usiku wa kuamkia Jumatatu akiwa katika chumba
chake.
Askofu Henry, Jimbo la Parma Italia, kwa niaba ya Kanisa
lote la Parma, amepeleka pia niaba ya waamini wa Parma , salaam zake za
rambirambi kwa Usharika wa Missionari Xaverians, wakiwafariji kwa sala
ya imani kwa Bwana wa Maisha. Askofu pia ametoa ombi kwa Wakristo wa
Jimbo la Parma na kwa wote wenye mapenzi mema, kuwakumbuka Masista hawa
katika sala zao.
Tuesday, September 9, 2014
Thursday, August 28, 2014
Wednesday, August 27, 2014
Nembo ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016
Heri
wenye rehema maana hao watapata rehema, ndiyo kauli mbiu itakayoongoza
maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016 itakayofanyika
Jimbo kuu la Cracovia, Poland. Kamati kuu ya maandalizi imechapisha
nembo itakayotumika kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani
ambayo Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuhudhuria na kushiriki
kikamilifu.
Nembo ina rangi kuu tatu: Bluu, Nyekundu na Njano; inaonesha ramani ya Poland na ndani yake kuna Msalaba inayomwonesha Yesu Kristo, kiini cha mkutano huu. Nembo hii inawaalika vijana kujiaminisha mikononi mwa Mungu, utekelezaji wa maneno ya Mtakatifu Faustina Kowalska aliyeeneza Ibada ya Huruma ya Mungu.
Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016 itaanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 26 hadi Julai 2014. Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuwasili nchini Poland hapo tarehe 28 Julai 2016.
Nembo ina rangi kuu tatu: Bluu, Nyekundu na Njano; inaonesha ramani ya Poland na ndani yake kuna Msalaba inayomwonesha Yesu Kristo, kiini cha mkutano huu. Nembo hii inawaalika vijana kujiaminisha mikononi mwa Mungu, utekelezaji wa maneno ya Mtakatifu Faustina Kowalska aliyeeneza Ibada ya Huruma ya Mungu.
Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016 itaanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 26 hadi Julai 2014. Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuwasili nchini Poland hapo tarehe 28 Julai 2016.
Kambumbu kuchezwa kwa ajili ya kueneza Ujumbe wa amani duniani
Septemba
Mosi katika viwanja vya Olympic vya mjini Roma, kutafanyika mashindano
ya mpira wa miguu kati ya timu mbili za kidini kwa heshima ya Papa
Francisco, kwa ajili ya kutoa ujumbe wa nguvu wa amani duniani. Ni
mpango uliowasilishwa siku ya Jumanne kwa wanahabari katika ukumbi wa
Makao Makuu ya Redio Vatican. Kati ya walio shiriki katika mkutano huo
ni Msgr. Guillermo Karcher, afisa katika Sekretarieti ya Vatican kwa
ajili ya khafla za Kipapa , mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu Javier
Zanetti, wakiwepo pia wachezaji kutoka timu ya Lazio, Cristian
Ledesma,na Juan Iturbe wa timu ya Roma.
Mchezo huu utakao
fanyika katika uwanja wa Olympic Roma, Mosi Septemba 20:45, si mechi
za kipinzani bali ni mchezo wa kirafiki kwa ajili ya kutoa ujumbe wa
amani, na washiriki wa mechi hii wanatoka mataifa mbalimbali na watu wa
imani mbalimbali . Sehemu ya mapato yake yatatengwa kwa ajili ya
kufanikisha miradi ya Papa kwa ajili ya elimu na ustawi wa maisha kwa
watu maskini mradi unaofanikishwa na kuendelezwa na taasisi ya
"Scholas Occurentes" ambayo ni taasisi ya elimu, mkono wa Papa
Francisko katika utoaji wa misaada na chama cha "Pupi" kilicho anzishwa
na aliyekuwa Argentina mchezaji wa mpira wa miguu Javier Zanetti na mke
wake Paula, kwa ajili udumishaji juhudi za kutoa msaada katika mradi
unaoitwa "maisha mbadala". Kwa ajili hii, pia unaalikwa kutoa msaada
wako katika juhudi hizi kwa kutuma ujumbe wa SMS namba 45593.
Katika
mkutano wa waandishi wa habari, Msgr. Guillermo Javier Karcher,
aliwasilisha rasmi salaam za Papa Francisko, ambamo alitoa shukurani
zake za dhati kwa mpango huo uliandaliwa kwa ajili ya amani, kama
alivyowahi kupendekeza siku za nyuma, uwepo wa mechi ya kirafiki kati ya
wachezaji kutoka kila timu na wa dini zote na madhehebu yote
Kikristo.Taasisi ya “Scholas Ocurrentes”, ililichukua kwa makini
pendekezo hilo na kuandaa mechi hii na pia ina lenga kujenga mtandao
kwa ajili ya kubadilishana miradi na maadili elimu kwa ajili ya
kuendeleza utamaduni wa mijadala na utamaduni wa amani. Katika mtazamo
huo, Papa Francisko alipendekeza kwamba kabla ya kila mchezo, kila timu
ipande mti wa mzeituni, kama ishara ya amani , kama ilivyo fanyika
katika maadhimisho ya mwaka Mtakatifu 2000, yeye akiwa Askofu Mkuu wa
Buenos Aires, alipanda mti katika uwanja wa Plaza de Mayo , akiwa na
wanafunzi elfu saba kutoka shule za Kiserikali bila ya utengano wa
kidini.
Waandaaji wa tukio hili wanatumaini, mchezo huu wa kwanza
wa madhehebu,utaweza kuwa hatua ya mwanzo katika juhudi za kueneza
ujumbe wa amani kwa njia ya michezo, kama Papa Francisco alivyo
pendekeza. Michezo pamoja na kuwa ni uwanja wa upinzani kati ya timu
mbili zinazocheza, lakini ni tukio ambalo daima hufanyika katika hali ya
amani na utulivu, kuburudisha na kufurahisha mioyo ya watu. Na hivyo
unakuwa ni mfano mzuri wa kuigwa na vyama vya kisiasa , kwamba licha ya
kuwa na maoni tofauti katika utendaji lakini katika utofauti huo,
unakuwa ni nafasi ya kujenga mazuri kwa ajili ya ustawi wa jamii. Na
kuwa mchezaji wa mpira au mwana riadha hakumwondolei mtu imani yake.
Imani ni suala linalo ambatana na mtu katika maisha yake yote. Na
ndivyo licha ya watu kuwa na imani mbalimbali, wanapaswa kuchanganyika
na kucheza pamoja kwa amani na utulivu kama ilivyo timu za mpira katika
mechi, hucheza kwa ajili ya manufaa ya wote.
Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya 21 ya Kipindi cha Mwaka A wa Kanisa
Mwamini
mwana wa Mungu unayetegea sikio Radio Vatican, Tumsifu Yesu Kristo.
Tunakuleteni tafakari ya Neno la Mungu Dominika ya 21 mwaka A
tukiongozwa na Nabii Isaya, Mtume Paulo na Mwinjili Matayo, ambao
wanatuambia kuwa imani thabiti katika Yesu Kristo Mwana wa Mungu ni
msingi wa wokovu wetu.
Nabii
Isaya katika somo la kwanza anatoa mafundisho yake wakati wa utawala wa
Hezekia, yaani wakati wa utawala huu aliyekuwa mtunza mfuko anatumia
vibaya mali aliyokabidhiwa yaani hajali shida za watu. Anajitazama yeye
binafsi, anajiimarisha katika utajiri binafsi na anakuza jina lake.
Ni
kwa shida hii Nabii Isaya anafundisha kinyume na madhulumu yanayofanywa
na wenye madaraka. Anawaambia kuwa watanyanganywa funguo na
watakabidhiwa wengine wenye kushika sheria ya Bwana. Funguo ni alama ya
madaraka, ni alama ya utawala na hivi nabii anawaambia kuwa madaraka
yenu yatapokonywa na Mungu. Mpendwa msikilizaji, ndiyo kusema hivi leo
kuna wenye mamlaka wengi ambao wamejiimarisha katika mali, katika ubaya,
kiasi kwamba wanapopita mitaani petu wanajionesha katika sura hiyo!
Wanatoa harufu ya dhuluma.
Nabii anawaonya kuacha mali hizo na
kumrudia Bwana. Hata hivyo tukumbuke kuwa Mungu hachukizwi na mali bali
na tunaweza kuwa na mali na madaraka halali kama vitu hivi vinatupatia
nafasi ya kuwaongoza wengine vema tukiwajalia haki na ustawi wa maisha
yao.
Mtume Paulo anatualika kutambua mara na kuacha ubaya
tukiongozwa na hekima ya Mungu ambayo inapita ufahamu wa kibinadamu. Kwa
jinsi hiyo hatuna budi kuitafuta na kuipokea hekima ya Mungu ili
itusaidie katika kutawala taifa la Mungu na mali tulizokabidhiwa na
Mungu mwenyewe. Mtakatifu Paulo anazidi kutuambia jinsi hekima ya Mungu
ilivyo ya ajabu ya kwamba katika ubaya wa Wayahudi yaani wanapomkataa
Masiha, mara moja milango inafunguka kwa ajili ya mataifa ndiyo sisi!
Hakika hekima yake haichunguziki, hatuna uwezo wa kuielewa vema kumbe
yafaa kusadiki na kujiweka katika maongozi ya Mungu. Ndiyo kusema katika
udhaifu wetu Mungu aweza kuibua jambo la ajabu kwa ajili ya wokovu
wetu.
Mwinjili Mathayo anatuletea Kristu aliye katika harakati za
uchungaji, yuko Kaisaria Filipi, yuko katika kutekeleza utume wake
uliomleta duniani. Huko anataka kuhakiki kama watu na mitume wanamfahamu
kina au bado. Anaweka swali mbele ya mitume, Je watu wasema mimi ni
nani? Na ninyi mwasema mimi ni nani? Jibu toka jumuiya ya watu ni kwamba
Yesu ni mmojawapo wa manabii, ni Ni nabii Eliya, ni Yohane Mbatizaji na
mwishoni jibu la Mitume linatolewa na Mtakatifu Petro akisema “wewe
ndiye Kristo, mwana wa Mungu aliye hai” Jibu hili la Mtakatifu Petro
ndilo linabeba kiini cha injili, ni ufunuo wa Masiya mpakwa mafuta wa
Bwana.
Kwa njia ya jibu hili mwinjili Mathayo anataka watu wote
wamjue Kristo kama masiya na hakuna tena mfalme mwingine zaidi yake.
Watu walitoa jibu kuwa ni nabii lakini sasa mwinjili anatuambia wakati
wa manabii umekwisha na hivi ni Kristo pekee mwana wa Mungu aliye hai.
Mpendwa hivi leo ukiulizwa Yesu ni nani utasema nini? Kwangu mimi Kristu
ni mkombozi wa maisha yangu anayenipenda katika udhaifu wangu,
anayeniita kila siku kutubu na kumrudia yeye kwa njia ya kitubio. Ni
yule anayewapenda wote bila ubaguzi maskini kwa matajiri.
Tupige
hatua kidogo mbele katika tafakari yetu tuone je jibu la Mt Petro
linaishia pale tu au lina matunda? Jibu la Mtakatifu Petro lina matokeo
makubwa mno, Mtakatifu Petro atakuwa mwamba ambapo Kanisa la Kristu
litajengwa. Na si mwamba tu bali ni mwamba wa kujengea, ni mwamba wa
imani. Makatifut Petro amekiri imani ambayo lazima ikue na izae matunda.
Mwamba huu ni imara na hivi hata nguvu za kuzimu haziwezi kuubomoa.
Anakabidhiwa funguo ambazo tulisikia Nabii Isaya akizungumzia kwamba
mtunza hazina atanyanganywa na Bwana. Tunarudia tena kusema kuwa funguo
ni alama ya madaraka, uwezo juu ya taifa la Mungu.
Oneni
mpendwa, ni mamlaka gani Mtakatifu Petro amepewa ili ailinde imani!
Asimamie Kanisa, afundishe, aonye na zaidi aimarishe imani ya waamini
wote wa taifa la Mungu. Leo hii wajibu huu anao Baba Mtakatifu, Khalifa
wa Mtakatifu Petro, Askofu wa Roma na mchungaji mkuu wa Kanisa lote la
ulimwengu. Tunao wajibu wa kumwombea ili imani yake ibaki imara na abaki
katika kuhudumu na kusimamia taifa takatifu la Mungu akijiimarisha
katika imani na umisionari. Tumsifu Yesu Kristo. Tafakari hii imeletwa
kwako na Padre Richard Tiganya C.PP.
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...