Monday, September 16, 2013

FUATILIA DEKANIA CUP HAPA......

Tamasha la Mchezo la Dekania ya Mt. Gasper Del Bufalo - Mbezi Beach, lilifunguliwa jana rasmi, katika viwanja wa Parokia ya Mt. Gasper Mbezi Machakani, akifungua mashindano hayo Paroko wa Parokia ya Gasper ambaye pia ni Mlezi wa Vijana Dekania Padre Kimaro aliwahasa Vijana kufanya michezo iwe sehemu ya burudani, kujenga upendo na kupata marafiki wapya, ili kuzidi kuitanga injili kwa watu wengi zaidi.

Dekania ya Mt. Gasper ina jumla ya Parokia kumi, lakini katika mashindano haya Parokia zinazoshiriki ni saba, na kuna Michezo mitatu, Mpira wa Miguu, Pete na Wavu.

Mashindano haya yanatarajia kufika kikomo siku ya somo wa Dekania yetu tarehe 20/10/2013.

Matokeo ya Mechi za jana
Mpira wa Miguu   St. Gasper 2  St. Dominiko 0
Mpira wa Pete St. Gasper 24 St. Dominiko 4

ratiba full itakuwepo hapa na msimamo siku si nying

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR