Adui
mkubwa wa mchakato wa majadiliano ya kidini ni woga na wasiwasi
usiokuwa na msingi, mambo yanayochangia watu wa dini mbali mbali
kushindwa kufahamiana na hatimaye kuishi kwa amani, umoja na udugu kwa
kutambua kwamba, wote wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na hivyo
tofauti zao za kidini si sababu msingi ya malumbano na kinzani zisizo na
tija wala mashiko kwa watu.
Katika mchakato wa majadiliano ya
kidini, Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuhimiza umuhimu wa waamini
wa dini mbali mbali kufahamiana. Hii ni kati ya changamoto zilizotolewa
na Padre Miguel Angel Ayuso Guixot, Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la
majadiliano ya kidini pamoja na ujumbe wake walipokuwa wanatembelea na
kukutana na viongozi mbali mbali wa kidini nchini Indonesia, ambako kuna
idadi kubwa ya waamini wa dini ya Kiislam.
Ujumbe wa Baraza la
Kipapa la majadiliano ya kidini, umekumbushia kwamba, majadiliano ya
kidini na waamini wa dini mbali mbali ni sehemu ya vinasaba vya Kanisa
Katoliki ili kujenga na kudumisha amani, upendo na mshikamano kati ya
watu na wala si kwa bahati mbaya kwamba, Kanisa katika mikakati na
vipaumbele vyake katika mchakato wa Uinjilishaji linaendelea kukazia
majadiliano ya kidini na waamini wa dini mbali mbali duniani. Waamini
wanaweza kujenga na kudumisha umoja, udugu na urafiki kwa kusaidiana
katika hija ya maisha yao hapa duniani.
Ujumbe wa Vatican nchini
Indonesia umepokelewa kwa heshima na taadhima, huo ni ukarimu
unaooneshwa na waamini wa dini ya Kiislam wanaoishi huko Indonesia
katika ujumla wao. Majadiliano ya kidini kati ya Waislam na Wakristo
nchini Indonesia yamejikita katika mang'amuzi na maisha ya kila siku,
tofauti kabisa na hali inavyooneshwa na vyombo vya upashanaji habari.
Ujumbe wa Vatican umepata nafasi ya kushuhudia na kubadilishana uzoefu
na mang'amuzi katika mchakato wa majadiliano ya kidini, ili kujenga na
kudumisha misingi ya haki, amani na udugu kati ya watu.
Waamini
wa dini ya Kiislam wanaofanya kazi katika taasisi za Kanisa Katoliki
wanasema, wanaendelea kufurahia huduma yao na kwamba, wanajisikia wako
nyumbani na wala hawajawahi kutengwa wala kunyanyaswa kwa misingi ya
kidini. Kila mtu anaheshimiwa kama binadamu na kwamba, tofauti zao za
kiimani ni utajiri mkubwa unaoweza kutumika kwa ajili ya kudumisha
amani, upendo na mshikamano wa kidugu.
Wednesday, October 8, 2014
Mkesha wa sala kuombea Sinodi Maalum ya Maaskofu
Jumamosi
majira ya saa moja za jioni, makumi ya maelfu ya watu wajumuika
katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , kwa ajili ya mkesha wa
sala, ulio ongozwa na Baba Mtakatifu Francisko, kuombea Sinodi Maalum
ya Maaskofu, ambayo imefunguliwa Jumapili hii kwa Ibada ya Misa katika
Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican. Sinodi hii maalum inachambua
changamoto cha Kichungaji katika familia, kwenye muono wa Uinjilishaji .
Katika
Mkesha huu wa sala, Baba Mtakatifu Francisko,alitoa wito kwa Waamini
wawaombee Mababa wa Sinodi , kwa namna ya pekee, zawadi ya kuisikiliza
sauti ya Mungu inavyo waambia na kuwa na moyo wa uwazi katika
majadiliano na kukaza macho yao kwa Yesu Kristo.
Kabla ya sala
ya Mkesha, kulikuwa na utaratibu wa kusikiliza Neno la Mungu ,
Maandiko Matakatifu, ushuhuda wa wanandoa, maombi, kuimba na tafakari
juu ya maandishi ya Papa Francisco na watangulizi wake.
Baba
Mtakatifu alisema, ushirikiano katika maisha ya ndoa, uwazi kwa zawadi
ya maisha, kulindana, kuheshimiana, kukutana na kumbukumbu ya vizazi
vilivyopita, msaada wa elimu, maambukizi ya imani ya Kikristo kwa
watoto wao. . .pamoja na mengine, kwa yote hayo , familia inaendelea
kuwa shule iliyosimikwa katika ubinadamu , na mchango muhimu katika
haki na umoja katika jamii. (Cf. ibid., N. Evangelii gaudium, 66-68).
Na
kwa kadri familia inavyozamisha mzizi wake katika kina kirefu cha
umoja wa familia , ndivyo inavyo wezekana maisha hayo kuzama zaidi
ndani yake bila kupoteza hisia zake katika mambo mageni. Kwa upeo huo,
inatusaidia kufahamu umuhimu wa mkutano huu wa Sinodi Maalum ya
Maaskofu, inayofunguliwa kesho.
Zaidi ya yote, Papa alisema,
tunaomba Roho Mtakatifu awape Mababa wa Sinodi, zawadi ya kusikiliza,
kusikiliza kwa namna ya Kimungu, ili wapate kusikia, pamoja naye, kilio
cha watu; kusikiliza kilio cha watu hadi waweze kupumua mapenzi Mungu.
Papa aliomba ili kwamba, Maaskofu waweze kupata zawadi ya
kusikiliza kwa makini na uwazi katika majadiliano ya kweli, uwazi wa
kidugu, wenye kuwawezesha kulibeba jukumu la Kichungaji, na uwajibikaji
kwenye hoja za mabadiliko, yanayojitokeza katika nyakati hizi.
Papa
alieleza katika hatua hiyo ya kusikiliza na majadiliano juu ya
familia, wakiwa pamoja na Kristo, inakuwa ni tukio la Kikudra ambamo
wanaweza kufanya upya utendaji kwa mfano wa Mtakatifu Francisco, kwa
Kanisa na jamii.
Pamoja na furaha ya Injili, aliendelea kusema,
tutaweza kugundua njia ya mapatano, na huruma ya kanisa katika kuwaona
maskini na rafiki wa maskini, kwa nguvu ya kanisa inawezekana, kukua
katika uvumilivu na upendo, na kuondokana na hofu na changamoto zake,
katika yote, ndani ya kanisa lenyewe na nje yake (Lumen Gentium, 8).
Papa
alikamilisha kwa kuomba uvuvio wa Roho Mtakatifu, uvume juu ya kazi za
Sinodi na Juu ya Kanisa na juu ya Ubinadamu wote. Uweze kufungua
vifundo vyote vinavyozuia watu kukutana mmoja kwa mwingine, kuponya
majeraha yanayovuja damu , na kufufua matumaini. Bwana na atupatie
mbinu hizi za upendo kama Yesu alivyopenda. Na ili ujumbe wetu uweze
kuleta uhai na shauku ya Wamisionari wa kwanza wa Injili.
Washiriki
wa sinodi hii, wametoka bara zote tano za dunia kuzungumzia changamoto
za Kichungaji kwa familia, katika muono wa Uinjilishaji, ni kama
ifuatavyo: Kuna Marais wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki 114, Wakuu wa
Makanisa ya Katoliki ya Mashariki 13, Wakuu wa Idara za Curia ya Roma
25, Wajumbe 9 kutoka Sekretariati ya Baraza la kawaida wa Sekretarieti,
Katibu Mkuu wa Jimbo la Papa, na katibu mwandamizi, Wajumbe 3 kutoka 3
wanaowakilisha Wakuu wa Mashirika, na wajumbe 26 walioteuliwa na Papa.
Washiriki wengine ni pamoja na 8 Mabruda wanane, Wajumbe 38 wakiwa ni
wakaguzi, wakimwemo wanandoa 13 wanandoa, na 16 wataalam. Jumla ya idadi
ya washiriki wote wa Sinodi ni 253.Sinodi hii ni hatua ya kwanza kwa
ajili ya Sinodi ya kawaida ya mwaka kesho 2015, na hivyo itakamilika
bila kutoa tamko la mwisho juu yale yaliyojadiliwa, kwa kuwa maoni
yatakayotolewa yatafikishwa katika Sinodi ya Kawaida ya mwaka kesho
ambayo itatoa hati yenye tamko juu utendaji wa kanisa katika kupambana
na changamoto za Kichungaji katika familia.
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...