Saturday, April 27, 2013

Matangazo ya Dominika ya kesho Tarehe 28/04/2013

Mpendane. kama vile nilivyowapenda ninyi nanyi mpendane vivyo hivyo huu ni mwaliko tuupatao kutoka kwa kristo mwenyewe. neno upendo ni neno dogo au fupi kiherufi lakini linabeba maana nzito na kubwa sana hasa kwetu sisi tulio wafuasi wa kristo. na ambao tunafanya utume wa Vijana Wakatoli (askari kamili wa Yesu) Salamu yetu ni Mapendo.......Daima. swali ni je tunayaishi haya Mapendo tunayoyatamka.....tunakuwa wavumilivu kwa wengine, tunawapenda wengine kama sisi tunavypjipenda na tupo tayari kuteseka kwa ajili ya mwengine.

Tunaona ilikuwa siku ya alhamisi katika karamu ya mwisho Yesu kama mkubwa wa familia na yeye na mitume wake akichukua nafasi ya ukubwa wa familia; anatimiza wajibu wake wa kuwapa maneno machache mitume wake yawe kama mwongozo wa maisha yao. Yesu akijua wazi kuwa hiyo ndiyo karamu yake ya mwishona mitume wake,......ni kweli sisi kama wakubwa au viongozi wa ngazi fulani tuyatekeleza yale tulipewa kufanya......au sisi ndiyo chanzo cha kuyazima yale yenye nuru ya Mungu na kupandikiza ya kishetani.....

MATANGAZO YA JUMAPILI YA KESHO
KIGANGO CHA BOKO
IBADA YA KWANZA
 SAA 12:15-2:00 ASUBUHI
IBADA YA PILI
SAA 2:00-4:00 ASUBUHI
IBADA YA TATU
SAA 4:00-5:30 ASUBUHI
Viongozi wote wa VIWAWA ngazi ya Kanda Mkutane na Uongozi wa VIWAWA wa Kigango mara baada ya misa ya Pili.

KIGANGO CHA MT. RAPHAEL- MBWENI MALINDI
IBADA YA KWANZA
 SAA 1:00-3:00 ASUBUHI
IBADA YA PILI
SAA 3:00-5:00 ASUBUHI

KIGANGO CHAMBWENI
IBADA YA KWANZA
 SAA 1:15-3:00 ASUBUHI
IBADA YA PILI
SAA 3:00-5:00 ASUBUHI

KANDA YA MT. ANTONY WA PADUA
IBADA YA KWANZA
 SAA 3:15-5:00 ASUBUHI
UONGOZI WA VIWAWA PAROKIA UTAKUWEPO KWA AJILI YAKUTOA SEMINA JUU YA UTUME WA VIWAWA NA KUONA MAENDELEO YA VIJANA WA KANDA HIYO...FIKA NA UMWAMASISHE MWENZAKO.........

NAFASI ZA USHIRIKI WA ZIARA YA MBULU ZIMEBAKI CHACHE JITAHIDI UCHUKUE FORM MAPEMA......USIJE JUTIA NAFASI HII MWISHO WA KUREJESHA FORM NI TAREHE 29/05/2013.....TUNAWATAKIA MAANDALIZI MEMA

        ................................DOMINIKA NJEMA................................

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR