Eneo lake ni 14,763 km² na kijiografia inaendelea ndani ya Kenya inapoitwa Hifadhi ya Masai Mara.
Kuna idadi kubwa ya wanyamapori. Serengeti pamoja na Masai Mara inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aina nyingi nyingine za wanyama, kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, fisi, kifaru na nyati.
Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya zamadamu yalipatikana liko ndani ya Serengeti.
Mazingira ya Serengeti ni kanda ya kijiografia katika kaskazini-magharibi mwa Tanzania na inaenea kusini-magharibi mwa Kenya kati ya latitude 1 na 3 Kusini na longitude 34 na 36 Mashariki. Inaenea kiwango cha mraba kilometa 30,000 2.
Serengeti ina gura/uhamiaji ya wanyama kwenye ardhi kubwa na ndefu zaidi duniani, ambao hua ni tukio wa nusu mwaka . Uhamiaji huo ni moja ya maajabu kumi ya asili ya ulimwengu ya kusafiri.
Kanda hii ina hifadhi za taifa na hifadhi mchezo kadhaa. Jina Serengeti limechukuliwa kutoka lugha ya Kimasai hasa, "Serengit" kumaanisha "Kiwara kisichoisha".
Inakadiriwa mamalia 70 kubwa na baadhi ya spishi 500 avifauna (yaani ndege) hupatikana huko. Tofauti hii ya juu upande wa spishi ni shughuli makazi mbalimbali kuanzia misitu ya riverine, mabwawa, kopjes mbuga na misitu. Nyumbu bluu, swara, punda milia na nyati ni baadhi ya mamalia kubwa ambao kwa kawaida hupatikana katika kanda hii.
Karibu Oktoba, karibu wanyama wanaokula majani (si nyama) milioni 2 husafiri kutoka milima ya kaskazini kuelekea nyanda za kusini na kuvuka mto wa Mara katika harakati za mvua. Katika mwezi Aprili, wao hurejea kaskazini kwa kupitia magharibi, na kwa mara nyingine tena kuvuka Mto wa Mara. Jambo hili la mara kwa mara huitwa kwa Kiingereza "Circular migration" yaani uhamiaji mviringo. Nyumbu zaidi ya 250,000 pekee watakufa safarini kutoka Tanzania kwenda katika mbuga ya wanyama ya Masai Mara huko Kenya pande za juu, ambayo ni jumla ya maili 500. Kifo mara nyingi unasababishwa na maudhi au uchovu. Uhamiaji huu umeonyeshwa katika filamu na programu nyingi za televisheni kote duniani.