Showing posts with label Masomo ya Jumapili 8/6/2014 Dominika ya sherehe ya Pentekoste Mwaka A. Show all posts
Showing posts with label Masomo ya Jumapili 8/6/2014 Dominika ya sherehe ya Pentekoste Mwaka A. Show all posts

Thursday, June 5, 2014

Masomo ya Jumapili 8/6/2014 Dominika ya sherehe ya Pentekoste Mwaka A



08
   JUNI 
 SHEREHE YA PENTEKOSTE
 MWAKA "A" 2014


RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
IBADA YA MISA YA KWANZA 12:15 – 1:45 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 2:00 – 3:50 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA TATU SAA 4:00-5:20 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:15 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:00 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA – MBWENI MPIJI.
IBADA YA MISA NI 3:00 – 5:00ASUBUHI
Zaburi: Tazama sala ya siku
Zab: 104:1-24, 29-31,34
Ee Bwana, Nawe waufanya upya uso wa nchi.

SOMO LA 1: Mdo. 2:1-11

  Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. kakaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? Waparthi na wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapodokia, Ponto na Asia, Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu ba Kerene, na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu

SOMO 2:1Kor.12:3b-7, 12-13

   Hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yule yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. kisha pana tofauti za kutenda kazi bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. maana kama vile mwili mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi , ni mwili mmoj; vivyo hivyo na Kristo. kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

INJILI:Mt. 28:16-20

  Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana. Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawambia, pokeeni Roho Mtakatifu. Wo wote mtakaowaondolea dhambi wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.

 

 MATANGAZO

mara baada ya misa ya pili saa 4:00 asubuhi, Parokiani Boko, Tutakuwa na kikao cha VIjana waote wanaotarajia kushiriki ziara ya uinjilishaji Jimbo la Mbulu Parokia za Dareda, Sanu, Daudi na endabashi, pia kwenda kutembelea mbuga ya Wanyama ya ngorongoro.

Fika na mchango wako ikiwa bado haujamalizia mchango ni tshs 150,000 kwa mshiriki, ziara ni tarehe 01/07 mpaka tarehe 07/07/2014....

Tunawatikia Dominika njema, Amani ya Bwana Iwe nasi.........Mapendo sana,,,,,,, 

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR