Showing posts with label MASOMO YA DOMINIKA YA MWILI NA DAMU TAKATIFU YA YESU JUNE 22. Show all posts
Showing posts with label MASOMO YA DOMINIKA YA MWILI NA DAMU TAKATIFU YA YESU JUNE 22. Show all posts

Friday, June 20, 2014

JUMAPILI YA MWILI NA DAMU TAKATIFU YA BWANA WETU YESU KRISTU MASOMO MWAKA A



22
   JUNI 
 JUMAPILI YAMWILI NA DAMU TAKATIFU YA BWANA WETU YESU KRISTU
 MWAKA "A" 2014


RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
IBADA YA MISA YA KWANZA 12:15 – 1:45 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 2:00 – 3:50 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA TATU SAA 4:00-5:20 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:15 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:00 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA – MBWENI MPIJI.
IBADA YA MISA NI 3:00 – 5:00ASUBUHI



Zaburi: tazama sala ya siku
Zab:147:12-15. 19-20
K. Msifu Bwana, Ee Yerusalemu

SOMO 1:Kum.8:2-3, 14-16a
Musa aliwaambia makutano:
         Utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako, aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu, kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo. Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana. Usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana. Basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, uliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu, aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zao.

SOMO 2:1Kor. 10:16-17
Kikombe kile cha Baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.

INJILI: Yn.6:51-58
Yesu aliwaambia Wayahudi:
          Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sis mwili wake ili tuule? Basi Yesu akawaambia, Amin, Amin, nawaambieni, msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye  mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; name nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, name hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, name ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele.



 MATANGAZO

mara baada ya misa ya pili saa 4:00 asubuhi, Parokiani Boko, Tutakuwa na kikao cha VIjana waote wanaotarajia kushiriki ziara ya uinjilishaji Jimbo la Mbulu Parokia za Dareda, Sanu, Daudi na endabashi, pia kwenda kutembelea mbuga ya Wanyama ya ngorongoro.

Fika na mchango wako ikiwa bado haujamalizia mchango ni tshs 150,000 kwa mshiriki, ziara ni tarehe 01/07 mpaka tarehe 07/07/2014....

Tunawatikia Dominika njema, Amani ya Bwana Iwe nasi.........Mapendo sana,,,,,,, 

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR