Jumatatu, 22 Desemba 2014
Juma la 4 la Majilio
1 Sam 1: 24-28;
1 Sam 2: 1, 4-8;
Lk 1: 46-56
Msifu Mungu Muda Wote!
Wimbo wa Bikira Maria lazima ulinganishwa na wimbo wa sifa wa Hana (1 Sam 2:1-10) na Zakaria (Lk 1:68-79). Wakati sifa za kinabii za Maria zinasimama kwa njia mbalimbali, tofauti kubwa zaidi zipo katika hali zao. Hana alimsifu Bwana wakati akimtoa Samweli. Alikuwa katika haibu ya utasa (1Sam 1:7). Kuzaliwa kwa Samweli kulibadilisha hayo yote, na hivyo Hana alikuwa na sababu ya kumsifu Bwana. Vilevile, Zakaria alivumilia miaka mingi sana bila kuwa na mtoto na kuwa kiziwi na bubu kwa muda wa miezi tisa (Lk 1:20, 62). Sasa wakati mwanae wa kiume alipozaliwa, ulimi wake ulifunguka (Lk 1:64), na alikuwa na sababu ya kumsifu Bwana. Kinyume chake, Mwinjili Luka anaweka sifa za Maria mwanzo wa ujauzito wake. Maria alikuwa akimsifu Bwana sio tu baada ya mateso yake bali kabla na wakati wa mateso yake. Yeye hakusifu tu baadae bali alisifu popote pale. Alikuwa akisifu kwa imani na sio kwasababu aliona hali fulani iliyo nzuri. (2 Kor 5:7).
Sala: Tusaidie Maria, kumsifu Bwana daima kama ulivyomsifu wewe. Amina.
"Kwa upande wake, familia ya kikrlsto imepandildzwa katlka fumbo la Kanisa kwa kadiri hiyo hata kuwa mshiriki, kwa namna yake ya pekee katlka utume wa wokovu wa kanisa: Kwa nguvu ya Sakramenti, wakrlsto mume na mke na wazazl "katika hall na jinsi yao ya maisha wanayo karama ya pekee katika Taifa la Mungu". Kwa sababu hii hawapokei tu pendo la Kristo na kuwa jumuiya iliyookolewa, ball wanaitwa pia kuwashirikisha pendo la Kristo ndugu zao, na hivyo kuwa jumuiya yenye kuokoa. Kwa namna hii, pindi familia ya Kikristo ni tunda na ishara ya kuzaa kwa Kanisa kimungu, husimama pia kama mfano, ushuhuda na mshiriki wa umama wa Mungu(116)." – Baba Mtakatifu Yohani Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris Consortio (WAJIBU WA FAMILIA YA KIKRISTU KATIKA ULIMWENGU WA KISASA)- 49.
VIWAWABOKO
www.viwawaboko.blogspot.com
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...