Showing posts with label jinsi ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa 2015. Show all posts
Showing posts with label jinsi ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa 2015. Show all posts

Monday, October 12, 2015

JINSI YA KUPIGA KURA TAREHE 25/10/2015

 
1.  Mkabidhi Msimamizi wa kituo kadi yako ya Kupigia Kura,
2.  Jina lako litasomwa kwa sauti kubwa ili Mawakala wa Vyama vya Siasa waliopo kituoni wasikie,
3.  Wasimamizi wa vituo, na hata Mawakala wa vyama vya siasa wakiwa na shaka wana haki ya kukuuliza maswali ili wajidhihirishe,
4.  Msimamizi wa kituo atakukabidhi karatasi 3 za kura  – yaani ya( Rais, Mbunge na Diwani) na pia atakuonyesha jinsi ya          kukunja karatasi hizo,
5.  Utaenda sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya Kupiga Kura yako,
6.  Utaweka alama ‘V’ ndani ya chumba kilichopo chini ya Mgombea unayemtaka.
 7.  Utatumbukiza karatasi zako za Kura katika masanduku ya Kura kwa jinsi utakavyoelekezwa.
 8.  Kabla ya kuondoka ,utachovya kidole chako kidogo cha mkono wa kushoto katika Wino Maalum usiofutika kwa urahisi.
 
 

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR