Baba
Mtakatifu Francisko, amepeleka salaam zake za rambirambi kwa familia za
Masista watatu wanashirika la Mtakatifu Xavery, waliouawa katika
nyumba yao ya Kamenge, Kaskazini mwa mji wa Bujumbura siku ya Jumapili.
Majina ya Marehemu Masista ni Sista Olga Raschietti, Sista Luchia
Pulici na Sr Bernadetta Boggian. Wote wanatajwa kuwa raia wa Italia.
Rambirambi
za Papa zimetumwa kwa Mjumbe wake wa Kitume nchini Burundi, Askofu
Mkuu Evariste Ngoyagoye na nyingine kwa Mama Mkuu wa Shirika la
Masista wa Mtakatifu Xavery, akionyesha kusikitishwa sana na
kilichotokea kwa Masista hao. Papa anatumaini damu hii ya watu wa Mungu
iliyomwangika bure, itaweza kuwa mbegu ya matumaini katika ujenzi wa
udugu wa kweli kati ya jamii ya watu wa Burundi. Na ameahidi
kuwakumbuka katika sala zake mashahidi hawa wa Injili , na ukaribu wake
kwa shirika, na jumuiya ya waamini nchini Burundi.
Mkuu wa
Shirika la Watawa Xaverian nchini Burundi, Padre Mario Pulcini,
akithibitisha uwepo wa tukio, ameonyesha hisia kwamba ni tukio la wizi.
Na kwamba, Sista Lucia na Sista Olga, waliuawa Jumapili mchana wakati
Sista Bernadetta, alikwenda kupokea Masista wengine waliowasili katika
uwanja wa ndege tokea Italia.
Wakati aliporejea nyumbani
alikutana na hali ya ukimya uliompa wasiwasi na baadaye akiwa na Padre
Mario waliona wenzao tayari walikuwa wameuawa ndani ya nyumba yao. Na
Sista Bernadetta ameuawa usiku wa kuamkia Jumatatu akiwa katika chumba
chake.
Askofu Henry, Jimbo la Parma Italia, kwa niaba ya Kanisa
lote la Parma, amepeleka pia niaba ya waamini wa Parma , salaam zake za
rambirambi kwa Usharika wa Missionari Xaverians, wakiwafariji kwa sala
ya imani kwa Bwana wa Maisha. Askofu pia ametoa ombi kwa Wakristo wa
Jimbo la Parma na kwa wote wenye mapenzi mema, kuwakumbuka Masista hawa
katika sala zao.
Tuesday, September 9, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...