Monday, February 2, 2015

Mwaka watawa wafunguliwa rasmi Jimbo kuu la Dar es salam

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linafungua rasmi Maadhimisho ya Mwaka wa Watawa Duniani, uliotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 2 Februari 2015, Siku kuu ya kutolewa Bwana Hekaluni, sanjari na maadhimisho ya siku ya kumi na tisa ya watawa duniani, iliyoanzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II. Maadhimisho haya yanafanyika katika ngazi ya Kijimbo na katika baadhi ya Majimbo makuu.  
Hayo yamesemwa na Askofu Renatus Nkwande, Mwenyekiti wa Tume ya Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika mahojiano maalum na Radio Vatican. Kwa namna ya pekee anasema, Watawa wanapaswa kuwa ni mashuhuda wa imani dhidi ya ukanimungu, kwa kujikita katika maongozi ya Mungu, Injili ya Kristo na Mashauri ya Kiinjili.

Mons. Liberatus Sangu ateuliwa kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Tanzania!

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Liberatus Sangu kutoka Jimbo Katoliki la Sumbawanga, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Tanzania. Kabla ya uteuzi wake, Askofu mteule Sangu alikuwa ni Afisa mwandamizi katika Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu mjini Vatican.

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR