Thursday, June 26, 2014

World cup 2014 live here>>>>>>>>>.Angalia mechi zote za kombe la Dunia hapa

click here  Portugal vs Ghana
Bonyeza hapa Portugal vs ghana

Safari ya Mwisho ya Marehemu Sr. Kapuli (wasifu wa Sister aliye uwawa na majambazi)


 Sr. Crescentia Kapuli (52) wa Shirika la Bikira Maria Malkia wa Mitume, Jimbo Katoliki la Mbeya meuwawa kikatili kwa kupigwa risasi kifuani na watu wanaosadikiwa kuwa ni amajambazi, siku ya Jumatatu alasiri, tarehe 23 Juni 2014 wakati akitoka Benki, eneo la Ubungo Riverside, Dar es Salaam. 
Jimbo kuu la Dar es Salaam Alhamisi tarehe 26 Juni 2014, majira ya saa 5:00 asubuhi linatarajia kuadhimisha Ibada ya Misa takatifu kwenye Parokia ya Mtakatifu Gaudencia, Makoka kwa ajili ya kumwombea na hatimaye, kuanza safari kuelekea Jimboni Mbeya, atakapopumzishwa kwenye makao ya milele pamoja na watawa wenzake
 Wasifu wa marehemu
Sr. Crescentia Kapuli wa Shirika la Watawa wa Bikira Maria Malkia wa Mitume Jimbo Katoliki Mbeya. Amezaliwa katika Kijiji cha Mkulwe, Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya, Agosti, 29, 1962 katika Kijiji cha mkulwe na kupata ubatizo Agosti, 31, 1962 huko Mkulwe na nambari ya cheti cha Ubatizo ni LB 19703, amepata Komunio ya kwanza Oktoba,11, 1972 na kuimarishwa kwa Sakramenti ya Kipaimara Oktoba, 12, 1972 huko huko Mkulwe.

Sr.Crescentia alikuwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto 12 wa Mzee Peter Kapuli na Mama Maria Nakana. Sr.Cresensia ameingia utawani kama mwomboaji kunako mwaka 1979. Upostulanti mwaka 1980. Unovisi mwaka 1981 hadi mwaka 1983. Akafunga nadhiri za kwanza tarehe 12 Desemba 1983 na baadaye kunako tarehe 12 Desemba 1991 akafunga nadhiri za daima. Tarehe 31 Mei 2009 akaadhimisha Jubilee ya miaka 25 ya maisha yakitawa.

ELIMU
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Mkulwe mwaka 1972 hadi 1978, elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Bigwa ( Bigwa SR’s Secondary School) Mwaka 1994 hadi Mwaka 1997, amesoma chuo cha maarifa ya nyumbani homecraft Mwanjelwa mwaka 1991 hadi mwaka 1992, amesoma Chuo cha Uhasibu Mbeya na Dare Es salaam Mwaka 2000 hadi Mwaka 2002.

UTUME

Sr. Crescentia amewahi kufanyakazi katika Convent ya Kyela akifanya Utume Parokiani mwaka 1984 na kusimamia mradi wa mashine ya kusaga katika nyumba ya watawa iliyoko Mlowo mwaka 1985. Msimamizi wa Jiko la Nyumba ya Utawala Jimbo Katoliki la Mbeya mwaka 1986 hadi mwaka 1989. Mlezi msadizi wa Wanafunzi wa Kitawa(Wanovisi) Mlowo mwaka 1993 hadi mwaka 1998. Mlezi Msaidizi wa Wanafunzi wa Kitawa - Kisa Aspiranti Mwaka 1999 hadi mwaka 2000.

Utume katika Convent Parokia ya Mwambani mwaka 2001. Utume Uaskofuni Convent akiwa Mama Mkubwa wa nyumba na Mhasibu Jimboni Mbeya mwaka 2002 hadi 2009. Utume Gua Convent akiwa Mama Mkubwa wa nyumba; Utume Parokiani na Mlezi wa Wawata 2009 – 2011.

Utume Jimbo kuu la Dar es Salaam akiwa Mama Mkubwa katika Convent ya Makoka, Mhasibu Sekondari ya Makoka na Chuo cha Ufundi cha Mwenyeheri Anwarite 2011 – 2014 hadi mauti yalipomfika.

Jimbo kuu la Dar es Salaam, Alhamisi asubuhi tarehe 26 Juni 2014 wanaadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumwombea na kumwaga Marehemu Sr. Crescentia Kaupili na baadaye msafara utaondoka kuelekea Jimboni Mbeya. Taarifa za awali zinasema mara baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu Sr.Cresensia utaingizwa katika makao makuu ya Shirika la Bikira Maria Malkia wa Mitume, Jimbo Katoliki la Mbeya.

Baada ya kutoka katika makao makuu ya Shirika safari itaanza kuelekea katika safari yake ya mwisho hapa duniani Sr.Cresensia katika shamba la Mungu la Masista maeneo ya Hasamba, wilayani Mbozi, mkoani Mbeya. Maziko yanatarajiwa kufanyika Jumamosi, tarehe 28 Juni 2014, Mama Kanisa atakapokuwa anaadhimisha Siku kuu ya Moyo Safi wa Bikira Maria.

Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa amani, Amina.

MASOMO YA 29 JUNI JUMAPILI YA 14 YA MWAKA "A" 2014 (KIJANI)

29
   JUNI 
 JUMAPILI YA 14 YA MWAKA "A"
2014 (KIJANI)


RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
IBADA YA MISA YA KWANZA 12:15 – 1:45 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 2:00 – 3:50 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA TATU SAA 4:00-5:20 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:15 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:00 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA – MBWENI MPIJI.
IBADA YA MISA NI 3:00 – 5:00ASUBUHI

SOMO 1:Zek.9:9-10


Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokuvu; ni mnyenyekevu, amepanda Punda; naam, mwana-punda, mtoto wa Punda. Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na Farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiri mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka mto hata mwisho wa dunia.



SOMO 2:1Rum. 8:9, 11-13

Roho wa Mungu anakaa ndani yetu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na roho wa Kristo, huyo si wake. Lakini ikiwa roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa roho wake anayekaa ndani yenu. Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili; kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa roho, mtaishi.



INJILI: Mt.11:25-30

Wakati ule Yesu alijibu, akasema, Nashukuru, Baba, Bwana wa mbingu na Nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. Akasema, nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuae mwana, ila Baba; wala hakuna amjuae Baba, ila mwana, na ye yote ambaye mwana apenda kumfunulia. Nyoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini; na mzigo wangu ni mwepesi.



 MATANGAZO

mara baada ya misa ya pili saa 4:00 asubuhi, Parokiani Boko, mazoezi ya washiriki wa ziara ya taendelea;

Jumanne tarehe 1/7/2014 tunatarajia kuanza safari ya kuelekea Dareda, na tutainjilisha hapo kwa siku nne na tarehe 5/7. tutaelekea parokia ya BM-mpalizwa mbinguni Sanu ....tarehe 6/7 tutaenda parokia ya Daudi na endabashi na tarehe 7/7 tutaenda Mbuga ya Wanyama ya Ngorongoro,,,,,Sisi ni Askari kamili wa Yesu tuzidi kuombeana tuweze kwenda kumtangaza huyu Yesu ambaye ndiye Njia ya Uzima na Ukweli katika Maisha yetu sisi Vijana.......Mapen

Tunawatikia Dominika njema, Amani ya Bwana Iwe nasi.........Mapendo sana,,,,,,,

MAJAMBAZI WALIOMUA MTAWA ( SISTER KAPULI) WA MAKOKA

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imeanzisha msako mkali, kuwatafuta watu waliohusika na mauaji ya Mhasibu wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makoka jijini Dar es Salaam, Sista Cresencia Kapuri (50), ambao utahusisha vikosi vyote vya Polisi. Vikosi hivyo ni Usalama Barabarani, askari wa doria wanaotumia pikipiki na magari, wapelelezi na askari Polisi wa kawaida.
 
Mauaji ya mtawa huyo, yalitokea juzi mchana katika eneo la Ubungo Riverside, jijini humo, ambapo alipigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi na kumpora Sh milioni 20 pamoja na nyaraka mbalimbali za ofisi.
 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliwaambia waandishi wa habari ofisi kwake jana kuwa Sista Cresencia wakati anapigwa risasi, alikuwa ameongozana na wenzake, ambao ni Sista Brigita Mbaga (32) na dereva wao Mark Mwarabu, aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Hilux Pick-Up, yenye namba T213 CJZ.
 
Kova alisema wakati watawa hao, wakitoka katika Benki ya CRDB Tawi la Mlimani City, walipofika Ubungo Riverside kulipa deni la chakula katika duka la Thomas Francis, ndipo walitokea watu hao wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa na pikipiki, ambayo haikusomeka namba, huku mmoja akiwa na bunduki aina ya SMG.
kova  
“Yule dereva wa gari la masista walimpiga risasi katika kidole gumba cha mkono wa kulia na kisha kumpiga mtawa huyo risasi ya kifuani na kupora kiasi hicho cha fedha na nyaraka hizo,” alisema Kova. 
 
Alisema kuwa jambo kubwa walilogundua ni kuwa matukio mengi ya ujambazi, hasa unaohusisha wananchi kuporwa kiasi kikubwa cha fedha, yanaanzia katika mabenki, hivyo kuna uwezekano wa watu ambao si waaminifu, wanafanya uhalifu huo.
 
Alisema kuwa katika matukio ya aina hiyo, majambazi huwafuatilia wateja wanapoingia au kutoka katika benki mbalimbali.
 
Alisema imeonekana kwamba mara nyingi benki, zinapohitaji kusafirisha pesa nyingi, hutumia askari au taasisi nyingine za usalama kusafirisha fedha zao.

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR