Tuesday, December 30, 2014

masomo ya tarehe 30/12/2014

Jumanne, 30 Desemba 2014
Jumanne katika Octava ya Kuzaliwa Bwana

1 Yoh 2:12-17;
Zab 95: 7-10;
Lk 2: 36-40

Kuitwa kuwa Watakatifu

Katika Injili Yesu anatamka kuwa yeye pekee anamfahamu Baba. Ni Neno la Mungu ndilo linaufanya ujio wake mioyoni mwetu, ndilo linalomfanya Yeye afahamike mioyoni mwetu. Jibu letu sio tu kushinda ovu, bali katika hali chanya kutembea katika njia ya utakatifu. “watakatifu sio watu wakubwa sana, wala hawakuzaliwa wakamilifu. Wapo kama sisi, kama kila mmoja wetu … je, nini kiliyabadilisha maisha yao? Walipo utambua upendo wa Mungu, waliufuata kwa moyo wao wote bila ya kubakiza wala bila ya unafiki” – Papa Fransis. Utakatifu sio upendeleo wa watu wachache, wa wale wote wanaovaa kanzu au kiremba, bali pia wale wote wenje majinsi na viatu vya tennis; ni wa wale wote wanaokwenda katika filamu, wanaosikiliza muziki, wanaotumia muda wao na marafiki zao. Lakini wote wanahitaji kumpatia Mungu nafasi ya kwanza, awe mbele ya kazi zao, familia zao, na marafiki zao. Tunawahitaji watakatifu wanaotafuta muda kwa ajili ya kusali kila siku na wanaojua namna ya kuwa katika upendo na usafi, useja, na mambo yote mema. Tunawahitaji watakatifu walio na moyo wa kujitolea katika kuwasaidia masikini na kuyafanya mabadiliko yanayohitajika katika jamii.

Sala: Bwana, tupe busara ya kuishi katika ulimwengu lakini si kujikita sisi wenyewe katika hali yake. Amina.

"Kusudi kubwa la sala ya kanisa la nyumbani ni kuhudumia kama utangulizi wa kiasili kwa ajili ya watoto kuwa sala ya kiliturjia ya Kanisa zima, katika maana ya kuifanyia maandalizi na kuieneza katika maisha ya binafsi, familia na kijamii. Kwa sababu hiyo, ni muhimu kushiriki kwa wanajumuiya wote wa familia ya Kikristo katika adhimisho la Ekaristi, hasa siku za Jumapili na sikukuu, na masakramenti mengine, hasa sakramenti za kuingizwa watoto katika Ukristo. Miongozo ya Mtaguso Mkuu ilifungua wajibu Mpya kwa familia ya kikristo ilipoorodhesha familia kati ya vikundi vile ambavyo ilipendekeza kusali sala ya Kanisa kwa pamoja. Kwa namna hiyo hiyo, familia ya Kikristu itakazana kuadhimisha nyumbani, na kwa namna inayofaa kwa wanajumuiya wake, nyakati na sikukuu za mwaka wa kiliturjia." – Baba Mtakatifu Yohani Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris Consortio (WAJIBU WA FAMILIA YA KIKRISTU KATIKA ULIMWENGU WA KISASA)- 61.

VIWAWA BOKO
www.viwawaboko.blogspot.com

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR