Showing posts with label UCHAGUZI WA PAPA 2013. Show all posts
Showing posts with label UCHAGUZI WA PAPA 2013. Show all posts

Tuesday, March 12, 2013

Makardinali wanaoingia kwenye Conclave mjini Vatican

Jiografia ya Makardinali wanaoingia kwenye Conclave mjini Vatican



Wakati huu wa uchaguzi wa Papa Mpya jambo la msingi kukumbuka ni kwamba, Kanisa ni moja, Takatifu, Katoliki, na la Mitume. Makardinali katika mwelekeo wa mawazo yao ya jumla wamebainisha kwamba, wanataka kumchagua Kiongozi mkuu wa Kanisa atakayeliongoza Kanisa la Kristo kama Baba mwenye huruma na mapendo, kielelezo cha umoja na mshikamano wa Kanisa; kiongozi mwenye dhamana ya kulinda na kusimamia kweli za Kiinjili, Maadili na utu wema. Haijalishi mahali anapotoka mtu, jambo la msingi ni kiongozi.

Kwa jumla, kuna Makardinali 115 wenye haki ya kupiga na kupigiwa kura wanaoanza mchakato huu kwenye Kikanisa cha Sistina kwa kula kiapo, tafakari ya Neno la Mungu na uchaguzi wa kwanza. Makardinali 60 wanatoka katika nchi za Ulaya, kuna Makardinali 33 kutoka Amerika, Makardinali 11 kutoka Barani Afrika, Asia kuna Makardinali 10 na Oceania kuna Kardinali mmoja. Itakumbukwa kwamba, kwenye Conclave ya Mwaka 2005, Kenya haikuwa na Kardinali, lakini mwaka huu, Kardinali John Njue yupo.

Kuna Makardinali 40 ambao wametekeleza utume wao au bado wanaendelea kufanya shughuli mbali mbali mjini Vatican. Kati ya Makardinali wenye haki ya kupiga na kupigiwa kura 67 ni wale walioteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita.

Wastani wa umri wa Makardinali wanaopiga kura ni kati ya miaka 71. Kardinali Walter Kasper mwenye umri wa miaka 80 ni kati ya wale waliobahatika kuingia katika Conclave wakiwa na umri mkubwa zaidi. Kati ya Makardinali vijana wana umri wa miaka 54 na 56. Kardinali Luis Antonio Tagle ana umri wa miaka 56.

Mwishoni, itakumbukwa kwamba, kundi la Makardinali Maaskofu lina Makardinali 6; Kundi la Makardinali Mapatriaki lina jumla ya Makardinali 4; Kundi la Makardinali Mapadre lina jumla ya Makardinali 153 na Makardinali Mashemasi wako 44. Kuna jumla ya Makardinali 207.

Hatua za mwisho mwisho(PAPA)

Hatua za mwisho mwisho kabla ya Papa Mpya kutokeza hadharani!



Padre Federico Lombardi msemaji mkuu wa Vatican anabainisha kwamba, uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro unakamilika kwa Kardinali kupata theluji mbili ya kura zote halali zilizopigwa. Baada ya hapo, Dekano wa Makardinali ambaye wakati wa uchaguzi ni kardinali Giovanni Battista Re, atamuuliza Kardinali aliyechaguliwa kama anakubali kisheria kwamba, amechaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Baada ya hapo, ataulizwa jina ambalo atalitumia katika utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Wakati wote huu, Mshehereheshaji mkuu wa Papa ndiye atakayekuwa anachukua rasmi taarifa zinazotolewa na Papa Mteule akisaidiwa na Washereheshaji wengine wawili wanaokuwepo mahali hapo kama Mashahidi. Seehemu hii ya mchakato ikikamilika, hapo karatasi zilizotumika kwa ajili ya kupigia kura zinachomwa na hapo moshi mweupe unatoka kuashiria kwamba Kanisa limempata Papa Mpya.

Papa Mpya ataelekea kwenye "Chumba cha machozi" neno ambalo pengine linaonesha ile hali ya ndani anayokuwa nayo Kardinali baada ya kuambiwa kwamba, amechaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Anaporudi kwenye Kikanisa cha Sistina, Injili inayozungumzia Ukulu wa Mtakatifu Petro inasomwa, Makardinali wanasali kwa kitambo kidogo na hapo Makardinali moja baada ya mwingine wanaanza kwenda kula kiapo cha utii kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro, wakati wote huu, Makardinali na Papa wanaendelea kumshukuru Mungu kwa kuimba utenzi wa shukrani, Te Deum.

Padre Lombardi anasema, Papa Mpya kabla ya kwenda kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kutoa baraka zake kwa mji wa Roma na Ulimwengu kwa ujumla, "Urbi et Orbe" atapitia kwanza kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Paulo kusali kwa kitambi kifupi na baadaye atawasalimia na kuwapatia baraka zake za kitume waamini, mahujaji na wote watakaokuwa wamekusanyika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro. Papa mpya ataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kusimikwa kwake, siku yoyote inayoonekana inafaa zaidi!

Shirikisha Invia articolo

Saturday, March 9, 2013

UCHAGUZI WA PAPA 2013


Masuala ya Jamii

Makadinali wakutana vatikani

Makardinali wa kanisa Katoliki kutoka sehemu tofauti za dunia,wameanza utaratibu wa kumchagua mrithi wa Papa Benefickt wa XVI aliyejiuzulu mwezi uliopita.
Zoezi hilo limeanza leo Vatican saa 3.00 asubuhi kwa saa za Vatican sawa na saa 6 mchana kwa saa za Afrika Mashariki kwenye ukumbi wa New Synod Hall.
Mkutano huo ndio utafungua mchakato wa uchaguzi wa Papa mpya na unatarajiwa kuandaa ratiba ya uteuzi wa papa mpya.Makardinali hao ndio watapanga siku ya kufanyika mkusanyiko wao unaoitwa `Papal Conclave' kwa ajili kufanya uchaguzi huo.
Kutokana na utaratibu wa kanisa Katoloki, uchaguzi wa Papa hutakiwa kufanyika siku 15 hadi 20 kufuatia siku kiti cha papa kilipoanza kuwa kitupu na Uchaguzi kwa kawaida hufanyika katika Kanisa la Sistine Chapel.
Takribani makardinali 115 kutoka nchi mbalimbali duniani,wanahusika na uchaguzi huo wa Papa ambapo Kati ya hao, makardinali 67 waliteuliwa na Papa Benedict,Joseph Aloisius Ratzinger.
Kwa upande wake aliyekuwa papa ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani amekuwa akitumia muda kufanya ibada, kusoma vitabu na meseji za kumtakia kila la kheri papa aliejuzulu kutoka sehemu mbalimbali duniani na kutafakari.
Hadi sasa hakuna tarehe yoyote iliotajwa kuhusu uchaguzi huo wa papa ingawa vyanzo vya habari vya Italan vimedokeza kuwa huenda Machi 11 2013 ikawa siku hiyo ya uchaguzi wa papa.
Kiongoazi wa chuo cha makardinali Angelo Sodano ameongea kuwa siku maalumu ya kuanza kwa uchaguzi huo,haitatajwa hadi hapo makardinali wateule wote watakapo wasili mjini Rome
Papa mpya atatokea bara gani?

Kadinali Ricardo Jamin Vidal wa Philippines(kulia) na Luis Antonio Tagle wamewasili kuhudhuria mkutano wa makadinali kabla ya kongamano litakalomchagua Papa mpya

Nafasi ya Papa ajae imeendelea kuwa wazi kwa kila mtu kutoka katika maeneo mbalimbali ya dunia, na kutoka katika makanisa mbalimbali.
"Wakati alipofariki John Paul II mwaka 2005, kila mtu alikuwa anafikiria atakaeshinda nafasi hiyo kwa mwezi huo naku ra ilikuwa muda mfupi tuu'' amesema kadinali alijiuzulu akiongea na shirika la habari la AFP.
Kwa upande wa Afrika Makardinali waliotajwa ni pamoja na Peter Turkson kutoka Ghana, Robert Sarah Guinea na Wilfrid Napier kutoka Afrika Kusini

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR