Wednesday, July 18, 2012

KUTOKA VIWANJANI
Jana zilichezwa mechi za  ligi ya Parokia ya Boko maarufu kama Majeta cup, mechi ambayo ilikuwa na msisimko mkubwa ilikuwa kati ya Bunju na Mbweni iliyochezwa katika uwanja wa Mbweni, majigambo yalikuwa mengi kabla ya mechi ,mvuto mkubwa ukiwa kwa makocha wa timu hizo ndg James Nkii kocha wa timu ya Bunju, na ndg Fabian Masanja kocha wa timu ya Mbweni. mpira ulikiwa upo sawa kwa timu zote mpaka wakati wa mapumziko timu hizi zilikuwa hazijafungana, kipindi cha pili kilianza kwa nguvu sana, huku kila timu ikifanya mabadiliko ambayo kwa upande wa mbweni, yalizaa matunda kwani walipata magoli wawili ya haraka, dakika chache kabla mpira kuisha bunju nao waliamkaa na kupata goli moja la kufutia machozi mwisho wa mpira matokeo yalikuwa Mbweni 2 na Bunju 1
HISTORIA YA VIWAWA KIDUNIA.
Viwawa ilianzishwa mwaka 1924 mji wa Brussel nchini Ubelgijina Padri Joseph Cardjin na kupitishwarasimi na kama chama cha kitume cha vijana Kimataifa na Balaza la Kipapa Vatican mwaka 1950.Padri Joseph Cardjin pia alianzisha YCS,hivyo VIWAWA Na YCS alianzisha yeye.Makao makuu ya VIWAWA Duniani yako Roma-Italia chini ya Rais Seraphina kutoka Korea,Katibu Mkuu Jules Adached toka Bejin,Mhazini Lisa Vaccariano toka Italia na Mratibu wa kimataifa Arniel Iway toka Philipini na mshauri Pd.Joseph Ramaguera toka Spain. 
 HISTORIA YA VIWAWA TANZANIA.
Viwawa Tanzania iliingia mwaka 1959 katika Parokia ya Msimbazi,Jimbo kuu la Dar es salaam chini ya Mwanzilishi Padri Hendrikus Johannes Brinkhof maarufu kama Padri Mansuetus na kupitisha rasimi chama cha Kitume cha Vijana na Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) mwaka 1979.Baada ya kupitisha hapo kilitambulishwa pote Tanzania kama chama cha Vijana Wakatoriki Wafanyakazi Tanzania(VIWAWA).
Mpaka sasa chama hiki kip ,kuanzia ngazi ya Jumuiya,Mtaa,Kanda,Kigango,Parokia,Kijimbo,Taifa na Kimataifa.

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR