Tuesday, April 30, 2013

PAROKO CUP 2013

Baada ya kufanikiwa kwa asilimia kubwa, kwa msimu wa mwaka jana...Mwaka huu maandalizi yameanza mapema kabisa.

Msimu wa mwaka 2012 tulikuwa na timu nne za mpira wa miguu,kwa upande netball hapakuwa na timu.
Mashindano yaliendeshwa kwa mfumo wa ligi, Mshindi kwa upande wa mpira wa miguu walikuwa Kigango cha Mbweni- walipata zawadi ya kombe na Medali,kwa upande wa Mpira wa Pete (Netball) tulifanya Bonanza na washindi walikuwa Kigango cha Boko- walipata zawadi kombe na medali

kw msimu huu wa mwaka 2013-2014 tumejitahidi kuboresha zaidi kwa kuongeza idadi ya timu toka timu nne hadi timu saba za mpira wa miguu na mpira pete.
pia tumeandaa zawadi nyingine zaidi ya kombe na medali. ikiwa ni pamoja na vyeti vya ushiriki kwa kila mwanamichezo.
Kwa upande wa michezo ya ndani tumejipanga kuboresha Vikundi vya maigizo, kuunda kikundi vya ngoma, lengo nikuona kila kijana anashiriki kikamilifu 

ili kumuwezesha kila kijana kushiriki tukaona tuunde vigango vya kimichezo. kama imefuatavyo;
Kigango cha boko tumekigawa sasa vitakuwa vigango vinne lengo kubwa ni kila kijana aweze kushiriki
Kigango cha Mt. Raphael
kigango cha Mbweni
Kanda ya Antony wa Padua(kigango kimichezo)

Tukiwa tunaamini michezo huwa inaleta afya nzuri pia inaweleta watu pamoja ni malengo yetu kuona kila kijana wa parokia hii anashiriki kwa namna moja katika michezo hii.
tunatarajia mashindano kufunguliwa mwezi june, hivyo tunazidi kusisitiza timu ziendelee na mazoezi muda si muda tutawatangazia ratiba nzima ya mashindano.

TUNAWATAKIA MAANDALIZA MEMA ...MAPENDO SANA

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR