Tuesday, January 22, 2013

nembo ya mwaka wa imani





Nembo ya Mwaka wa Imani
Imeundwa kwa alama mbalimbali zinazobeba maana maalum.
A) Mashua: Hii ni ishara ya Kanisa linalosafiri.
B) Mlingoti: Huu ni Msalaba ambao juu yake kuna monogramu (chapa ya herufi zaidi ya moja zinazochanganyika pamoja, moja juu ya nyingine) IHS. Hizi ni herufi tatu za kwanza za Kigriki za jina la Yesu: I = Iota, H = eta, S = Sigma. Alama hizi zinatumika pia kuonyesha kifupisho cha jina la Yesu ambapo kwa kilatini zinatumika kusimama badala ya maneno: Iesus Hominum Salvator; yaani, Yesu Mwokozi wa Wanadamu.
C) Mduara: Nyuma ya monogramu ipo alama ya mduara ambao unaizunguka pia monogramu hiyo. Hii ni alama ya Jua ambayo inawakilisha Ekaristi Takatifu.
(Tafsiri ya maelezo, TEC, 2012)
Nembo ya Ofisi ya Vijana
Vijana wane walioshikana mikono wanasimamia vyama vya Kitume vinavyounda umoja wa Vijana. Katikati kuna alama ya kamba, chini ya neno Fidei. Kamba ni chombo cha kufunga vitu viwili au zaidi. Kamba inayoshikanisha vijana wote ni Imani. Neno Fidei ni neno la Kilatini lenye maana, “ya Imani”. Yaani, umoja huu unahusu imani.
Programu zote za Mwaka wa Imani zitakuwa na nembo hii. Pia, kauli mbiu ya mwaka huu, kwetu vijana, itakuwa pia sala, maneno ya mwinjili Luka,


“Bwana, utuongezee imani

Luka 17:5.
                                   2012—2013

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR