kuelekea kwenye semina ya Mwaka wa familia tarehe 28-29/11/2014. vijana wanaandaliwa kujenga familia Bora familia ya Kikristo, familia ambayo ni kanisa Dogo, kanisa la nyumbani
Matunda ya familia bora ni kuwa na Imani, mapendo na matumaini miongoni kwa wanafamilia, kazi mbayo ni kubwa, familia ilikabiliana na kinzani
pamoja na changamoto kubwa za kitamaduni, lakini imani ikaendelea kukua
na kuota mizizi katika familia zetu,
tunu za maisingi ya Kikristo kuleta mabadiliko miongoni mwa
wa vijana ambao walianza kupata malezi hayo tokea utotoni ,hapo ndipo huibuka miito ya kipadre na kitawa, neema na baraka
kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Kwa sasa vijana tunaendelea kukabiliana na
changamoto mbali mbali katika maisha, hasa kutokana na ongezeko la
umaskini, hali ambayo inazifanya familia nyingi kutafuta njia za mkato;
mambo ambayo wakati mwingine yanahatarisha imani na matokeo yake ni watu
kukata tamaa. Baba Mtakatifu anasema, Familia inapaswa kupewa
kipaumbele cha kwanza kwani ni msingi wa Jamii, mahali ambapo watu
wanajifunza kuishi kwa pamoja, licha ya tofauti zao msingi na kwamba ni
mahali pa kurithisha imani, dhamana inayotekelezwa na wazazi. Familia ni
madhabahu ya Injili ya Uhai, inayopaswa kudumishwa na kuendelezwa.
Wanandoa ambao wengi ni wazazi wetu na vijana wenzetu
wadumishe uaminifu na mapendo ya ndoa, wasaidie majiundo ya kina kwa
watoto wao sanjari na kudumisha tunu msingi za maisha ya ndoa na familia
yanayojikita katika Mafundisho tanzu ya Kanisa na kumwilishwa katika
uhalisia wa maisha, ili kuwa kivutio kwa vijana wanajianda kuingia kwenye wito huo.
Viongozi wa Kanisa
waendelee kuwa karibu zaidi na vijana katika malezi na makuzi yao, ili
waweze kuwa na utambulisho makini, tayari kushiriki katika kazi ya
uumbaji kwa kujikita katika wito wa ndoa au Daraja takatifu au maisha ya
kitawa kwa ajili ya wokovu wa roho za watu. Vijana wafundwe
kuchuchumilia usafi wa moyo pamoja na kukuza ushirikiano miongoni mwa
utume wa vijana wa Parokia hizi, ili wote waweze kujisikia kuwa wako ndani
ya Familia ambayo kimsingi ni Kanisa dogo la nyumbani. ...bonjeza hapa Kuendelea kusoma hapa
Tuesday, November 18, 2014
Mwaka wa Katekesi Jimbo Katoliki Ifakara
Mwaka
wa Imani uliotangazwa na kuzinduliwa na Baba Mtakatifu mstaafu
Benedikto wa kumi na sita na kuhitimishwa kwa kishindo kikuu na Papa
Francisko, lilikuwa ni tukio la neema kubwa kwa maisha na utume wa
Kanisa. Ilikuwa ni nafasi kwa waamini kupitia tena Mafundisho ya Mababa
wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, ili kuweza kuyapyaisha katika
uhalisia wa maisha na utume wa Kanisa katika ulimwengu mamboleo.
Mwaka wa Imani, ulikwenda sanjari na maadhimisho ya miaka 20 tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipochapisha kwa mara ya kwanza Katekesi Mpya ya Kanisa Katoliki, bila kusahau Kitabu cha Sheria za Kanisa; matunda makuu ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican. Waamini kwa namna ya pekee kabisa walihamasishwa kufanya tafakari ya kina kuhusu Imani wanayoungama katika Fumbo la Utatu Mtakatifu, Kanisa na Mambo ya nyakati.
Waamini walihimizwa kutambua umuhimu wa maadhimisho ya Sakramenti za Kanisa, ili waweze kushiriki kikamilifu na hatimaye kujipatia neema na baraka zinazotolewa na Mama Kanisa. Mwaka wa imani, ulikuwa ni nafasi kwa waamini kujikita katika ushuhuda unaoonesha imani tendaji kwa kukumbatia Amri za Mungu kama dira na mwongozo wa maisha yao ya kiroho na maisha ya hadhara.
Waamini kwa mara nyingine tena, walihimizwa na Mama Kanisa kumwilisha imani yao kwa Kristo na Kanisa lake kwa njia ya Sala na Matendo ya huruma. Kwa maneno machache, Mwaka wa Imani, ilikuwa ni fursa ya kutafakari kwa kina na mapana kuhusu: Imani, Sakramenti za Kanisa, Amri za Mungu na Maisha ya Sala. Mwaka wa Imani, kimekuwa ni kipindi cha neema ambacho kimeyasaidia Makanisa mahalia kujiwekea mbinu mkakati wa kuimarisha imani kwa njia ya Sinodi za Majimbo au Mwendelezo wa Maadhimosho ya Mwaka wa Imani kwa kuchagua mada mbali mbali kadiri ya mahitaji ya Kanisa mahalia.
Askofu Salutaris Melchior Libena wa Jimbo Katoliki la Ifarakara, Tanzania, katika mahojiano maalum na Gazeti la AMECEA anasema kwamba, mara baada ya kuadhimisha Mwaka wa Imani, kulionekana kwamba, kunahitaji la kuendelea kuwaimarisha waamini katika Mafundisho tanzu ya Kanisa kwa kujikita hasa zaidi katika Katekesi ya kina, zoezi la kiroho linaloigusa Familia ya Mungu Jimboni Ifakara.
Kutokana na hitaji hili msingi, Jimbo Katoliki la Ifakara hapo tarehe 19 Marchi 2013, katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Mtakatifu Yosefu mchumba wake Bikira Maria na Msimamizi wa Kanisa la Kiulimwengu, Askofu Libena akazindua Mwaka wa Katekesi Jimbo Katoliki Ifarakara, utakaofungwa rasmi hapo tarehe 19 Marchi 2015, Jimbo Katoliki Ifakara litakapokuwa linaadhimisha Mwaka wa Tatu tangu kuundwa kwake na Baba Mtkatifu mstaafu Benedikto XVI. Ifakara ni kati ya majimbo machanga sana nchini Tanzania, lakini linaendelea kucharuka kwa maendeleo ya watu kiroho na kimwili.
Askofu Libena anasema, Mwaka wa Katekesi umekuwa ni fursa kubwa kwa Familia ya Mungu Jimboni Ifakara kuweza kupyaisha tena mafundisho tangu ya Kanisa, dhamana inayotekelezwa kuanzia kwenye ngazi ya: Familia, Jumuiya ndogo ndogo za Kikristo, Vigango, Parokia na katika ngazi ya Jimbo. Lengo ni kuhakikisha kwamba, Jimbo Katoliki Ifakara litakapokuwa linaadhimisha kumbu kumbu ya miaka mitatu tangu kuundwa kwake, waamini wawe wameifahamu Katekesi kwa kina na mapana yake.
Jimbo Katoliki Ifakara linapenda kumwilisha imani katika matendo kwa kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu ambayo kwa sasa inaonekana inahitaji kupewa uzito wa pekee kutokana na ukweli kwamba, kwa masuala ya afya, Jimbo limejiimarisha kwani kuna Hospitali ya Rufaa yenye vitanda 370 na idadi nzuri ya Zahanati ambazo zinaendelea kutoa huduma bora kwa kuzingatia utu na heshima ya binadamu.
Jimbo Katoliki la Ifakara linamiliki na kuendesha shule kadhaa za msingi, lakini kwa bahati mbaya, linamiliki Sekondari moja tu, changamoto ya kuendelea kuwekeza katika elimu, ili kuweza kuwafunda vijana wa kizazi kipya: kiroho na kimwili, tayari kulitumikia Taifa na Kanisa kwa ujumla.
Itakumbukwa kwamba, Jimbo Katoliki la Ifakara liliundwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kunako tarehe 14 Januari 2012 na kuzinduliwa rasmi tarehe 19 Marchi 2012 na Askofu Salutarius Libena akawa ni Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki Ifakara:>>>>>bonyeza hapa soma zaidi hapa

Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...