Wednesday, February 27, 2013

HISTORIA FUPI YA MAKANISA YA MWANZO YA ZANZIBAR

WARENO 1500 – 1800

Ukiristo uliletwa kwa mara ya mwanzo Zanzibar na Wareno.  Wareno wakielekea juu kutoka kusini baada ya kufanikiwa kuizunguka Rasi ya matumaini mema – Cape of Good Hope katika mwaka 1488 walifanya jaribio la nguvu la kudai bandari, njia za biashara na raslimali kiasi cha maili 2000 za mwambao wa Afrika.
Mara tu ya kuwasili Zanzibar Wareno katika mwaka 1499 walianzisha Ujumbe wa Kanisa la Kikatoliki na kituo cha biashara ndani ya mji wa Zanzibar.  Wareno kwa miaka 200 iliyofuata walihodhi njia za baharini za meli za Afrika Mashariki na walijitahidi kuanzisha msururu wa makaazi katika eneo la mwambao.  Mabaki ya makaazi ya Wareno bado yanaweza kuonekana karibu na Fukuchani Kaskazini Unguja na Kisiwani Pemba.  Ngome Kongwe ambayo ipo karibu na bandari ya mji wa Zanzibar ilijengwa juu ya eneo lilipokuwepo kanisa dogo la kikatoliki la mwanzo baada ya kutekwa na Jeshi la Oman.  Jeshi hili la Oman inasemekana liliitwa na wenyeji wa Zanzibar na Pemba ili kuwasaidia kuwangóa Wareno waliokuwa makatili na madhalimu.
Baada ya miongo ya vita na maangamizo ambayo yaliyoshuhudi  kuwaka moto mji wa Mombasa, Wareno walirudi nyuma, na kurejea kuendea kusini, mbali na mafikio ya mashambulizi ya moja kwa moja ambayo yaliyotokana na pepo za miongo za jahazi (waarabu). 

OASISI YA UVUMILIVU (OASIS OF TOLERANCE)

Katika mwaka 1841 mpiganaji wa Kioman/Oman Sultan, Seyyid Said alivutiwa sana na visiwa hivyi vya Zanzibar kwa hiyo alihakikisha anahamishia makao makuu yake Zanzibar kama ni mji mkuu.  Malezi yake katika maisha ya Jangwani yalimshajiisha yeye kwa nguvu zake zote kuviendeleza visiwa hivyi vyenye ustawi.  Sultan Seyyid Said aliona Zanzibar kama kama ni Oasisi katika bahari.  Alisimamia mipango  mikubwa ya upandaji miti, alichimba visima vya maji vyingi tu na kujenga nyumba nyingi ambazo zilitosha mamia ya wageni.  Sultan alitambua wageni watakaa na kujiliwaza katika Oasisi.  Na alijua kwamba biashara itakuwa na kufanyika katika eneo hili ikiwa litaimarishwa kwa vitu na mambo mengine pamoja na usalama.  Vile vile alitarajia na kutambua kwamba angelipata asilimia fulani inayotokana na shughuli za kibiashara zitakazo endeshwa Visiwani kama ni malipo ya kuviimarisha visiwa hivyi.  Aliwakaribisha na kuwaomba wafanyabiashara kutoka India kufungua matawi ya ofisi zao ndani ya Zanzibar ili kuimarisha biashara.  Wafanyabishara hawa wengi kutoka India walikuwa ni raia wa kiingereza hii ilikuwa ni kwa sababu ya kutekwa India na Uingereza.  Kwa maana hiyo, alianza kuwakaribisha maofisa wa kiingereza visiwani ili kuwakilisha maslahi ya raia hawa wahindi wa kiingereza.  Mara tu tena baadae alianza kuingia katika mikataba rasmi ya kibiashara na Serikali ya kiingereza na Serikali nyengine za Magharibi.
Majengo ya biashara yalijengwa ndani ya Mji Mkongwe na Kampuni za Kimarekani, Kijerumani, Ufaransa na na Kiingereza.  Bandari ya Zanzibar ilitoa huduma za fueli na kufanyia matengenezo Meli za kivita na vyombo vya usafiri vya wafanyabiashara.  Meli hizi zilileta mapote ya ziada ya watu wa magharibi ndani ya Zanzibar.  Kama ni makaribisho mema ya wageni wengi katika Oasisi yake.  Sultani aliruhusu watu wa imani zote kuendesha shughuli zao za kidini walivyopenda.
Akiwa Muislamu mwenye imani kamili, Sultani alionyesha mfano bora wa uvumilivu juu ya mahitajio  ya kidini ya watu wengine.  Wakati huo huo akijenga furaha na imani katika dini ya mababu zake, kwa bidii zote.  Warithi wake alifuata utaratibu wa Sultani Seyyid, wakiruhusu kuanzishwa mahekalu mengi tu ya kihindi, makanisa mawili, moja la kikatoliki na kiprostanti, sehemu za kimazishi za zoroastriani na misikiti kwa kila dhehebu kuu au dogo la kiislamu ndani ya mji mmoja.

1800 – 1900

WAKATOLIKI, MAKUNDI YA WAKIRISTO WASIOPENDA MIKUTANO ASMI, VITA AU GHASIA (QUAKERS) NA UJUMBE WA VYUO VIKUU KWA AFRIKA YA KATI ( UMCA)

Baada ya Wareno kurudi nyuma Wakiristo kidogo tu Wakigoa ndio waliobakia Zanzibar.  Wakiristo hawa hawakuwa na kanisa la kufanyia Ibada lakini waliweza kuifanya hai jumuia yao kwa kwa kuifanya ibada zao kibinafsi.  Baadae katika miaka 1800 makundi ya watu wa wamagharibi yalianza kujumuisha wamisionari na wachungaji wamisionari waliokuwa wakipita pita mara chache na wachungaji katika meli bandarini.  Katika mwaka 1844 wamisionari wa kikiristo zaidi wa kudumu waliwasili Afrika mashariki kwa kupitia mchungaji wa kilutheri Joseph Krapf na wafuasi wawili ambao walifanya kazi kwa ajili wa Jumuia ya kimisheni ya kanisa la kiingereza (English Church Missionary Society).  Wakifanyakazi, Mombasa, walitembelea Zanzibar na miaka michache mbeleni walitoa kamusi bora kabisa la Kiswahili lakini hawakuwahi kuanzisha kanisa ndani ya visiwa hivyi. 
Ukuwaji wa harakati dhidi ya utumwa ndani ya Uingereza ulishajiisha raghba ya wamisionari wakiristo, ikikuzwa na hotuba ya David Livingstone aliyoitoa mwaka 1857 akiomba Uingereza kupeleka wamisionari na wafanyakazi Afrika.  David Livingstone alilingania kwamba mwisho wa utumwa utakuwepo tu kupitia “ biashara na ukiristo”.  Baadae Livingstone alitumia siku nyingi tu Zanzibar ambao alipatiwa nafasi ya kutumia nyumba ya Sultani.
Hotuba zake zilipelekea kuundwa kwa ujumbe wa Vyuo Vikuu  kwa Afrika ya Kati (UMCA).  Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati ulikuwa ni mashirikiano baina ya kitivo na wanafunzi waliopitia vyuo vikuu vya Oxford and Cambridge, ambao baadae tu waliungana na mashabiki kutoka vyuo vikuu vya Durham na Dublin.  Katika mwaka 1860 walimchagua Charles Mackenzie kama ni “Askofu wa Afrika ya kati” na ilipofikia mwezi wa Oktoba wa 1860 alikuwa njiani kuelekea huko Afrika ya Kati.
Lengo la ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya kati (UMCA) lilikuwa ni kufikisha dini ya kikiristo kwa watu wengi sana waliokuwa Afrika ya Kati, kuzunguka ziwa Nyasa, ambalo Livingstone alilizungumzia kwa ufanisi.  Kwa ajili hiyo, baada ya kufika Afrika Kusini Askofu Mackenzie na wafuasi aliokuwa nao walisafiri kwa boti mpaka mto Zambezi na baadae hadi mto shire kuasisi ujumbe wa mwanzo wa ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya Kati katika Afrika katika sehemu iliyojulikana kama Magomero.
Wakati ujumbe huu na eneo lake ulichukuana na jina na ari ya jumuia mama, Ujumbe huu ulishuhudia   kushindwa kwa aina yake kutekeleza malengo yake.  Maradhi na njaa na ukame uliwakumba wamisionari wa mwanzo na kupelekea kufa kwa askofu.  Kundi hili lililazimika kuondoka katika eneo hilo ndani ya kipindi
cha miaka mitatu kwa sababu eneo hilo lilikuwepo mbali sana na upatikanaji wa bidhaa kutoka nje na vituo vya mawasiliano, eneo hilo halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya kwa wale ambao hawana uzoefu na mazoea na hali ya hewa ya hapo na pia eneo halikuwa na utulivu wa kisiasa.  Askofu mpya, George Tozer, kwanza alijaribu kuupeleka ujumbe maili 200 mafikio ya mtiririko wa mto kuelekea eneo la muanuko lakini hata hivyo eneo hilo mara tu  liligundulika kuwa halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya na kwa hiyo lilihamwa kwa miezi hivi tu.
Wakichukua bidii za makusudi, ili kutorejea makosa yaliyopita viongozi wa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) waliangalia uwezekano wa kituo au eneo jengine ambalo litatumika kuweza kufika kati kati ya Afrika.  Maeneo mbali mbali yalifikiriwa kutumika kama Kisiwa cha Johanna,  maeneo katika mwambao wa Afrika Kusini lakini kwa bahati Zanzibar ilikubalika kutumika kutokana na muundo mzuri wa njia za mawasiliano, upatikanaji mzuri wa bidhaa za chakula na wingi wa upatikanaji nguvu kazi bora.  Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) uliobakia uliwasili Zanzibar tarehe 31/08/1864.
Ujumbe huu ulipowasili ulipokewa na wamisionari wakatoliki wa Kifaransa.  Wamisionari wa kikatoliki waliwasili mwanzo Zanzibar kwa kiasi ya miaka minne kabla ya wamisionari wa kiingereza.  Katika mwezi Septemba mwaka 1860 Abbe Favat ambaye alikuwa Mfaransa mdini  maarufu mwenye nguvu alitiliana mkataba na Seyyid Said kumruhusu yeye Abbe Favat kuhamishia Makao Makuu yake katika Kisiwa cha Reunion na kuwa Zanzibar kufikia mwezi Disemba kikundi chake cha “mapadri wawili wasio watawa na watawa sita wa kike” (“Filler de Marie”) walikuwa wakiishi katika makaazi ya watawa ambayo pia yalikuwa na kanisa dogo hapo Shangani.  Jengo hili la watawa linasemekana na lilijengwa katika mwaka 1860, lakini ujenzi huu inawezekana ulikuwa ni matengenezo makubwa ya nyumba iliyokuwepo kabla.  Kanisa dogo katika jengo hili lilikuwa ni kanisa la kwanza lililojengwa Zanzibar kwa miaka 200.

Click here: Kuendelea ..........

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR