Baba
Mtakatifu Francisko amemteua Padre Joseph P. Mlola , wa Shirika la
Kazi ya Roho Mtakatifu (ALCP / OSS) kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki
Kigoma, Tanzania. Kabla ya uteuzi mpya , alikuwa ni Gombera wa Seminari
Kuu ya Mtakatifu Paulo Kipalapala, Tabora Tanzania.
Askofu Mteule
Joseph P. Mlola, ALCP / OSS, alizaliwa Januari 9, 1966 Mashati Rombo,
Moshi. Baada ya elimu ya msingi na sekondari, alijiunga na seminari
ndogo ya Uru (Moshi), na baadaye kujiunga Shirika la Utume wa Yesu
akiwa katika Seminari Kuu Kenya, ambako alichukua masomo ya falsafa.
Na alikamilisha masomo ya Teolojia katika Seminari Kuu ya Mtakatifu
Paulo Kipalapala, Tabora.
Alipokea Daraja la Upadre Julai 12, 1997,
chini ya maisha ya Jumuiya ya Mapadre wa Kazi ya Roho Mtakatifu "Opus
Spiritus Sancti - ALCP / OSS". Baada ya Upadrisho alishika nyadhifa
mbalimbali ifuatavyo :
1997-1999:Paroko Msaisizi wa Parokia ya Nairagie Enkare, Jimbo la Ngong, Kenya;
1999-2000: Makamu wa Ngombera katika nyumba ya malezi ya Roho Mtakatifu, Morogoro Tanzania
2000-2001: Paroko msaidizi Parokia ya Caliti, Avellino, Italia;
2001-2005:
Alijiunga katika masomo ya juu ya shahada ya Uzamivu (udaktari),
katika kanuni ya Teolojia, katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana.
2005-2011: Makamu Ngombera katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Charles Lwanga Segerea, Dar-es-Salaam Tanzania ;
tangu mwaka 2011 hadi uteuzi mpya, alikuwa Gombera wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo Kipalapala, Tabora Tanzania.
Jimbo
la Kigoma, liliundwa mwaka 1953,chini ya Jimbo Kuu La Tabora. LIna
eneo la kilomita mraba 45 066 kukiwa na idadi ya watu milioni 2, ambao
kati yao 515 701 ni Wakatoliki. Kuna Parokia 22, , Mapadre 55 (
Mapadre wa Jimbo wakiwa 42 na Mapadre wa Mashirika 13 ), watawa ni 65
na Waseminaristi 19.
Jimbo la Kigoma, imekuwa wazi tangu Juni 27,
2012, kufuatia Askofu wake Protase Rugambwa, kuteuliwa na Baba
Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kumteuwa kuwa Askofu mkuu, Katibu
mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu na Rais wa Mshirika
ya Kimissionari ya Kipapa mjini Roma.
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...