22
Marchi
Mwanzo
Ee Bwana Mungu wetu, tunakuomba utusaidie tuwe na mapendo kama ya mwanao, aliyeipenda dunia hata kujitoa auawe. tunaomba hayo kwa njia ya Bwana.........
SOMO 1: Yer. 31:31- 34Somo katika kitabu cha Nabii Yeremia.
Angalia siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. si kwa mfano wa agano lile nililofanya na Baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.
Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; ,maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.
WIMBO WA KATIKATI.
Zab. 19:7-10.
Kiitikio. Ee Mungu, uniumbie moyo safi..