*Liverpool waoga kichapo kwa Newcastle
Chelsea wameendeleza rekodi ya kutofungwa baada ya kuwachapa QPR 2-1,
Arsenal wakavuna pointi tatu na mabao matatu bila majibu kwa Burnley
huku Liverpool wakipoteza mechi.
Chelsea sasa wanaongoza kwa tofauti ya pointi nne, baada ya kufikisha
26 katika michezo 10, wakiwa mbele ya Southampton. Diego Costa alirejea
dimbani baada ya kukosekana katika mechi nne zilizopita, lakini
hakufunga bao.
QPR walicheza vyema na kuwabana wenyeji, kwani hadi dakika ya 74
mabao yalikuwa 1-1, Chelsea wakaja kubahatika kwa bao la penati la Eden
Hazard dakika moja baadaye na kutoka na ushindi. Bao jingine lilifungwa
na Oscar wakati la QPR lilifungwa na Charlie
Kocha Jose Mourinho amesema hakufurahia ushindi huo akisema timu yake
hawakucheza vizuri, tofauti na alivyotarajia. Kocha wa QPR, Harry
Redknapp alisononeshwa na penati iliyotolewa, akisema haikuwa haki.
Katika mechi nyingine Arsenal wamewafurahisha washabiki wao kwa
kuwatandika Burnley 3-0 kwa mabao mawili ya Alexis Sanchez ambaye kwa
msimu huu amefikisha 10 wakati furaha nyingine ilikuwa kwa beki kinda
Calum Chambers aliyefunga bao lake la kwanza tangu aanze kuchezea timu
ya wakubwa.
Theo Walcott alicheza kwa mara ya kwanza tangu alipoumia Januari,
akichukua nafasi ya Alex Oxlade-Chamberlain dakika 10 kabla ya mechi
kumalizika na Arsene Wenger anasema alivyocheza ni dhahiri atarudi
kwenye hali yake ya kawaida mapema.
Newcastle wameendelea kufufuka ambapo wamefanikiwa kuwalaza Liverpool
1-0, hali inayozidi kumfedhehesha kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers
na kumpa ahueni kubwa yule wa Magpies, Alan Pardew.
Bao pekee la mchezo lilifungwa na Perez Guiterez katika dakika ya 73,
ukiwa ni ushindi wa tatu mfululizo wakati Liverpool wamefikisha mechi
mbili bila ya kufunga hata bao moja. Watu walikuwa wakimwangalia Mario
Balotelli awe mkombozi wa Liver, lakini sasa amefikisha mechi nane
pasipo kuzifumania nyavu.
Showing posts with label Chelsea zashinda jana 1/11/2014. Show all posts
Showing posts with label Chelsea zashinda jana 1/11/2014. Show all posts
Saturday, November 1, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...