Showing posts with label Mwaka wa Imani 2012- 2013. Show all posts
Showing posts with label Mwaka wa Imani 2012- 2013. Show all posts

Monday, November 4, 2013

Kilele cha Mwaka wa Imani Kitaifa, Bagamoyo kufunika!



Maadhimisho ya Mwaka wa Imani  limekuwa ni tukio ambalo limeasidia kukuza na kuimarisha imani ya waamini kwa Kristo na Kanisa lake. Waamini katika ngazi mbali mbali wamefanya tafakari ya kina kuhusu: Fumbo la Msalaba, Sakramenti za Kanisa na umuhimu wake, Maisha ya Sala na Ushuhuda wa maisha ya Kikristo kama kielelezo makini cha imani tendaji.

Maadhimisho ya Mwaka wa Imani nchini Tanzania yanakwenda sanjari na Jubilee ya Miaka 150 ya Ukristo nchini Tanzania. Katika kipindi chote hiki Kanisa Katoliki limejikita katika Uinjilishaji unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili. Mheshimiwa Padre Patern Patrick Mangi, Katibu mtendaji Idara ya Liturujia ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania  anafafanua kuhusu mikakati ya Maaskofu Katoliki Tanzania katika kufunga Mwaka wa Imani huko Bagamoyo.

Maadhimisho haya yataanza hapo tarehe 8 Novemba 2013 na kilele cha Maadhimisho ya Kufunga Mwaka wa Imani Kitaifa ni hapo tarehe 10 Novemba 2013, ili kutoa nafasi kwa Familia ya Mungu Majimboni, kushiriki na Baba Mtakatifu Francisko katika kuufunga rasmi Mwaka wa Imani wakati wa Sherehe za Kristo Mfame wa dunia. Familia ya Mungu itapata nafasi ya kutafakari mada mbali mbali zilizoandaliwa na Maaskofu Katoliki Tanzania.

Tuesday, January 22, 2013

nembo ya mwaka wa imani





Nembo ya Mwaka wa Imani
Imeundwa kwa alama mbalimbali zinazobeba maana maalum.
A) Mashua: Hii ni ishara ya Kanisa linalosafiri.
B) Mlingoti: Huu ni Msalaba ambao juu yake kuna monogramu (chapa ya herufi zaidi ya moja zinazochanganyika pamoja, moja juu ya nyingine) IHS. Hizi ni herufi tatu za kwanza za Kigriki za jina la Yesu: I = Iota, H = eta, S = Sigma. Alama hizi zinatumika pia kuonyesha kifupisho cha jina la Yesu ambapo kwa kilatini zinatumika kusimama badala ya maneno: Iesus Hominum Salvator; yaani, Yesu Mwokozi wa Wanadamu.
C) Mduara: Nyuma ya monogramu ipo alama ya mduara ambao unaizunguka pia monogramu hiyo. Hii ni alama ya Jua ambayo inawakilisha Ekaristi Takatifu.
(Tafsiri ya maelezo, TEC, 2012)
Nembo ya Ofisi ya Vijana
Vijana wane walioshikana mikono wanasimamia vyama vya Kitume vinavyounda umoja wa Vijana. Katikati kuna alama ya kamba, chini ya neno Fidei. Kamba ni chombo cha kufunga vitu viwili au zaidi. Kamba inayoshikanisha vijana wote ni Imani. Neno Fidei ni neno la Kilatini lenye maana, “ya Imani”. Yaani, umoja huu unahusu imani.
Programu zote za Mwaka wa Imani zitakuwa na nembo hii. Pia, kauli mbiu ya mwaka huu, kwetu vijana, itakuwa pia sala, maneno ya mwinjili Luka,


“Bwana, utuongezee imani

Luka 17:5.
                                   2012—2013

Monday, January 7, 2013

MWaka WA IMANI

Tarehe 12/01/2013 Dekania Ya Gasper watakabidhiwa Msalaba wa Imani..tayari kwa kuupitisha kila Parokia...Na utaanzia kwenye Parokia ya Mwenye heri Isidori Bakanja Boko ambapo utafika siku hiyo ya Jumamosi saa nane mchana ukitokea Pugu.
 Hivyo waamini wote wa Parokia ya Boko tujitokeze kwa wingi hiyo siku kuupokea huo Msalaba ambao utapita katika Jumuiya zote na wale wenye Bibilia na Katekisimu ya Kanisa Katoliki zitabarikiwa.CLICK hapa kusoma zaidi kuhusu mwaka wa IMANI

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR