Dekania ya Mt. Gasper ni Dekania ilipo katika Jimbo kuu la Dar es salaam, inaundwa na Parokia kumi na moja ambazo ni Parokia ya Bunju, Boko Tegeta, Madale, Bahari Beach, Mtongani, St. Gasper, Maria Del Mathias, Sala sala, Mt. Dominiko, Bikira Maria Mama wa huruma, Mbezi Beach Pamoja na Parokia teule za Thomas More Mbezi Beach, Yohane Mtume, Nyaishozi Tegeta na Parokia ya Ununio tegeta.
Baada ya Baba mlezi wa vijana wa Dekania kuona mwenendo mbaya wa viongozi na kuamua kuwashirikisha Mapadre wote wa parokia za Dekani hii, kwa pamoja wameridhia kuvunja uongozi wa VIWAWA dekania, na kuitisha uchaguzi mpya ili wapatikane viongozi wapya watakao leta maendeleo kwenye dekania yetu.
Uchaguzi huo utafanyika tarehe 10/01/2015 Parokiani Bunju kuanzia saa 3:00 asubuhi, wajumbe wa uchaguzi huo ni Kamati tendaji ya VIWAWA, Parokia zote za dekania yetu.
Pia tarehe 17/01/2015 kutakuwa na Semina ya vijana wote wa Dekania itakayofanyikia Pale Parokiani St. Gasper na atakuwepo Msanii wa Nyimbo za Bongo Fleva Roma Mkatoliki.
Tuesday, January 6, 2015
IBADA YA MISA TAKATIFU YA UTOAJI DARAJA LA USHEMASI NA UPADRE LEO KANISA LA ST. JOSEPH, JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM
Mafratel waliopata Ushemasi,
Baba Askofu Kardinal Pengo atangaza Kigango cha Orongoni kuwa Parokia na kitahudumiwa na Mapadre wa Shirika la Wamisionari wa Mt. Francis wa Asizi.
Pia ametangaza Parokia Teuli ambazo zitakuwa chini ya uangalizi mpaka zitakapokuwa Parokia ambazo ni;
- Shemasi DanielMatugwa Vicent - Parokia ya Changombe
- Shemasi Meinrad Bigirwamungu - Parokia ya Mtongani
- Shemasi Raymond AlbanoMbaula - Parokia ya Kigamboni
Baba Askofu Kardinal Pengo atangaza Kigango cha Orongoni kuwa Parokia na kitahudumiwa na Mapadre wa Shirika la Wamisionari wa Mt. Francis wa Asizi.
Pia ametangaza Parokia Teuli ambazo zitakuwa chini ya uangalizi mpaka zitakapokuwa Parokia ambazo ni;
- Kigango cha Ununio kilichokuwa chini ya parokia ya Tegeta na kitakuwa kinahudumiwa na Mapadre wa Shirika la Mt. Vicent wa Mbinga.
- Kigango cha Mt. Yohane Mtume Nyaishozi kilichokuwa chini ya Parokia ya Tegeta na kitakuwa kinahudumiwa na Mapadre wamisionari wa Maria Emaculate
- Kigango cha Thomas More kilichokuwa chini ya Parokia ya Mt. Gasper kitakuwa kinahudumiwa na Mapadre wa Jimbo na Paroko atakuwa PD. Gilbert Makuru aliyekuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mikocheni
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...