Saturday, November 29, 2014

Kikao cha Bunge chavunjika, Vurugu zatawala ukumbini

Dar/Dodoma. Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana usiku kilivunjika baada ya vurugu kutawala ukumbini humo.
Vurugu hizo zilianza saa 04:42 usiku hadi saa 04:49 usiku wakati Spika Anne Makinda alipolazimika kuahirisha Bunge hadi leo saa tatu asubuhi.
Chanzo cha vurugu ni kutokana na ugumu wa kutokukubaliana na azimio la tisa, lililolenga kumwajibisha moja kwa moja Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Azimio la PAC lilitaka Waziri Muhongo aadhibiwe kwa kufukuzwa kazi kutokana na tuhuma zilizokuwa zinazomkabili ikiwamo kulidanganya Bunge.
Hata hivyo, baadhi ya wabunge wengi wakiwa wa CCM walitaka waziri huyo asiadhibiwe na Bunge bali achukuliwe hatua na mamlaka iliyomteua.
Wakati ubishani huo ukiendelea, ikiwa imefika saa 4.42 usiku Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisimama na Spika Makinda alimruhusu kuzungumza.
“Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, lakini leo (jana) kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi,” ilikuwa ni kauli ya Mbowe.
Mara baada ya kutoa kauli hiyo, wabunge wote wa upinzani walisimama na kuanza kupiga kelele kwamba wezi waondoke…tunataka fedha zirudi…tunataka fedha zirudi…vijana msilale…vijana msilale.
Wakati wabunge hao wakiendelea kuimba, wabunge wa CCM wao walikuwa wakizunguka zunguka huku wengine wakitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Hata hivyo, wabunge wa upinzani waliendelea kusimama, kuimba na kupiga makofi, huku wabunge wa CCM wakimpongeza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele kwa kuruka kihunzi alichokuwa amewekewa na kamati ya PAC.
Kutokana na hali hiyo wabunge wengine walisimama vikundi vikundi, huku Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, na Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka walikuwa wakiwasihi wabunge wa upinzani wasiondoke bungeni.
Spika Makinda alisimama na kusema, “Mheshimiwa Mbowe kuondoka mapema ni mambo ya kitoto, semeni mnataka Bunge lifanye nini.”
Hata hivyo, kauli hiyo ya Makinda haikuwafanya wabunge hao kuacha walichokuwa wakikifanya, bali walibaki ndani ya ukumbi wakiwa wamesimama hadi ilipofika Saa 04:49 usiku wakati Spika Makinda aliposimama na kusema, “Waheshimiwa wabunge naahirisha kikao cha bunge hadi pale tutakaposhauriana.”
Kuvunjika kwa kikao hicho kinaweka njia panda hatima ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ambao Bunge lilikuwa halijafikia kufanya maazimio ya hatima yao.
Hoja ya baadhi ya wabunge wa CCM walikuwa wakitaka mapendekezo yaliyotolewa na Mbunge wa Bariadi (CCM), Andrew Chenge kuhusu hatima ya Pinda na Werema yapite.
Chenge alipendekeza kuwa, “Kuhusu suala la Waziri wa Nishati na Madini lifikishwe kwa mamlaka ya uteuzi kwa hatua zaidi (wakimaanisha Rais).”
Pendekezo ambalo lilipingwa na upinzani kwa kile walichoeleza kuwa Bunge linaweza kuwawajibisha kama ambavyo limewahi fanya hivyo. Spika Makinda akijibu hoja ya Bunge kuwawajibisha alisema; “Mnajua waheshimiwa wabunge huko nyuma mawaziri walikubali wenyewe, lakini hawa wamekataa ndiyo maana tunaona haya yanatokea.”
Awali, Bunge hilo limemwachia Rais Jakaya Kikwete kufanya uamuzi wa kuwawajibisha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi baada ya kuadhimia kuwa suala lake lifikishwe kwa Rais kwa hatua zaidi.
Mjadala wa kuchukuliwa hatua kwa Maswi uliwagawa wabunge na kuwafanya kujadili kwa zaidi ya dakika 30, kufikia uamuzi huo ambao hata hivyo ulipingwa na baadhi ya wabunge.
Hata hivyo, Bunge limemwokoa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele kwa kuona kuwa kauli yake aliyoitoa haikuwa na madhara yoyote hivyo hahusiki kwa vyovyote vile kwenye sakata hilo.
Hatua ya kuwashughulikia viongozi hao na wengine kuokolewa ilifikiwa baada ya mvutano mkali wa pande mbili ndani ya Bunge katika kukubaliana na mapendekezo ya kamati ya PAC.
Baada ya muda wabunge na mawaziri walioanza kuingia kwenye magari yao na kuondoka bila kujua nini kitaendelea leo.

ujasiramali ni nini

SEMINA YA MWAKA WA FAMILIA YA FANA JANA

Vijana wa Parokia za Boko na Bunju Jana waliaanza Kongamano la Ujirani Mwema, kwa semina ya mwaka wa Familia.
Semina hiyo iliongozwa na Padre Nicolaus Ngowi, Padre ambaye ni Mlezi wa Vijana Parokia ya Boko, akieleza maandalizi ya kwa vijana kuingia kwenye sakramenti ya Ndoa, ni vizuri maandalizi yafanyike vizuri, na uamuzi wa kuoa au kuolewa si vizuri uwe kwa sababu,
ikieleza zaidi alisema Familia nyingi kwa sasa zimepoteza Tuna za kikristo, Tunajua kabisa kuwa familia ni kanisa dogo la nyumbani, lakini kwa sasa Mababa wengi hawewezi hata kuongoza sala ya asubuhi, hii ni changamoto ambayo inayowafanya vijana wengi kukosa maadili mazuri.
swala la wazazi kutokuwajibika kwa watoto wao pia inachochea anguko kubwa la maadili, wababa wamesahau majukumu yao, akiwakumbusha kuwa wao ni maparoko wa familia, hawatakiwi kulegelega.......

itaendelea

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR