Showing posts with label VIONGOZI WA VIWAWA. Show all posts
Showing posts with label VIONGOZI WA VIWAWA. Show all posts

Thursday, March 7, 2013

VIONGOZI BORA 2013

Baada ya kupatikana Viongozi wa VIWAWA ngazi ya Jumuiya ndogo ndogo na kanda, na Baadaye wakapatikana Viongozi wa Kigango cha Mbweni, Mt. Rafael na Jumapili iliyopita tukahitimisha kwa kuwapata Viongozi wa Kigango Mama cha Boko.
Hii ilikuwa ni safari ndefu yenye Maombi kwani tunaelewa viongozi Bora ndiyo dira ya vijana wetu kwa kipindi kijacho cha miaka mitatu..
Shukrani nyingi kwa Kamati tendaji za Walei Vigango vyote kwa usimamizi mzuri walioufanya, na viongozi wetu walichaguliwa kuanzia jumuiya mpaka Kigango ni jukumu lenu kuona mashirikiano kati yenu yanakuwa mazuri na tunawajenga vijana wetu katika ustawi wa kiroho na kimwili.

Jumapili hii ndiyo tunawachagua Viongozi wa Parokia ambao ndiyo kiunganishi kati yetu, ni jambo kubwa lahitaji maombi sana ili Roho Mtakatifu atuongoze kuwachagua wale ambao watakiongoza chama chetu na kutufikisha katika malengo yetu.
hili ni jukumu la viongozi wote wa Vigango na mnatakiwa kufika Parokiani Boko saa 4 asubuhi tayari kwa maandalizi ya Uchaguzi.
  
Tunawatakieni kila la kheri katika uchaguzi huo na Roho Mtakatifu awaongoze........Mapendo sana....

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR