Mwaka
wa Imani uliotangazwa na kuzinduliwa na Baba Mtakatifu mstaafu
Benedikto wa kumi na sita na kuhitimishwa kwa kishindo kikuu na Papa
Francisko, lilikuwa ni tukio la neema kubwa kwa maisha na utume wa
Kanisa. Ilikuwa ni nafasi kwa waamini kupitia tena Mafundisho ya Mababa
wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, ili kuweza kuyapyaisha katika
uhalisia wa maisha na utume wa Kanisa katika ulimwengu mamboleo.
Mwaka
wa Imani, ulikwenda sanjari na maadhimisho ya miaka 20 tangu Mtakatifu
Yohane Paulo II alipochapisha kwa mara ya kwanza Katekesi Mpya ya Kanisa
Katoliki, bila kusahau Kitabu cha Sheria za Kanisa; matunda makuu ya
Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican. Waamini kwa namna ya pekee kabisa
walihamasishwa kufanya tafakari ya kina kuhusu Imani wanayoungama katika
Fumbo la Utatu Mtakatifu, Kanisa na Mambo ya nyakati.
Waamini
walihimizwa kutambua umuhimu wa maadhimisho ya Sakramenti za Kanisa, ili
waweze kushiriki kikamilifu na hatimaye kujipatia neema na baraka
zinazotolewa na Mama Kanisa. Mwaka wa imani, ulikuwa ni nafasi kwa
waamini kujikita katika ushuhuda unaoonesha imani tendaji kwa kukumbatia
Amri za Mungu kama dira na mwongozo wa maisha yao ya kiroho na maisha
ya hadhara.
Waamini kwa mara nyingine tena, walihimizwa na Mama
Kanisa kumwilisha imani yao kwa Kristo na Kanisa lake kwa njia ya Sala
na Matendo ya huruma. Kwa maneno machache, Mwaka wa Imani, ilikuwa ni
fursa ya kutafakari kwa kina na mapana kuhusu: Imani, Sakramenti za
Kanisa, Amri za Mungu na Maisha ya Sala. Mwaka wa Imani, kimekuwa ni
kipindi cha neema ambacho kimeyasaidia Makanisa mahalia kujiwekea mbinu
mkakati wa kuimarisha imani kwa njia ya Sinodi za Majimbo au Mwendelezo
wa Maadhimosho ya Mwaka wa Imani kwa kuchagua mada mbali mbali kadiri ya
mahitaji ya Kanisa mahalia.
Askofu Salutaris Melchior Libena wa
Jimbo Katoliki la Ifarakara, Tanzania, katika mahojiano maalum na
Gazeti la AMECEA anasema kwamba, mara baada ya kuadhimisha Mwaka wa
Imani, kulionekana kwamba, kunahitaji la kuendelea kuwaimarisha waamini
katika Mafundisho tanzu ya Kanisa kwa kujikita hasa zaidi katika
Katekesi ya kina, zoezi la kiroho linaloigusa Familia ya Mungu Jimboni
Ifakara.
Kutokana na hitaji hili msingi, Jimbo Katoliki la
Ifakara hapo tarehe 19 Marchi 2013, katika Maadhimisho ya Siku kuu ya
Mtakatifu Yosefu mchumba wake Bikira Maria na Msimamizi wa Kanisa la
Kiulimwengu, Askofu Libena akazindua Mwaka wa Katekesi Jimbo Katoliki
Ifarakara, utakaofungwa rasmi hapo tarehe 19 Marchi 2015, Jimbo Katoliki
Ifakara litakapokuwa linaadhimisha Mwaka wa Tatu tangu kuundwa kwake na
Baba Mtkatifu mstaafu Benedikto XVI. Ifakara ni kati ya majimbo
machanga sana nchini Tanzania, lakini linaendelea kucharuka kwa
maendeleo ya watu kiroho na kimwili.
Askofu Libena anasema,
Mwaka wa Katekesi umekuwa ni fursa kubwa kwa Familia ya Mungu Jimboni
Ifakara kuweza kupyaisha tena mafundisho tangu ya Kanisa, dhamana
inayotekelezwa kuanzia kwenye ngazi ya: Familia, Jumuiya ndogo ndogo za
Kikristo, Vigango, Parokia na katika ngazi ya Jimbo. Lengo ni
kuhakikisha kwamba, Jimbo Katoliki Ifakara litakapokuwa linaadhimisha
kumbu kumbu ya miaka mitatu tangu kuundwa kwake, waamini wawe
wameifahamu Katekesi kwa kina na mapana yake.
Jimbo Katoliki
Ifakara linapenda kumwilisha imani katika matendo kwa kuwekeza zaidi
katika sekta ya elimu ambayo kwa sasa inaonekana inahitaji kupewa uzito
wa pekee kutokana na ukweli kwamba, kwa masuala ya afya, Jimbo
limejiimarisha kwani kuna Hospitali ya Rufaa yenye vitanda 370 na idadi
nzuri ya Zahanati ambazo zinaendelea kutoa huduma bora kwa kuzingatia
utu na heshima ya binadamu.
Jimbo Katoliki la Ifakara linamiliki
na kuendesha shule kadhaa za msingi, lakini kwa bahati mbaya, linamiliki
Sekondari moja tu, changamoto ya kuendelea kuwekeza katika elimu, ili
kuweza kuwafunda vijana wa kizazi kipya: kiroho na kimwili, tayari
kulitumikia Taifa na Kanisa kwa ujumla.
Itakumbukwa kwamba, Jimbo
Katoliki la Ifakara liliundwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI
kunako tarehe 14 Januari 2012 na kuzinduliwa rasmi tarehe 19 Marchi 2012
na Askofu Salutarius Libena akawa ni Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki
Ifakara:>>>>>bonyeza hapa soma zaidi hapa
Showing posts with label Mwaka wa Katekesi Jimbo Katoliki Ifakara. Show all posts
Showing posts with label Mwaka wa Katekesi Jimbo Katoliki Ifakara. Show all posts
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...