Jimbo
Katoliki la Mahenge, Tanzania, linaadhimisha kilele cha Jubilee ya
miaka 50 tangu lilipoanzishwa kunako mwaka 1964 na Marehemu Askofu Elias
Mchonde aliyekuwa Askofu msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam akateuliwa
kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Mahenge na kuliongoza Jimbo
hili kuanzia wakati huo hadi mwaka 1969 alipofariki dunia. Baadaye Jimbo
limeongozwa na Askofu Nikas Kipengele tangu mwaka 1970 hadi mwaka 1971;
Askofu Patrick Iteka kuanzia mwaka 1973 hadi mwaka 1993.
Askofu
Agapiti Ndorobo akapewa dhamana ya kuwaongoza waamini wa Jimbo Katoliki
la Mahenge tangu mwaka 1995 hadi wakati huu, Jimbo linapomwimbie
Mwenyezi Mungu utenzi wa shukrani na sifa kwa kuadhimisha Jubilee ya
Miaka 50 ya uwepo wake. Askofu Ndorobo ameliongoza Jimbo kwa miaka 19
sasa. Katika mahojiano maalum na Radio Vatican anabainisha: mafanikio na
changamoto anazokabiliana nazo katika kuwaongoza, kuwafundisha na
kuwatakatifuza Watu wa Mungu Jimboni Mahenge.Itakumbukwa kwamba,
Jimbo Katoliki la Ifakara lililoanzishwa na Baba Mtakatifu mstaafu
Benedikto XVI kunako mwaka 2012 na Askofu Salutaris Melchior Libena
kuteuliwa akuwa Askofu wake wa kwanza ni matunda ya Jimbo Katoliki la
Mahenge ambalo hapo awali lilikuwa na Parokia 38 lakini baada ya
kuligawa ili kurahisisha shughuli za kichungaji kwa Watu wa Mungu, sasa
Jimbo Katoliki la Mahenge lina Parokia 22, likiwa na waamini zaidi ya
215, 000 lakini hapo awali lilikuwa na waamini 487, 000.
Askofu
Ndorobo anasema kwamba, katika kipindi cha miaka 50 ya uwepo wa Jimbo
Katoliki la Mahenge kumekuwepo na maendeleo makubwa katika medani mbali
mbali za maisha, lakini zaidi ni upendeleo kwa maskini na wale
wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii. Kuna vituo vya kutunzia wagonjwa wa
kifafa, kituo cha wagonjwa wa Ukoma pamoja na kituo cha Watoto Yatima.
Jimbo
Katoliki la Mahenge linamiliki na kuendesha Sekondari 5; Vituo vya Afya
na Zahanati 9 na kwamba kuna mpango mkakati wa kuanzisha Hospitali ili
kujibu kilio cha watu wenye shida na mahangaiko wanaolazimika kutembea
umbali mrefu ili kutafuta tiba kwa magonjwa yanayowasumbua, lengo ni
kuendelea kutangaza Injili ya Uhai, kwa kutoa kipaumbele cha kwanza kwa
binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.
Askofu Ndorobo
anakiri kwamba, Jimbo la Mahenge limeendelea kuwa na miito mbali mbali
ya maisha ya: Kipadre, Kitawa na Ndoa. Kuna vyama vya miito
vinavyosaidia mchakato wa malezi ya miito ndani ya Kanisa, kwa njia ya
ushuhuda wenye mvuto na mashiko, unaowachangamotisha vijana kupenda
kushiriki katika maisha ya Kipadre, Kitawa na Ndoa takatifu.
Askofu
Ndorobo anasema miaka 19 ya utume wake kama Askofu wa Jimbo Katoliki
Mahenge amekumbana na changamoto nyingi, lakini katika mahojiano na
Radio Vatican anagusia changamoto kuu mbili, yaani umuhimu wa Jumuiya
Ndogo ndogo za Kikristo na Maisha ya Sala na Kisakramenti. Anasema, kwa
miaka hii yote amependa kukazia umuhimu wa waamini kushiriki katika
maisha ya Jumuiya ndogo ndogo za Kikristo kwani hizi ni shule ya Sala,
Neno la Mungu na kielelezo cha imani tendaji.
Huu ndio mwelekeo
ambao anapenda kuuendeleza hata baada ya maadhimisho ya Jubilee ya Miaka
50 ya Jimbo Katoliki Mahenge. Anasema, amependa kukazia umuhimu wa
waamini kushiriki kikamilifu katika maisha ya Sala na Sakramenti za
Kanisa ili waweze kujichotea neema na baraka; waweze kuonja huruma na
upendo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, tayari kufanya mabadiliko ya kina
katika maisha yao, kwa ajili ya sifa na utukufu wa Mungu. Viongozi wawe
ni mfano bora wa maisha ya sala na Sakramenti za Kanisa, ili wao
wakiishaimarika, waweze pia kuwaimarisha ndugu zao katika imani,
matumaini na mapendo.
Showing posts with label Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Jimbo Katoliki Mahenge.. Show all posts
Showing posts with label Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Jimbo Katoliki Mahenge.. Show all posts
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya...
-
Isidore Bakanja, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya imani ya Kikristo, Akiongozwa na maisha rahisi kama layman Katoliki wakati wa mauaj...
-
Mwandishi wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambamo tunapata somo la kwanza anatualika kutambua kuwa Mungu haachi kutimiza ahadi yake ya ...