Showing posts with label masomo ya jumapili ya 3 ya mwaka B wa kanisa tarehe 25/01/2015. Show all posts
Showing posts with label masomo ya jumapili ya 3 ya mwaka B wa kanisa tarehe 25/01/2015. Show all posts

Saturday, January 24, 2015

MASOMO YA TAREHE 25/01/2015 jumapili ya 3 ya mwaka B wa kanisa

25

Januari

 Jumapili: Dominika ya 3 ya Mwaka "B".
SOMO  1. Yon. 3:1-5, 10

 Neno la bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema, ondoka uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukaihubiri habari nitakayo kuamuru. Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikua mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu, Yona akaanza kuingia mjini mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR