1800 – 1900
WAKATOLIKI, MAKUNDI YA WAKIRISTO WASIOPENDA MIKUTANO ASMI, VITA AU GHASIA (QUAKERS) NA UJUMBE WA VYUO VIKUU KWA AFRIKA YA KATI ( UMCA)
Baada ya Wareno kurudi nyuma Wakiristo kidogo tu Wakigoa
ndio waliobakia Zanzibar.
Wakiristo
hawa hawakuwa na kanisa la kufanyia Ibada lakini waliweza kuifanya hai jumuia
yao kwa kwa kuifanya ibada zao kibinafsi. Baadae katika miaka 1800 makundi ya
watu wa wamagharibi yalianza kujumuisha wamisionari na wachungaji wamisionari
waliokuwa wakipita pita mara chache na wachungaji katika meli bandarini. Katika
mwaka 1844 wamisionari wa kikiristo zaidi wa kudumu waliwasili Afrika mashariki
kwa kupitia mchungaji wa kilutheri Joseph Krapf na wafuasi wawili ambao
walifanya kazi kwa ajili wa Jumuia ya kimisheni ya kanisa la kiingereza (English
Church Missionary Society). Wakifanyakazi, Mombasa, walitembelea Zanzibar na
miaka michache mbeleni walitoa kamusi bora kabisa la Kiswahili lakini hawakuwahi
kuanzisha kanisa ndani ya visiwa hivyi.
Ukuwaji
wa harakati dhidi ya utumwa ndani ya Uingereza ulishajiisha raghba ya
wamisionari wakiristo, ikikuzwa na hotuba ya David Livingstone aliyoitoa mwaka
1857 akiomba Uingereza kupeleka wamisionari na wafanyakazi Afrika. David
Livingstone alilingania kwamba mwisho wa utumwa utakuwepo tu kupitia “ biashara
na ukiristo”. Baadae Livingstone alitumia siku nyingi tu Zanzibar ambao
alipatiwa nafasi ya kutumia nyumba ya Sultani.
Hotuba zake zilipelekea kuundwa kwa ujumbe wa Vyuo Vikuu
kwa Afrika ya Kati (UMCA). Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati ulikuwa ni
mashirikiano baina ya kitivo na wanafunzi waliopitia vyuo vikuu vya Oxford and
Cambridge, ambao baadae tu waliungana na mashabiki kutoka vyuo vikuu vya Durham
na Dublin. Katika mwaka 1860 walimchagua Charles Mackenzie kama ni “Askofu wa
Afrika ya kati” na ilipofikia mwezi wa Oktoba wa 1860 alikuwa njiani kuelekea
huko Afrika ya Kati.
Lengo la ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya kati (UMCA)
lilikuwa ni kufikisha dini ya kikiristo kwa watu wengi sana waliokuwa Afrika ya
Kati, kuzunguka ziwa Nyasa, ambalo Livingstone alilizungumzia kwa ufanisi. Kwa
ajili hiyo, baada ya kufika Afrika Kusini Askofu Mackenzie na wafuasi aliokuwa
nao walisafiri kwa boti mpaka mto Zambezi na baadae hadi mto shire kuasisi
ujumbe wa mwanzo wa ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya Kati katika Afrika katika
sehemu iliyojulikana kama Magomero.
Wakati ujumbe huu na eneo lake ulichukuana na jina na ari
ya jumuia mama, Ujumbe huu ulishuhudia kushindwa kwa aina yake kutekeleza
malengo yake. Maradhi na njaa na ukame uliwakumba wamisionari wa mwanzo na
kupelekea kufa kwa askofu. Kundi hili lililazimika kuondoka katika eneo hilo
ndani ya kipindi
cha miaka mitatu kwa sababu eneo hilo lilikuwepo mbali sana
na upatikanaji wa bidhaa kutoka nje na vituo vya mawasiliano, eneo hilo halikuwa
na mazingira mazuri ya kiafya kwa wale ambao hawana uzoefu na mazoea na hali ya
hewa ya hapo na pia eneo halikuwa na utulivu wa kisiasa. Askofu mpya, George
Tozer, kwanza alijaribu kuupeleka ujumbe maili 200 mafikio ya mtiririko wa mto
kuelekea eneo la muanuko lakini hata hivyo eneo hilo mara tu liligundulika kuwa
halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya na kwa hiyo lilihamwa kwa miezi hivi tu.
Wakichukua bidii za makusudi, ili kutorejea makosa
yaliyopita viongozi wa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA)
waliangalia uwezekano wa kituo au eneo jengine ambalo litatumika kuweza kufika
kati kati ya Afrika. Maeneo mbali mbali yalifikiriwa kutumika kama Kisiwa cha
Johanna, maeneo katika mwambao wa Afrika Kusini lakini kwa bahati Zanzibar
ilikubalika kutumika kutokana na muundo mzuri wa njia za mawasiliano,
upatikanaji mzuri wa bidhaa za chakula na wingi wa upatikanaji nguvu kazi bora.
Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) uliobakia uliwasili Zanzibar
tarehe 31/08/1864.
Ruhusa iliyotolewa na Sultan Majid kwa Wafaransa hawa
kuanzisha duka ndani ya Zanzibar ilitafsiriwa kama ni juhudi za Sultani za
kuweka “ uwiano wa nafasi kubwa waliokuwa nao Waingereza Zanzibar kwa
kuwakaribisha wapinzani wao wakuu wa kizungu.” Ikiwa ushindani wa kisiasa ndio
uliompelekea Sultan Majid za kukaribisha pamoja matawi tofauti ya wamisionari
wakiristo hata hivyo matokeo hayakuwa hayo kwani kwa upande wa wamisionari hawa
hakukuwa na msuguano wowote. Mahusiano yao mazuri makundi hayo mawili ya
wamisionari ulitokana na ukweli kwamba Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati
wa kianglikana (UMCA Anglicans) ulikuwa ni ujumbe wa watu watukufu ambao wenye
mafunzo ya kikatoliki ya kiengereza (Anglon Catholic Learnings)
Wamisionari
wakifaransa walikuwa makini kuepuka matatizo yoyote Zanzibar “kwa kutambua
uhalisia wa maisha ulivyo ndani ya nchi ya kiislamu ya Zanzibar, Wafaransa
kuanzia 1862 wafuasi wa Holy Ghost Order, waliamua kujikita katika maeneo maalum
kama ya elimu, shughuli za uchungaji kwa jumuia ndogo ya mjini ya magoa
wakatoliki na huduma za afifu na walifungua hospitali ya mwanzo iliyopendekezwa
na Sultani ya kizungu. Kwa hili waliojenga maoni mazuri kwa warabu.
Juu ya ukarimu wa watu wa Zanzibar, Wazanzibar hawa kidogo
hawakuwa na azma yoyote kufuata imani ya wageni hawa wapya. Wamisionari wa
kikatoliki walilielewa hili lakini waliamini
kwamba
kundi kubwa la wafuasi wapya wa dini hii ya kikiristo litaweza kupatikana masafa
machache kuvuka mlango bahari wa Zanzibar huko Tanzania Bara.
Walipeleka ujumbe mdogo Bagamoyo katika mwambao wa Tanzania Bara katika mwaka
1868 na kwa sehemu kubwa walitumia nafasi walizonazo Zanzibar kama ni makao
makuu ya kuzidisha harakati zao Tanzania Bara. Harakati hizi ikiwemo ujenzi wa
“ Hospitali ya Kifaransa” ndani ya Bagamoyo.
“ Hospitali ya Kifaransa” ndani ya Zanzibar ilijengwa
mkabala na jengo la watawa. Hospitali ilimalizwa kujengwa na kuanza kazi
kufikia mwaka 1890. Kipindi hicho wakatoliki walien delea kutumia uhusiano
mzuri na majirani zao wa Zanzibar, wakipata ruhusa ya kujenga kanisa la
mtakatifu Joseph katika mwaka 1894. (Cathedral of Saint Joseph in 1894). Jiwe
la msingi la kanisa
hili kuu liliekwa tarehe 10 Julai 1896. Misa ya mwanzo katika kanisa hili kuu
jipya iliendeshwa na Askofu Allegeyer katika usiku wa krismas 1898.
Kadri
ya wakati ulivyokuwa ukienda, hospitali hii ya Zanzibar ilipungua umuhimu wake
na jengo hilo likafanywa kuwa ni skuli. Hii ilikuwa ni skuli ya kitawa ya
mtakatifu Joseph (St. Joseph Convent School).
Wamisionari wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati
(UMCA) hawakuzubaa katika kipindi hichi. Akianzia kwanza kuishi katika nyumba
Mambo Msiige, katika eneo la Shangani, ambapo haikuwa mbali na ujumbe wa
Kifaransa, Muingereza mchapa kazi shupavu alianzisha ustawi wa majengo
ya ukubwa wa kuvutia na ya aina tofauti. Kwanza walinunua sehemu ya ardhi ya
kilimo Kiungani pembezoni mwa mji wa Zanzibar Kaskazini. Ujenzi wa “bweni kwa
ajili ya vijana watumwa walioachiwa huru” uliendelea katika eneo hilo kufikia
mwaka 1866. Karibu ya hapo mava sehemu ya kuzikia ilianzishwa, na hadi leo mava
hii inayo baadhi ya mabaki ya wakiristo wa mwanzo wa Zanzibar.
Baadae ilinunuliwa ardhi nyengine katika mwaka 1873, ardhi
hii ilikuwa karibu na kitovu cha mji ambalo ni jengo kubwa zima la mjini ambalo
liliwahi kuwa uwanja wa soko kongwe, ambapo watumwa walikuwa wakiuzwa, Mara
wito ulitolewa wa fedha kusaidia ujenzi wa kanisa katika eneo hilo ambao uovu
huo wa biashara ya utumwa ulifanyika. Huu ulikuwa mwanzo kanisa kuu la kristo
(Christ Church Cathedral).
Mwaka uliofuata Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati
(UMCA) walinunua ardhi ya kilimo Mbweni kusini mwa mji karibu na bahari.
Jiwe la msingi la kanisa kuu la ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa
Afrika ya Kati (UMCA Cathedral)
liliekwa
mwaka 1873 katika siku ya siku kuu ya krismas katika eneo la mjini. Uwanja wa
soko kongwe ulianza kujazwa majengo ya ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati.
“Jumba la Mkunazini” lilijengwa katika mwaka 1875 na kanisa
mara baada ya kujengwa jumba la kunazini lilihamisha makao makuu yake kutoka
Mambo Msiige na kuwa Mkunazini. Zahanati
ilijengwa
katika mwaka 1877, hatimae iligeuzwa kuwa hospitali yenye kutoa huduma kamili
katika mwaka 1893. Skuli ya Mtakatifu Mon`ica, nyumba ya kasisi mkuu na Askofu
ilijengwa katika uwanja wa soko kongwe. Jengo hilo la skuli ya Mtakatifu Monica
bado mpaka leo linatumika kama ni hostel/dahalia Mtukufu Monica.
Mwenye kustahiki sifa ya mafanikio haya ilikuwa hakika ni
kanisa kuu la kristo. Mradi usio wa kibiashara ambao ulisimamiwa binafsi na
Askofu wa tatu wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati Edward Steere,
utabakia kuwa moja ya mifano ya kuvutia na bora wa usanifu majengo ndani ya
Afrika uliofanywa na wakiristo wa mwanzo.
Theodore Buft aliamini kwamba biashara na ukiristo ilikuwa
ndio njia ya uongofu na kuweza kuweza kuelimika.
Watumwa na Waliobadili Dini
Lakini juu ya hivyo, wingi wa wakiristo hawa wapya na
mahitaji yao maku bwa yalikuwa ni changamoto kwa raslimali na subira ya
wafadhili wao. Wakiangalia demografia wamisionari waliona njia pekee ya
kuwahudumikia wakiristo wapya ni kuanzisha chimbuko la Padri wa kiafrika.
Kwa hivyo wote wakatoliki na waprotestanti walifanya bidii
kuwajumuisha makundi ya kienyeji shughuli na mambo ya kanisa na hii yote
ilipelekea kujua na kufunza mtumishi bora kwa ajili ya kuendesha shughuli za
kidini.
Kwa Zanzibar harakati zote hizi zilikuwa katika eneo la
Kiungani ambapo kwanza ilianzishwa “dahalia kwa watumwa vijana walioachiwa huru”,
na baadae “Chuo cha Mafunzo ya ualimu cha Mtakatifu Andrew” na baadae “Chuo cha
kidini/theolojia” kila moja kati ya hivyo kilijaribu kuwafunza na kutathmini
matokeo ya vijana wa kiafrika. Kiasi cha wanafunzi 50 kwa kipindi kimoja cha
wakati waliishi na kusoma Kiungani. Mitaala ilisisitiza heshima, elimu, imani
na michezo. Wanafunzi wazuri walifanywa kuwa walimu na wanafunzi bora kuliko
wote walifanywa kuwa mapadri.
Serikali ya Zanzibar ilitoa stempu mwaka 1963 kuadhimisha
historia ndefu ya uvumilivu wa kidini Zanzibar.
Picha hizi za Stempu, kutoka kushoto kwenda kulia,
Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Kanisa Kuu la Kristo,
Msikiti wa Malindi, Msikiti wa Hujjatul Islam,
Hekalu la Kihindi.