Showing posts with label MASOMO YA HUNI 15 SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU MWAKA A. Show all posts
Showing posts with label MASOMO YA HUNI 15 SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU MWAKA A. Show all posts

Friday, June 20, 2014

MAOMO YA YA JUNE 15 SHEREHE YA PENTEKOSTE MWAKA A



15
   JUNI 
 SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU
 MWAKA "A" 2014


RATIBA ZA IBADA
KIGANGO CHA BOKO.
IBADA YA MISA YA KWANZA 12:15 – 1:45 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 2:00 – 3:50 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA TATU SAA 4:00-5:20 ASUBUHI
KIGANGO CHA MBWENI.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:15 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA MT. RAFAEL.
IBADA YA MISA YA KWANZA 1:00 – 2:55 ASUBUHI
IBADA YA MISA YA PILI 3:00 – 4:50 ASUBUHI
KIGANGO CHA ANTHONY WA PADUA – MBWENI MPIJI.
IBADA YA MISA NI 3:00 – 5:00ASUBUHI


Zaburi:Tazama sala ya siku.

Dan.3:52-56
K. Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.

SOMO 1:Kut.34:4b-6, 8-9
  Musa aliinuka asubuhi na mapema, naye akakwea katika mlima wa Sinai, kama Bwana alivyomwamuru, akazichukua hizo mbao mbili za mawe mkononi mwake. Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana. Bwana akapita mbele yake, akalitangaza, Bwana , Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu. Akasema ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.

SOMO 2:2Kor.13:11-14
Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, make katika Amani; na Mungu wa upendo na Amani atakuwa pamoja nanyi. Salimianeni kwa busu takatifu. Watakatifu wote wawasalimu. Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu. Na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.

INJILI:Yn.3:16-18
Yesu alimwambia Nikodemu: kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanae wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la mwana pekee wa Mungu.

 

 MATANGAZO

mara baada ya misa ya pili saa 4:00 asubuhi, Parokiani Boko, Tutakuwa na kikao cha VIjana waote wanaotarajia kushiriki ziara ya uinjilishaji Jimbo la Mbulu Parokia za Dareda, Sanu, Daudi na endabashi, pia kwenda kutembelea mbuga ya Wanyama ya ngorongoro.

Fika na mchango wako ikiwa bado haujamalizia mchango ni tshs 150,000 kwa mshiriki, ziara ni tarehe 01/07 mpaka tarehe 07/07/2014....

Tunawatikia Dominika njema, Amani ya Bwana Iwe nasi.........Mapendo sana,,,,,,, 

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR