Showing posts with label ZIARA YA MBULU. Show all posts
Showing posts with label ZIARA YA MBULU. Show all posts

Friday, June 21, 2013

ziara ya Mbulu tarehe 26June13

Tumsifu Yesu Kristo,
YAH:SAFARI YA ZIARA YA UINJILISHAJI PAROKIA YA DAUDI JIMBO LA MBULU MKOANI MANYARA.
Husika na kichwa cha habari hapo juu, siku ya jumatano tarehe 26/06/2013, VIWAWA wataanza safari ya kuelekea Jimbo la Mbulu Mkoani Manyara.
Kwanza tunatoa shukrani kwa Wazazi, Walezi, Viongozi wa JNNK kwa ushirikiano mkubwa waliotupatia kwa kuwachangia Vijana na kuwaruhusu kushiriki katika ziara hii.
Safari itaanzia Parokiani Boko saa kumi na moja asubuhi, na tunatarajia kwenda kupumzika katika mji wa Karatu Mkoani Arusha, Siku ya Alhamisi tarehe 27/06/13 tutaenda Ngorongoro na mchana tutafanya ziara katika Parokia ya Endabashi, Jioni tutaenda Parokia ya Mt. Francisco wa Asizi –Kijiji cha Daudi hapo tutakaa mpaka tarehe 29/06/2013. Jumapili Tarehe 30/06/2013 tutaenda Parokia ya Mt. Yosefu Mfanyakazi(JIMBONI), na kushiriki Ibada ya Misa Takatifu na baadaye kukutana na Vijana wenzetu. Jioni tutaanza safari na tutapumzika Karatu na tarehe 01/-7/2013, saa kumi na moja asubuhi tutaanza safari ya kurudi Dar es salaam.
Tuzidi kuombeana katika kufanikisha ziara hii ya kitume. Tunamwomba Mungu aongoze safari yetu, malaika mikaeli mlinzi wa safari atuongoze.
Mapendo..................................................

Tuesday, February 26, 2013

HISTORIA YA UJENZI WA KANISA LA MBULU

Shujaa wetu: Franz Wesinger-Mhandisi aliyejenga kanisa Katoliki Mbulu

  Kanisa la Mbulu ndilo kanisa kubwa kuliko yote Tanzania na la pili kwa ukubwa Afrika Mashariki kanisa hili lilijengwa na   Mhandisi Franz Wesinger aliyezaliwa mwaka 1928 huko Bavaria Ujerumani.
Mwaka 2003, akiwa na miaka 75 mhandisi Franz Wesinger ambaye pia ni msanifu wa majengo alirudi Tanzania kwa ajili ya kupanga ujenzi wa kanisa jipya la Katoliki Arusha na ni katika kipindi hicho ambacho mapadre wawili wa kanisa Katoliki jimbo la Mbulu walikumbwa na kashfa ya ufisadi kama baada ya kufuja jumla ya Shilingi za Kitanzania Milioni 340 kwa bei ya 1000 kubadili dola moja wakati huo  (dola 340,000). Mapadre hao, msaidizi wa askofu (Vicar General) John Nada na father Melkiadus Qameyu wa parokia ya Dareda walituhumiwa kupoteza kiasi hicho cha fedha baada ya kutapeliwa na mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la Mohamed mrisho kuwa angeziongeza mara mbili....mafaza wakaingia mkenge...
Turudi kwa Franz Wesinger, huyu bwana alifanya mahojiano na gazeti la Arusha Times mwaka 2003 na haya ni sehemu ya maelezo yake kuhusu ujenzi wa Kanisa hilo
"Katika miaka 15 iliyopita, Jimbo la Mbulu limepiga hatua kubwa sana. Jitihada za awali za marehemu Askofu Hhando zimezaa matunda kwani walianza kidogo au kusema ukweli halisia walianza bila fedha lakini waliweka imani yao kwa Mungu huku wakitumia msaada kidogo kutoka kwa wamihionari kutoka Ulaya na ujenzi ulianza. Amini usiamini, walianza ujenzi wakitumia sepetu lililovunjika na toroli la mbao. Kanuni kuu ilikuwa kubana matumizi na kuhudumu (huduma) pamoja kukawa kichocheo kikubwa katika jimbo zima kumtumikia Mungu" alisema Franz
"Hata baada ya ujenzi na kanisa kuwekwa wakfu zilibaki kontena 12 zikiwa zimejaa vifaa vya ujenzi, mashine, magenerata, jukwaa kubwa, magari mawili na lifti (cranes) bila kutumika"
"Kuna tofauti kati kuhudumu kwa imani na kutumaini kupata faida pasipo kufanya kazi" aliongeza Franz akizungumzia ufisadi uliotokea Mwaka moja baada ya ujenzi wa kanisa hilo kukamilika.
"Hata wana wa Israeli walimsahau Mungu na kuabudu ndama wa dhahabu baada ya Mungu kuwatoa utumwani mwa Wamisri na kuwapitisha katika bahari ya Shamu"
"Waisraeli walikombolewa lakini walitaka kupata faida pasipo kufanya kazi, hauwezi kumtumikia Mungu kwa ulanguzi"
Franz Wesinger alieleza kuwa anajisikia fahari kubwa sana moja ya sehemu maskini zaidi Tanzania ina Kanisa kubwa zaidi na zuri zaidi nchini na kuona fahari kuwa imejenga hilo kanisa lenyewe kwa msaada pekee wa Mungu"
Chini ya usimamizi wa Franz Wesinger ujenzi wa kanisa hili ambalo leo ni fahari kubwa kwetu ulikamilika kwa ufanisi wa hali ya juu na kutimiza ndoto ya aliyekuwa Askofu wa Jimbo Kuu la Mbulu Marehemu Hhando. Franz Wesinger anatoa funzo la uaminifu na kuacha "legacy" kwa vizazi vijavyo. Sina uhakika kama bado yupo hai lakini Franz Wesinger alifanya kazi kubwa sana tofauti na "wahandisi" wetu ambao ninauhakika kisingebaki kitu baada ya ujenzi na katu kazi ya ujenzi wa kanisa hilo usingekamilika.
 

Monday, February 25, 2013

YA KWETU TENA 2013

Ule mchakato wa Ziara katika Jimbo la Mbulu na kutembelea Mbuga ya Ngorongoro umekamilika, sasa kazi ni kwako kijana kuanza kufanya Maandalizi ya Ushiriki wako..ni nafasi ya pekee sana kwetu...

Tarehe 26-30/06/13..Vijana wa Parokia ya Boko tutafanya ziara ya kuinjilishi katika Parokia ya Daudi iliyopo Jimbo la Mbulu Mkoani Manyara......ikiwa ni pamoja na kutembelea Kanisa kuu la Jimbo la Mbulu ambalo ndilo kanisa Katoliki kubwa kuliko yote hapa Tanzania na la tatu kwa ukubwa Barani Afrika.
Pia tutatembelea mbuga ya wanyama ya Ngorongoro na kujionea mengi
WANYAMA WAKIWA WAMEPUMZIKA KANDO YA ZIWA HUKO NGOROGORO  

Kwa mchango wa Tshs 150,000/= tu wahi sasa kujiandikisha nafasi ni kwa vijana 60 tu........wasiliana na uongozi wa vijana mahali ulipo au waone viongozi wa Jumuiya yako.

Sunday, February 24, 2013

Jimbo Katoliki la Mbulu

Jimbo katoliki la Mbulu (kwa Kilatini Dioecesis Mbuluensis) ni mojawapo kati ya majimbo 33 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.

Kikanisa linahusiana na jimbo kuu la Arusha.
Askofu wake ni Beatus Kinyaiya.

Historia

  • 1943: Kuanzishwa kwa Apostolic Prefecture ya Mbulu kutokana na Apostolic Vicariate ya Dar-es-Salaam
  • 1952: Kupandishwa cheo kuwa Apostolic Vicariate ya Mbulu
  • 25 Machi 1953: Kufanywa dayosisi

Uongozi

  • Maaskofu wa Mbulu
    • Beatus Kinyaiya (since 2005)
    • Juda Thadaeus Ruwa’ichi OFMCap (1999 – 2005)
    • Nicodemus Atle Basili Hhando (1971 – 1997)
    • Patrick Winters SAC (1953 – 1971)
  • Vicar Apostolic wa Mbulu
    • Patrick Winters SAC (1952 – 1953)
  • Prefect Apostolic wa Mbulu
    • Patrick Winters SAC (1944 – 1952)

Takwimu

Eneo ni la kilometa mraba 16,057, ambapo kati ya wakazi 995,000 (2006) Wakatoliki ni 269,620 (27.1%).

MALENGO YA ZIARA YA MBULU

Lengo kubwa la ziara hii ni kwaona Vijana wenzetu na kushirikiana nao jinsi ya kueneza Injili  pia kujenga mashirikiano katika maswala ya kiuchumi na maendeleo kwa ujumla pia tutapata nafasi ya kujifunza tamaduni mpya kutoka katika makabila mbali mbali yalipo huko

Zaidi tutafika katika kanisa Kuu la Jimbo la Mbulu na kujionea ukubwa wake ambapo ndilo kanisa kubwa kuliko yote hapa Africa Mashariki.

mwisho tutaenda Mbuga ya wanyama ya Ngorongoro kuona uzuri wa nchi Yetu na Maajabu ya Mungu.

 KUWA TAYARI NA ANZA MAANDALIZI SASA KWA KUJAZA FORM NA KUWAKILISHA FEDHA YAKO NAFASI NI KWA VIJANA 60 TU.

Thursday, February 21, 2013

SAFARI YA NGORONGORO NA JIMBO LA MBULU

 Ule mchakato wa Ziara katika Jimbo la Mbulu na kutembelea Mbuga ya Ngorongoro umekamilika, sasa kazi ni kwako kijana kuanza kufanya Maandalizi ya Ushiriki wako..ni nafasi ya pekee sana kwetu...

Tarehe 26-30/06/13..Vijana wa Parokia ya Boko tutafanya ziara ya kuinjilishi katika Parokia ya Daudi iliyopo Jimbo la Mbulu Mkoani Manyara......ikiwa ni pamoja na kutembelea Kanisa kuu la Jimbo la Mbulu ambalo ndilo kanisa Katoliki kubwa kuliko yote hapa Tanzania na la tatu kwa ukubwa Barani Afrika.
Pia tutatembelea mbuga ya wanyama ya Ngorongoro na kujionea mengi

Kwa mchango wa Tshs 150,000/= tu wahi sasa kujiandikisha nafasi ni kwa vijana 60 tu........wasiliana na uongozi wa vijana mahali ulipo au waone viongozi wa Jumuiya yako.

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR