Wednesday, July 18, 2012

HISTORIA YA VIWAWA KIDUNIA.
Viwawa ilianzishwa mwaka 1924 mji wa Brussel nchini Ubelgijina Padri Joseph Cardjin na kupitishwarasimi na kama chama cha kitume cha vijana Kimataifa na Balaza la Kipapa Vatican mwaka 1950.Padri Joseph Cardjin pia alianzisha YCS,hivyo VIWAWA Na YCS alianzisha yeye.Makao makuu ya VIWAWA Duniani yako Roma-Italia chini ya Rais Seraphina kutoka Korea,Katibu Mkuu Jules Adached toka Bejin,Mhazini Lisa Vaccariano toka Italia na Mratibu wa kimataifa Arniel Iway toka Philipini na mshauri Pd.Joseph Ramaguera toka Spain. 
 HISTORIA YA VIWAWA TANZANIA.
Viwawa Tanzania iliingia mwaka 1959 katika Parokia ya Msimbazi,Jimbo kuu la Dar es salaam chini ya Mwanzilishi Padri Hendrikus Johannes Brinkhof maarufu kama Padri Mansuetus na kupitisha rasimi chama cha Kitume cha Vijana na Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) mwaka 1979.Baada ya kupitisha hapo kilitambulishwa pote Tanzania kama chama cha Vijana Wakatoriki Wafanyakazi Tanzania(VIWAWA).
Mpaka sasa chama hiki kip ,kuanzia ngazi ya Jumuiya,Mtaa,Kanda,Kigango,Parokia,Kijimbo,Taifa na Kimataifa.

1 comment:

  1. NAMI KAMA M/MWENY.KITI
    Nawahimiza kujitokeza kwa wingi ili tuweze kupata kile ambacho roo mtakatifu amewaongoza wao kuandaa kwa ajili yetu.

    ReplyDelete

NCHI YANGU FAHARI YANGU TOUR